SoC04 Tanzania tuitakayo baada ya miaka sita kufikia 2030 ni kufuta mimba za utotoni na ndoa za utotoni

SoC04 Tanzania tuitakayo baada ya miaka sita kufikia 2030 ni kufuta mimba za utotoni na ndoa za utotoni

Tanzania Tuitakayo competition threads

JOHNGERVAS

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2016
Posts
1,011
Reaction score
1,681
TANZANIA TUITAKAYO BAADA YA MIAKA MITANO NI KUTOKEMEZA MIMBA Z A UTOTONI NDOA ZA UTOTONI KWA KUANZISHA NA KUIMARISHA MITANDAO YA KIJAMII NA KISHERIA AMBAYO INASHUGHULIKIA UKATILI WA KIJINSIA, KUFUTA HAKI FULANI ZA KIJAMII AU KISHERIA KWA WAHALIFU WA UKATILI WA KIJINSIA, KAMA VILE HAKI YA KUWANIA NAFASI YA UONGOZI AU HAKI YA KUSHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA KIJAMII AU HAKI NYINGINE

watototoo.jpg

CHANZO JAMII 360.


N.B Kwenye andiko langu nitazungumzia zaidi mimba z autoto kwa sababu mimba za utotoni zinasababishwa kwa kaisi kikubwa na ndoa za Utotoni.

UTANGULIZI

Mimba za utotoni ni pale binti anapopata mimba kabla ya kutimiza miaka 18.

Wataalamu wa afya ya uzazi wanashauri ili kuepukana na matatizo ya kiafya ni vyema kupata mimba baada ya kufikisha umri wa miaka 18. Inatajwa kwamba, chini ya miaka 18 wasichana bado hawajakomaa kiakili na kimwili.

Kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto namba 21 ya mwaka 2009 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019, mtoto ni mtu yoyote aliye chini ya umri wa miaka kumi na nane

Tatizo la mimba za utotoni ni suala kubwa nchini Tanzania na katika nchi nyingine nyingi duniani. Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni, asilimia kubwa ya wasichana huanza kushiriki ngono katika umri mdogo sana na hii mara nyingi husababisha mimba za utotoni.

MIMBA ZA UTONI.jpg


PICHA KWA MSAADA WA MTANDAO WA WABUNIFU MEDIA

Kwa mujibu wa Takwimu msingi zinazotolewa na Ofisi ya Rais,Tawala za mikoa na serikali za mitaa Kumekua na ongezeko la mimba za utotoni zimekuwa zikongezeka mwaka hadi mwaka ambapo hadi mwaka 2019 kulikuwa na ongezeko la 57% la wanafunzi a sekondari walioacha shule yaani wanafunzi 5398 ukilinganisha na 3439 mwaka 2015.

Kama ambvayo zinaonekana kwenye Jedwali hapa chini

mimba-pc.jpg

CHANZO TOVUTI YA MWANANCHI.

Lakini pia hivi karibuni huko mkoani Songwe kuliripotiwa kwamba watoto 194 wenye umri chini ya miaka 18 walipata ujauzito huko mkoani songwe kwa kipindi cha mwezi mmoja.




SOURCE SONGWE TV I

October mwaka Jana
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza katika uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na viashiria vya Malaria Tanzania ya mwaka 2022 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam Alisema kwamba Ripoti hiyo imeonesha mikoa inayoongoza mimba za utotoni ni Songwe asilimia 45, Ruvuma asilimia 37, Katavi asilimia 34, Mara asilimia 31 na Rukwa asilimia 30.

Hali ni mbaya sana kwa sana licha ya jitihada mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanywa na serikali lakini bado tatizo linaonekana kuwa ni kubwa sana.

Wanafunzi wengi wamekatisha ndoto zao za Elimu kwa sababu ya mimba za mapema, lakini pia hata wale ambao hawasomi wameshindwa kufikia malengo yao ya kiamisha.

Mimba za utoni na ndoa za utoto ni suala sugu sana hapa Tanzania kama zinavyooneka kwenye jedwali hapa chini.

NDOA ZA UTOTONI.jpg


CHANZO TANZANIA WEB

MADHARA YA KIAFYA NA KITAALUMA


Mimba za utotoni huathiri afya, elimu na haki za mtoto wa kike. Mtoto wa kike asiye na elimu atakuwa na ugumu kupata ajira na kujijengea maisha bora na familia yake.

