WAPEKEE_
Member
- May 23, 2024
- 21
- 28
TANZANIA TUITAKAYO : ELIMU YA VYUO VYA UFUNDI IWE LAZIMA KISHERIA KWA VIJANA WOTE WANAOSHINDWA KUENDELEA ELIMU YA JUU.
UTANGULIZI.
Awali ya yote nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, niwapongeze sana jukwaa la JAMII FORUMS, kwa kuanda shindano hili la kibunifu zaidi na lenye tija ya kitaifa kwa miaka 25 ijayo ambayo kimsingi inakaa kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Tanzania.
NGUVU NA UMUHIMU WA ELIMU YA UFUNDI
Kwasasa nchi ya China na Mataifa yaliyoendelea yamewekeza zaidi kwenye ELIMU TAALUMA NA ELIMU UFUNDI, huku bunifu zote zikipewa kipaumbele na nguvukazi kushindana kwenye soko la ajira la ndani na baadae kwa weredi mkubwa kupeleka bidhaa hizo za kibunifu kwenye soko la nje na kimataifa.
Uchumi wa nchi zilizoendelea, unabebwa na siri ya uchumi wa viwanda na biashara. Na watendaji wa wake ni wale ambao waliopikwa na tasnia ya ELIMU. Kwani rasilimali watu katika sekta hii ni wale ambao wana ujuzi na taaluma ya kuendesha mitambo, kubuni bidhaa, kuitumia sayansi na teknolojia kwa weredi, na ujuzi wa biashara na masoko ambayo inakamilisha mnyororo wa thamani na kuleta maendeleo makubwa ya kimaendeleo.
Tanzanaia Elimu ya ufundi na ubunifu inatolewa kwenye ngazi za vyuo vya ufundi na vyuo vikuu. Huku ndio kunapaswa kuwandaa watendaji na rasilimali watu watakaokuwa kwenye ushindani wa uchumi duniani.
Kwenye Dira ya Maendeleo ya Taifa kwa miaka 25 ijayo (2050) na Mipango ya Muda Mrefu ya Maendeleo naiomba sana nchi yangu kuwekeza kwenye Elimu ya Ufundi na Mafunzo ili watanzania wengi zaidi waingie kwenye soko la ajira, biashara na mzunguko wa kiuchumi wa taifa letu wakiwa wanaelimu na wanaendelea kujielimisha ili wawe mahiri na wabobevu.
ELIMU YA UFUNDI STADI IWE LAZIMA KISHERIA
Ni wazi kuwa elimu ya Tanzania, kwa miaka zaidi ya 50 iliyopita, imekuwa elimu ya NADHARIA zaidi kuliko vitendo. Bado elimu yetu haitoi wataalamu wa kutosha kwenye nyanja mbalimbali .
Hivyo basi ,Elimu ya ufundi stadi kupitia vyuo vya ufundi iwe lazima kisheria na hasa katika ule mzunguko wa elimu unaoanzia, Awali, Msingi, Sekondari na hapo katikati iwe ni Vyuo vya ufundi kwa wale ambao hawatafanikiwa kwenda vyuo vikuu , na ikijumuisha wale wanaoishia kidato cha sita, waende moja kwa moja vyuo vya ufundí. Hata wale ambao wanafeli kabisa kidato channe na sita, wote wawe wananafasi na uwezo wa kwenda vyuo vya ufundi.
Hivyo katika mabadiliko mapya haya ya sera ya elimu , suala hili litiliwe mkazo kutungiwa sheria bungeni na ipitishwe kwa kusainiwa na Raisi ili tudhihirishe kwa dhati kuwa tunataka kweli Tanzania ijayo iwe ya uchumi wa viwanda na uchumi mkubwa wa juu duniani.
VYUO VYA UFUNDI VIWE NA ELIMU YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Vyuo vya ufundi visitoe tu elimu ya ufundi stadi , ijumuishe na elimu ya sayansi na teknolojia. Tupo kwenye karne ya teknolojia ambayo kwa miaka 25 ijayo, nilazima kila kijana awe ana ujuzi na maarifa ya masuala ya kidijitali . Kwasasa kila sekta ya kimaendelo ipo kidijitali zaidi ambapo tukisema elimu hii itolewe vyuo vikuu pekee, basi idadi kubwa ya vijana watabaki nyuma na kuachwa na kasi kubwa ya maendeleo.Hivyo masuala ya sayansi na teknolojia yawe ya lazıma kwenye mitaala ya vyuo vya ufundi.
