SoC04 Tanzania tuitakayo: Bunge Mbadala kwa ukomavu wa kidemokrasia nchini

SoC04 Tanzania tuitakayo: Bunge Mbadala kwa ukomavu wa kidemokrasia nchini

Tanzania Tuitakayo competition threads

KISHOMBO

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2012
Posts
206
Reaction score
38
Utangulizi

Tanzania kama zilivyo nchi za Jumuiya ya Madola zina mfumo wa uwakilishi wa wananchi unaofanana kwa asilimia kubwa. Hata kanuni, miongozo na sheria zinazotumika kwenye mabunge ya nchi hizi zinafanana. Ni mfumo wa miaka mingi ambao chanzo chake ni tawala za kifalme za nchi ya Uingereza

Katika bunge la Tanzania asilimia zaidi ya 90 % ya wabunge wanatoka chama tawala (CCM) na kuna idadi ndogo sana ya wabunge kutoka kwenye vyama vya upinzani au vyama mbadala. Kutoka na mazingira haya kumekuwepo na kero na manung’uniko kadha wa kadha kwamba inaonesha bunge la Tanzania limeodhiwa na CCM kwamba limetekwa na chama tawala

Pia tumeshuhudia namna chaguzi zetu zinavyofanyika mara nyingi huacha malalamiko kutoka kwa watu wa upinzani kwamba chaguzi nyingi zinakiuka misingi ya kidemokrasia, haki na utawala bora. Kuna malalamiko ya kuibiwa kwa kura, matumizi ya vyombo vya serikali wakati wa uchaguzi, mizengwe na mambo kadha wa kadha

Pia tunashuhudiwa namna ya uendeshaji na utoaji hoja kwa wabunge wetu ndani ya bunge tulionalo kwa sasa. Pamoja na kwamba kuna idadi ya wawakilishi wachache kutoka kwenye vyama vya upinzani bado wanakumbana na hoja za wingi wa wabunge kutoka Chama cha Mapinduzi

Changamoto iliyopo: Changamoto kubwa iliyopo ni kwamba taswira ya bunge letu tulionalo ni kwamba kuna dalili ya kuminywa kwa demokrasia na haki kwa upande wa vyama mbadala kutokana kwamba kanuni za kupitisha hoja ndani ya bunge ni mfumo wa kula nyingi, ambavyo kwanamna ya wingi wa wabunge wa CCM ni ngumu kupitisha hoja ya upande wa hoja mbadala

Pia kuendelea kuwa na bunge la namna hii kutaendelea kuwepo na manun’guniko yasiyo na lazima kutoka kwa wananchi. Pia kutaendelea kutoa taswira mbaya kwa serikali maana kutafsiriwa kwamba serikali inaminya uhuru wa kujieleza. Kama nchi iliingia kwenye mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 basi hoja ya kuwa na bunge mbadala haiepukiki

Tunaweza kuwa tofauti: Katika dunia ya maendeleo ya sasa ambapo binadamu wanaendelea kuvumbia vitu katika ulimwengu uliyostaraabika tunaweza kuanzisha mifumo yetu ya kidemokarasia ambayo nchi nyingine duniani zije kujifunza kwetu.Tunahitaji kuwa na mifumo yetu ambayo inaendenda na mazingira yetu ya kidemokrasia

Bunge mbadala: Hili ni bunge la wawakilishi wa vyama kutoka upande wa upinzani.Hili bunge si la kikatiba ni bunge litakalo jadili masuala yote ikiwemo bajeti mbadala kwa uwazi kabisa. Ni bunge ambalo litakaa mara 3 kwa mwaka. Bunge hili litajihusisha na kusoma bajetii za vyama vya upinzani kwa uwazi kupitia vikao vitatu kwa mwaka. Katika bunge hili wapinzani watakuja na bajeti zao, watachagua spika wao wa kuendesha vikao, watasoma bajeti zao na kuja na mbadala wa bajeti za kisekta.

Katika bunge hili wabunge hawa watapatikana kwa kupitishwa katika vyama vyao au watapatikana baada ya uchaguzi mkuu wa wabunge. Katika uchaguzi mkuu wa wabunge tunaweza kuja na utaratibu wa karatasi ya kupigia kura tukaongeza jina la mbunge mbadala yaani kama mtu atachagua mbunge wa CCM kwa ajili ya kwenda kwenye bunge kuu, basi awe na haki ya kuchagua pembeni mbunge mbadala wa bunge mbdala

Kupitia bunge hili tunataraji hoja zenye mashiko, zenye uchambuzi wa hali ya juu. Hatutarajii bunge hili kuwa la mipasho na kashfa kwa serikali iliyopo madarakani. Tunahitaji kushuhudia wabunge wakinoa bongo zao na kutoa mbadala wa changamoto zinazolikumba taifa

Kwa utaratibu huu wa kupata mbunge mbadala kutasaidia kuimarika kwa demokrasia, kupanua wigo wa ushindani katika siasa za nchi, kuongeza ubunifu kwenye vyama vyetu vya siasa, pia kutaongeza wigo wa kupata wawakilishi wenye weledi na wacahapakazi kwa ajili maendeleo ya nchi.Kwa kuwa uwakilishi utakuwa wazi basi bunge hili litasaidia chama cha CCM kuteua wawakilishi wenye weledi zaidi ambao wakakuwa na kazi ya kushindanisha hoja na wenzao wa upande wa upinzani

Pia kupitia bunge hili tunatarajia kupunguza malalamiko ya siyo ya lazima kwa serikali kwamba serikali inaminya demokrasia

Aidha katika bunge hili hatutarajii kujenga bunge jipya maana vikao vya bunge hili ni baada ya vikao rasmi vya bunge kuu kukaa. Wabunge hawa wanaweza kutumia majengo yaliyopo na mikutano yao itarushwa mbashara ili kila mwananchi aweze kufuatilia

Kupitia bunge hili kutasaidia wananchi kuwafahamu zaidi uwezo wa wakilishi wao kwenye majimbo yao.

Pia kutokana na uwakilishi wa namna hii kutasaidia mawaziri wa sekta mbalimbali kuchukua hoja zenye mashiko katika kuboresha mipango yao katika kutekeleza bajeti

Mwisho: Wabunge wa bunge hili watapata posho tu za vikao kwenye vikao vitatu ndani ya mwaka. Hawatapewa malupulupu mengine au kiinua mgongo
 
Upvote 1
Yaani unamaanisha kama tulivyo na mawaziri vivuli, ndio tuwe na wabunge vivuli?

Sasaa, kama watakaa kivyaovyao itatusaidiaje katika kuzinoa hoja zinazotolewa bungeni (kuzichallenge)
 
Back
Top Bottom