SoC04 Tanzania tuitakayo by Yasam Legend

SoC04 Tanzania tuitakayo by Yasam Legend

Tanzania Tuitakayo competition threads

Yasam legend

New Member
Joined
Jun 3, 2024
Posts
1
Reaction score
1
Ni mengi yapo katika jamii yetu( nchi yetu) ambayo ni nyenzo kubwa katika maendeleo ya nchi yetu na jamii kwa ujumla. Kuna vipengele mbali mbali kama uchumi, sayansi na teknolojia, siasa, afya na mengi neyo mengi. Kwa upande wangu nitaelezea baadhi kulingana na upeo wangu na maono yangu.

KIJAMII NA AFYA
Ni malengo kwa kila mwananchi kupata huduma bora za kijamii ususani huduma bora za matibabu. Kwa miaka michache ijayo ninge pendekeza kuwepo kwa bima ya afya kulingana na kipato cha mtu anacho kipata pia kulingana na mahitaji yake, uwepo wa sheria kila mtanzania awe na bima, lakini changamoto kubwa ni kuwa wengi wenye hali ngumu za maisha awawezi kukidhi au kufikia malipo ya kila mwaka. Mtu mkulima mdogo mdogo ana shamba dogo na mauzo yake yanatosha yeye na familia yake basi kuwe na asilimia ambazo mkulima huyu atalipia ili kupata huduma ya bima ya afya.

Pia nimeona changamoto kwenye kuwasilisha kadi za bima ili kuthibitisha kwamba mtumiaji ni mtu sahihi mana kuna baadhi huwa wanachangia bima moja. Hivyo kuwe na mfumo wa finger print ambo kila mtumiaji wa mfuko wa bima atasaini kila anapo pata huduma ya afya, hii itasaidia kupunguza asala inayotokana na matumizi mrudio kwa watu wawili tofauti kwenye kadi moja ya bima.

Kwa teknolojia hiyo pia itasaidia kujua moja kwa moja muhusika ni mfanyakazi wa wapi na anapaswa kulipa asilimia kiasi gani kwa kila mwaka kulingana na kipato chake kwasababu finger print inabeba taalifa zote za mtu tofauti na mfumo wa kutumia nida namba ambazo aziwezi kutambua mabadiliko ya masisha ya mtu.

Nida inaonyesha ulikuwa mkulima lakini baada ya miaka miwili hali ikabadilika na ukawa muuza genge au mchoma mahindi nida number aiwezi tambua uhalisia.
Kwa upande wa technology. Kiuhalisia kuitazama kwa kiasi kikubwa utaona upande wa technology tumepiga atua japo kidogo lakini bado tunahitaji mabadiliko mengi na yaliyo bora.

Teknolojia ya ujenzi, ni barabara nyingi utakuta zina mashimo na matuta yaliyo tengenezwa baada ya kupita mahali au vyombo vya usafiri vyenye uzito mkubwa ukilinganisha na ubora wa barabara. Mfano mzuri ni TUNDUMA ROAD, kutoka MBEYA kwenda tunduma kupitia iyunga, MOROGORO - DODOMA ROAD UKIANZIA MSAMVU STENDI KUTOKEA ROUND ABOUT na zinginezo nyingi za mikoani ambao zinahitaji ubora na maboresho.

Nini kifanyike ili kuepuka tatizo hili??, kwanza kabisa ni mkandarasi, mkandarasi awe na ujuzi wa kuchagua materials ambayo yanafaa na yenye ubora kulingana na matumizi ya barabara husika, tunawezaje kujua kuwa mkandarasi anastahiki kupewa kazi, basi tufanye ukaguzi na majalibio kwa makandarasi wote wa serikali kujua ni wapi wanastahiki na wapi hawastahiki, mfano madarasa ya liyojengwa na babu zetu ambao hawakuwa na elimu kipindi cha mjerumani miaka zaidi ya 80 iliopita si ajabu unaweza usikute shimo ndani ya darasa, lakini leo darasa linaweza kujengwa likiwa na miezi sita tu utaona mashimo yanaanza kutokea ndani ya darsa na kusababisha vumbi. Chanzo ni ukosefu wa ubunifu na kutumia vifaa duni au ubadhilifu kwa kutokuwa na wakandarasi wenye uwezo. TANZANIA TUITAKAYO, Ni kuwa na miundombinu bora za usafirishaji kwa kuwa kuzingatia yafuatayo.