VYUO VYA UFUNDI VIWE NA ELIMU YA VIPAJI NA SANAA
Elimu ya miaka 5 mpaka 25 ijayo itoe mafunzo ya vipaji, sanaa, ubunifu na ugunduzi ili kuwaendeleza, kuwatambua na kuwarasimisha vijana ili waweze kujiajiri na kujielimisha katika safari yao ya maisha. Leo tunaona wazi jinsi watu wenye vipaji kama ‘Ramadhani Brothers’ wanasarakasi walioshinda tuzo na mamilioni ya fedha nchi za nie, wanamichezo kama kina Mbwana Sammata , wasanii kama Diamond Platnumz na wanariadha kama kina Alphonce Simbu, ambao wameonesha mafanikio makubwa kwenye vipaji, sanaa na michezo na kuchochoea ukuaji wa maendeleo ya taifa kwenye tasnia hizo.
Badala ya kuwapata watu kama hawa kwa bahati tu, tuwe na dhamira ya dhati ya kuwandaa kwa kutumia vyuo vya ufundi na vyuo vya kati na kuwarasimisha.
VYUO VYA UFUNDI VIPATIWE MIKOPO KWASABABU WAHITIMU WANAINGIA KWENYE AJIRA MOJA KWA MOJA
Kwasasa vyuo vya elimu ya juu tu, na sasa mapendekezo ya vyuo vya kati ndio wanapata mikopo pekee, lakini tuseme ukweli wengi wametumia pesa za mikopo na hawapo kwenye soko la ajira, na zile pesa zimepotea kwasababu hazipo kwenye mzunguko wa pesa kupitia ajira za taaluma zao.
Lakini leo wanafunzi wa vyuo vya ufundi wakikopeshwa, tuna uhakika kwa asilimia kubwa kurejesha pesa hizo kwasababu wahitimu hawa wana fursa kubwa ya kujiajiri na kurejesha pesa hizo kwa wingi kuliko hata hawa wa vyuo vikuu wanaoenda kwenye sekta za kitaaluma ambao kimsingi ni wachache.
SERIKALI ISHIRIKIANE NA SEKTA BINAFSI KUWEKEZA KWENYE VYUO VYA UFUNDI
Ili tupige hatua kwa haraka, serikali iwe na sera rafiki za kuruhusu uwekezaji kutoka sekta binafsi na uwekezaji kutoka nje ya nchi katika sekta ya elimu kama tunavyohubiri uwekezaji kwenye utalii, biashara, rasilimali na mikopo kutoka nje. Turuhusu na tuingie mikataba mikubwa na nchi zilizoendelea kama CHINA, MAREKANI, UFARANSA, URUSI, KOREA na mataifa yaliyoendelea kuja kujenga vyuo vikubwa vitakavyozalisha watanzania wenye ujuzi wengi watakao jiajiri ndani na nje ya nchi .
VIPAUMBELE VYA AJIRA NA TENDA ZA KAZI KWA WAHITIMU WA VYUO VYA UFUNDI
Kwa makusudi kabisa, tena kwa nguvu ya sheria lazima, matokeo na bidhaa inayotoka vyuo vya ufundi, wapewe kipaumbele kwenye ajira, kwenye kupewa tenda za kazi zinazohitaji stadi za kazi na taaluma za ufundi. Badala ya kuwapa tenda wageni, sasa ili kulinda rasilimali watu wa ndani tunaowazalisha wenyewe na kuchochoea ukuaji wao, sasa watu hawa wawe chaguo la kwanza kwenye kupewa kazi na tenda za kufanya ili kujipatia kipato na kurejesha ile mikopo waliyopewa wakiwa vyuo vya ufundi.
HITIMISHO
TANZANIA TUITAKAYO ni ile watanzania wana ujuzi, maarifa, taaluma na shauku ya mageuzi ya kiuchumi na kimaendeleo, ambapo kupitia elimu ya vyuo vya ufundi, vyuo vya kati na vyuo vikuu tutatengeneza watanzania wanaojiajiri zaidi kuliko kuajiriwa.
Hivyo mimi WAPEKEE KEPHAS YOHANA PAUL, naiomba sana serikali na wadau wote wa elimu na maendeleo kupitisha sera na sheria ya kufanya VYUO VYA UFUNDI VIWE LAZIMA KWA KILA MTANZANIA kwa mustakabari wa maendeleo ya Tanzania.
Wenu katika kulijenga taifa la Tanzania, WAPEKEE KEPHAS YOHANA PAUL

Upvote
1