Wataalamu wa afya ya uzazi wanashauri ili kuepukana na matatizo ya kiafya ni vyema kupata mimba baada ya kufikisha umri wa miaka 18. Chini ya miaka 18 msichana bdo hajakomaa kiakili na kimwili kuweza kubeba majukumu ya malezi,pia nyonga huwa changa na nyembamba hivyo kutoweza kubeba kiumbe na kusababisha madhara makubwa wakati wa kujifungua.

Madhara mengine ya kiafya yatokanayo na mimba za utotoni ni kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua,Fistula(kutokwa na haja ndogo),kifafa cha mimba na vifo vya mama na mtoto.

NINI CHANZO CHA MIMBA ZA UTOTONI NCHINI TANZANIA?

Chanzo cha mimba za utotoni nchini Tanzania ni pamoja na mambo mengi, lakini baadhi ya sababu kuu ni pamoja na;Elimu duni kuhusu afya ya uzazi: wengi hawapati elimu sahihi kuhusu afya ya uzazi na njia za kuzuia mimba. Hii inaweza kusababisha kutokuwa na habari sahihi na kufanya maamuzi yasiyo sahihi.

Ukatili wa kijinsia; Ukatili wa kingono dhidi ya watoto na vijana ni tatizo kubwa. Watoto na vijana wanaweza kubakwa au kuingiliwa kingono na watu wa umri mkubwa, ikisababisha mimba za utotoni.

Umaskini;Familia maskini mara nyingi hawana rasilimali za kutosha kumudu huduma za afya ya uzazi au elimu. Vijana katika mazingira haya wanaweza kuwa katika hatari zaidi ya kushiriki ngono mapema na kupata mimba.

Mila na tamaduni; Baadhi ya tamaduni zinaweza kuweka shinikizo kwa wasichana kuolewa na kupata watoto katika umri mdogo.

Upatikanaji mdogo wa huduma za afya; Vijana wanaweza kukosa upatikanaji wa huduma za afya ya uzazi, ikiwa ni pamoja na kupata kondomu au upatikanaji wa dawa za kuzuia mimba.

NINI KIFANYIKE ILI KUMALIZA KABISA TATIZO LA MIMBA ZA UTOTONI TANZANIA?

Kupambana na ukatili wa kijinsia ni moja ya hatua muhimu katika kumaliza tatizo la mimba za utotoni nchini Tanzania. Hii inahusisha hatua za kisheria, elimu, na mabadiliko ya kitamaduni ili kujenga jamii salama na yenye usawa. Fafanuzi zaidi:

Sheria kali dhidi ya ukatili wa kijinsia: Kuweka sheria kali zinazolinda watoto na wanawake dhidi ya ukatili wa kijinsia, ikiwa ni pamoja na adhabu nzito kwa wanaovunja sheria hizo. Sheria hizo zinapaswa kutekelezwa kikamilifu na kwa ufanisi,
.

Elimu kuhusu haki za kibinadamu na ukatili wa kijinsia: Kuweka mipango madhubuti ya elimu katika shule na jamii kuhusu haki za kibinadamu, ukatili wa kijinsia, na njia za kuzuia na kuripoti vitendo vya ukatili.

Kuboresha huduma za kisheria na kijamii: Kuhakikisha upatikanaji wa huduma za kisheria na kijamii kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia, ikiwa ni pamoja na vituo vya kutoa ushauri nasaha, huduma za afya, na mahakama zinazoshughulikia kesi za ukatili wa kijinsia.

Kuelimisha jamii kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia: Kuendeleza kampeni za elimu katika jamii kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia kwa waathirika, familia zao, na jamii kwa ujumla ili kubadilisha mitazamo na kukomesha ukimya unaozunguka suala hilo.

Kuimarisha mtandao wa kijamii na kisheria: Kuanzisha na kuimarisha mitandao ya kijamii na kisheria ambayo inashughulikia ukatili wa kijinsia, ikiwa ni pamoja na mashirika ya kiraia, asasi za kisheria, na mashirika ya kutoa misaada.

Kosa lolote la ukatili dhidi ya mtoto litungiwe sheria kali na utekelezaji wake ufanyike na kuonekana umefanyika.

MWISHO NI JUKUMU LETU SOTE KUPINGA VITENDO VYOVYOTE VYA UKATILI WA KIJINSIA, UKATILI WA WATOTO NA KUTOA ELIMU YA UZAZI KWA WATOTO SAMBAMBA NA KUJILINDA NA KUWALINDA WATOTO DHIDI YA AMGONJWA YA ZINAA IKIWEMO UKIMWI.

MANDISHI YOHANE GERVAS MASSAWE
EMAIL @Yohanegervas@gmail.com
 
Upvote 8
Back
Top Bottom