1. Mizani zimewekwa barabara za mikoani, na kuacha barabara za ndani ya mikoa zikiwa mbovu hii ni kutokana na madereva na wamiliki wa vifaa vya usafirishaji kubeba mizigo mizito kuzidi uwezo wa barabara na kusabisha mashimo na mwisho kuipa serikali hasara ya matengenezo ya mala kwa mla ( hivyo kuwe na mizani nandani ya mikoa kwa magali yanayo beba mizigo mizito ili kulinda viwango vya barabara)

Ajali za barabarani ni nyingi mno, mbazo zingine ni zinatokana na uzembe wa madereva hasa kutumia mwendo makubwa ( speed) hi ni kutokana na ukosefu wa vifaa vya kupima speed ( speed tracker) katika barabara nyingi za nchi yetu, hivyo kusababisha ajali zisizo za laizma. ( Hivyo ichukuliwe tathmin, kuweza kuweka katikati ya majiji na mikoa vifaa na kamera zinazo nasa speed ya kila gali pia itasaidia kupunguza ushahidi ( ushuhuda ) wa uongo pindi ajali inapotokea ili kuwaokoa na wanyonge wasio na hatia kupakaziwa kesi za kusababisha ajali

3. Uwepo wa traffic Barabarani imeonekana kuwa changamoto badara ya kuonekana ndio usalama hii ni kutokana na uwepo wa rushwa. Kwa upande wangu naona tukimtoa traffic tuweke robot ni kusabisha kuongeza wimbi la ukosefu wa ajila nchini ila mbadala wake, unaweza kumtumia traffic akiwa amevaa voice record device, kifaa ambacho kinarecord sauti ndani ya masaa 24, au kinaweza kusetiwa kulingana na muda traffic anao kaa barabarani. Kufaa hivyo litalazimika kiwa on( kimewasha) na kurekodi mazungumza yote yatakayo fanyika barabarani kati ya traffic na watumiaji wa vyombo ya usafili. Na settings zote za kifaa zinatakiwa ziunganishwe moja kwa moja na kituo kikuu cha mkoa ambacho kitakagua kila kifaa na mzungumzo yake. Iwapo kama traffic atakizima hivyo kifaa basi mako makuu watajua basi atatakiwa aeleze sababu ya kuzima kifaa hicho. Vinginevyo adhabu au faini itatolewa .

Kwa upande wa uchumi, ni dhali na lengo letu kuwa fedha ipande thamani, na ili kupanda thamani lazima uwe inatumika katika masoko nje na ndani ya nchi. Namna gani tutafanikisha hili!!, tutoe sapoti kwa wakulima wadogo kufikia kilele cha wakulima wa daraja la kati ili kuongeza uzalishaji, baada ya hatua hiyo kuongezwe viwanda kulingana na mahitaji ya nchi, atuwezi sema tunashida na sukari alafu serikali ijaze titi kwenye ukulima wa pamba na kujenga viwanda vya nguo na viwanda vya tumbaku. Bila kusahau wawekezaji wanakuja kulingana na miundombinu kama luvyo eleza wali iwapo **** zitawekwa kwa usawa na ubora basi ni dhahiri kuwa ata shilingi itapanda kwasababu wawekezaji ni nyenzo katika kuizungusha pesa.

Uboreshaji wa masoko ya ndani ya nchi ni dhahiri hulenga moja kwa moja udhamini kutoka nje, hivyo ongezeko la fedha za kigeni na matumizi na mahitaji makubwa ya shilingi yataongezeka hivyo kuitangaza zaidi katika soko na kuleta ushindani ndani na nje ya Afrika Mashariki.

Kujaza titi kuuza mazao ya biashara zaidi nje ya nchi kuliko mazao ya chakula. Kwa miaka mitano ijayo au 25 ijayo nina matumaini kwa hali hii Tanzinia haitakuwa na neno linalo itwa " NJAA" AU " UKAME". Tuna lima sana lakini kuwe na kiwango maalumu ambacho akitakiwi kuzidi ili kuweza kuilinda nchi. Tusiwe tukipata kidogo tu na kimezidi kidogo tu basi tukiuze la ( Japan), tuongeze mikakati, kuna nchi zinalima mpaka juu ya maghorofa na uwezi kusikia neno " NJAA" Japo wana ardhi ndogo sana lakini mikakati ya kulinda chakula kisitoke nje ya nchi ni mikubwa kiasi kwamba kinawatosheleza wao kama wao

Elimu. Kiukweli kwaitaka maisha yote katika nchi yoyote mzizi mkubwa wa MAALIFA ni "MWALIMU ", basi tuwathamini na tuiyone thamani yao. " Migomo yao ya kugoma kufundisha kisa mishahara na ukosefu wa miundombinu bora za ufundishaji". Bila mwalimu kusingekuwa na wimbi kubwa na kupunguza ujinga kwa vijana. Kwa miaka ijayo nadhani ni vyema kuwatizama mala mbili mbili na kutatua changamoto zao na mazingira yao ya kuishi ikiwemo yafuatayo.

1 . Mishahara yenye kukidhi mahitaji yao na familia zao( sio individual) tukumbuke nao wanategemewa na familia zao.

2. Kujenga makazi bora ya walimu ( tena kukaa bure) bila kulipia gharama yoyote ya makazi kwani huongeza motisha na kuwapa hamasa vijana wanaojua ili ualimu uwe ndio chaguo lao la kwanza na kuipa kazi ya ualimu kipaumbele kwenye fikra zao, hii itasaidia kuongeza idadi ya watu wenye MAALIFA pia kuondoa kabisa tatizo la ajira. Iwapo kama vijana watajikita moja kwa moja kwenye uhandisi na udaktari , data science na telecommunication je nani atakaye mfundisha mtoto wa mwaka 2050 na 2080?

Tuliangalie na hili mana walimu wazoefu wanaisha kila siku ( either kwa vifo, kuzeeka, kustaafu, magonjwa, kukata tamaa na kuacha kazi na kuingia kwenye biashara) na mengineyo mengi .

3. Miundombinu za madarasa. Elimu bora haitokani na kuwa na mwalimu bora mwenye kukidhi vigezo ambaye anakula sifa, ila kwa upande mwingine mazingira pia yanasaidia kukuza uelewa wa mwanafunzi na kukuza ubunifu, kuna wanafunzi wanasoma sekondari wanaambiwa sheria za kuingia laboratory ni hizi eg. Do not touch any chemical in the laboratory without permission from your instructor ( teacher), lakini mwanafunzi huyo huyo hajui hata iyo laboratory inaonekanaje, wala ajui chemical ni kitu gani hasa, hivyo kwa matarajio yangu miaka ijayo mbeleni TANZANIA TUITAKAYO iwe na utoaji elimu kwa vitendo kwa kila shule kuwe na maktaba zenye vitabu vya kutosha, maabara zenye uwezo wa kubeba vitu vingi na kuingiza wanafunzi wengi ili kuhakikisha kila mwanafunzi anapata elimu sahihi.

4. Wanafunzi wengi wanapata ujuzi mitaani ni kweli ( kwakuwa wanaishi day students ) lakini kiuhalisia wanafunzi wengi wanaalibikia mitaani, kuwepo na ongezeko la shule za bweni ili kupunguza idadi ya wanafunzi wanao iga tabia mbovu ambazo azifai katika jamii na kimaadili.

5. Elimu ni pana mno, ina jambo la mwisho ningependa kuzungumzia kwenye kipengele cha elimu ni MTIHANI, mfano mitihani ya kufuzu Aku kumaliza level furani nalenga zaidi kuanzia kidato cha nne mpaka chuo kikuu. Ni kweli mtihani wa mwisho ni muhimu sana lakini embu utizame kwa upande wa pili athali yake, unaweza kuwa na kijana anauwezo darasani na anafanya vizuri toka akiwa form one lakini kwa bahati mbaya huyu kijana akateleza kwenye mtihani wa mwisho wa form four, je tunampeleka wapi huyu kijana ??.

TANZANIA TUITAKAYO MIAKA ijayo tunahitaji Kila mwanafunzi agaiwe ufauru wake wa mwisho kulingana na mitihani alioyoianya kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne ukijumuisha na mtihani wa mwisho Ambi upewe asilimia atleast 40, ila 60 zitoke kwenye mitihani ya ndani hii itasaidia kuwacha kuwapoteza wale wenye malengo alafu mtihani wa mwisho ndio umempoteza. " MTIHANI NI MTIHANI" kama jina linavyo jieleza ila tukumbuke ataile tuliyofanya tukiwa ndani ya shule pia nayo ni mitihani iweje iwekwe pembeni na kutizamwa mtihani mmoja ambao una low impact??, je lengo la kufanya ile mitahani ya shule ni kwajili ya kutufanya tuwe na uzoefu?, je uzoefu huo uko wapi kama kila somo lina content na maswali yanabadilika??, nini faida ya mitihani ya shule? Kujenga madaraja? No, Tanzania TUITAKAYO iangalie na lile jasho analopoteza mwanafunzi , nateseka usiku na mchana kwa mitihani ya shule, ila mwisho wa siku mtihani mmoja tu ndio unampotezea jasho lake lote.

AJIRA: wanafunzi wengi wa vyuo mbalimbali nchini, wanamaliza kila mwaka lakini bado akuna mfumo sasahihi au mfumo mzuri ambao utawawezesha kupata ajira kwa urahisi. Nini kifanyike??

1. Kwa kila chuo kuunganishwe na sekta binafsi na za kiserikali kulingana na kozi husika ambazo chuo kinafundisha. Kila sekta itatoa vigezo na masharti ni mwanafunzi mwenye sifa gani anatakiwa na awe na ufauru gani, kisha wanafunzi wataandaa maombi na kuyakabidhisha chuoni alafu chuo kitachukua maombi yote cv za hao wanafunzi na kupeleka kwenye sekta husika. Hapo sekta itaamua nani aitwe nani aachwe nani aingie interview. Hii itasaidia kwa kiwango kikubwa wanafunzi kuomba ajila sehemu ambazo awastahiki kupeleka maombi. Kuna vijana wanasoma na wanamaliza lakini bado awahui iyo ajira anatakiwa akombe kwenye sekta gani.

VYUO VINGI VYA ENGINEERING, Wanafunzi wake wana masomo mengi zaidi, na kazi zinakuwa nyingi zaidi ukilinganisha na kozi zingine, mikopo wanayopata kwaajili ya maradhi na chakula ndio wanatumia kununua vitivo, kukamilisha project za ndani ( katika module wanazo soma), pesa hiyo hiyo atumie chakula, maradhi bado anachangamoto binafsi, kiuhalisia haitoshelezi kabisa na kukuta mwanafunzi yupo kwenye hali ngumu ya maisha akiwa bado yupo chuoni. Je nini kifanyike, Tanzania TUITAKAYO mwanafunzi wa chuo anaye soma engineering atleast kila mwanafunzi awe anapatiwa pesa ya vitivo na class works hii itasaidia mwanafunzi wa chuo kuacha ku focus moja kwa moja katika masomo na kuingia mtaani kutafuta pesa ili kukidhi mahitaji yake na ya darasani. Na mwisho wa siku mtoa ajira ( serikali) atapanga kwa kila coz kiwango chake cha ufauru ( GPA) ili mwanafunzi aweze kuajiliwa, na utakuta kwa kiwango kikubwa engineering wana GPA za chini , je kwanini?, ni ngumu? Yeah, ugumu upo ila kwa kiasi kikubwa ugumu unasababishwa na wanafunzi wengi ku focus zaidi na kipato ( maokoto) ila waweze kukamilisha kazi na mahitaji yao na hapo ndio utaondoa darasa ni gumu.

HIVYO BASI, Tanzania TUITAKAYO ni ile mambao itasikiliza kile wananchi wanachi kihitaji na kama mahitaji yana tija na positive resurts basi yafanyiwe kazi ili kulijenga taifa. ALWAYS TOGETHER WE CAN
 
Upvote 6
Back
Top Bottom