Emilionare Suluti
New Member
- Jun 17, 2024
- 1
- 1
Elimu ni kurithisha au kuhamisha maarifa, ujuzi, taarifa au taaluma kutoka kizazi kimoja kwenda kingine.
Malengo ya elimu katika nchi yetu ya Tanzania kuanzia 2025 adi 2050 yawe ni
i. Kurithisha au kutoa maarifa na ujuzi kwa vijana yatakayoweza kuwakwamua katika lindi la umaskini na waweze kujitegemea kiuchumi
ii. Kuleta usawa, heshima na utu au ubinadamu
iii. Kuwaongezea vijana uwezo wa uzalishaji katika viwanda vidogo, au shughuli zao za uzalishaji ikiwemo katika kilimo, uvuvi, nk
iv. Kuwaandaa vijana kutumika katika nyanja mbalimbali za kiuchumi, kisiasa, na kijamii.
SHULE YA MSINGI
Napendekeza shule ya msingi ianzie chekechea adi darasa la sita na lihusishe watoto wenye umri kati ya miaka 4 adi 12.
Wanafunzi wafundishe maarifa ya awali ikiwa ni pamoja na kusoma, kuandika na kuhesabu. Na kuanzia darasa la tatu wanafunzi wasome masomo kama sayansi, historia, tehama, hisabati, na masomo ya lugha.
UJUZI MPYA
Kuanzia darasa la tano wanafunzi waanze kufundishwa kilimo na kila mwanafunz awe na bustani yake shuleni ambayo atakuwa anaihudumia. Somo hili na kilimo litafundishwa kwa nadharia na practical. Na mwishoni mwa masomo yake hapo darasa la sita wanafunz watatahiniwa pia katika somo hili kwa nadharia na vitendo hii itajenga wigo wa kuweza kujitegemea.
ELIMU YA SEKONDARI, KIDATO CHA KWANZA ADI CHA NNE
Hii itahusisha wanafunzi kuanzia miaka 13 adi 16 au 17. wanafunzi watasoma masomo kama biolojia, hisabati, kemia, kilimo, biashara, jiografia, historia, fizikia na masomo ya lugha
UJUZI MPYA
Katika hatua hii ya kidato cha kwanza adi cha nne. Wanafunzi wote wafundishwe ujuzi mbalimbali, wanafunzi wa kanda ya ziwa wote, na yale maeneo ambayo kuna maziwa, bahari wafundishe shughuli za uvuvi na namna ya kufanya biashara ya uvuvi, na hili lifanyike kwa nadharia lakini pia kwa vitendo ili wawe na uwezo wa kuja kujiajiri.
Wanafunz wafundishwe shughuli za ujuzi kwa siku za alhamisi na ijumaa nchi nzima. Na hii iwe ni kwa nadharia na vitendo. Kila mwanafunzi achague kusomea ufundi au ujuzi ambao atakuwa anaupenda. Ujuzi ambao utakuwa unafundishwa ni pamoja na ususi na unyoaji, utengenezaji wa masofa, au utengenezaji wa thamani, ujuzi wa umeme ngazi ya awali, ujuzi wa kutengeneza magari ngazi ya awali nk
Kila mwanafunzi atachagua ujuzi mmoja ambao atakuwa anaupenda na ndio atakaousomea kwa siku ya alhamic na ijumaa akiwa kidato cha pili na tatu na atafanyia mtihani wa somo hilo kwa vitendo mwishoni mwa kidato cha tatu kabla hajaingia kidato cha nne.
MACHAGUO MBALIMBALI BAADA YA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE.
Wale watakaofaulu kwa division one au two watachaguliwa kuingia kidato cha tano na sita kwa ajili ya kusomea michepuo mbalimbali ili waje watumike katika nyanja mbalimbali.
Waliofaulu kwa division three au four watachaguliwa kwenda veta kwa ajili ya kuongeza ujuzi zaidi kwa kuzingatia matokeo yao waliyoyafanyia mtihani hapo kidato cha tatu ambapo alikuwa amesomea ujuzi mmoja na kufanya mtihani wa veta. Hiyo kada ya ujuzi ambayo aliisomea kidati cha pili na tatu kwa siku za alhamic na ijumaa kama atakuwa alifanya vizuri ataendelea na ngazi ya pili katika ujuzi huo.
KIDATO CHA TANO NA SITA
Kwa kidato cha tano na sita wanafunzi watasoma wakiwa na umri wa miaka 16 au 17 adi 19.
Kwa hatua hii wanakuwa wanaandaliwa kuja kutumika katika nyanja au kada mbalimbali kama vile madaktari, wachumi, nk. Ivyo watasoma katika michepuo mbalimbali ambayo itawaandaa kuja kutumika katika kada au nyanja mbalimbali baada ya kufaulu na kusoma zaidi katika kozi mbalimbali hapo vyuo vikuu.
VYUO VIKUU
Vitahusisha wanafunzi wa kuanzia miaka 20 na kuendelea ambao wataandaliwa kuja kuwa kutumika katika kada mablimbali za kiutumishi.
HITIMISHO
Tanzania tuitakayo ya Elimu yetu, maisha yetu itahusisha mabadiliko chanya katika elimu kwa kuboresha na kuongeza utoaji wa ujuzi katika nyanja mbalimbali sambamba na maarifa ya kitaaluma. Ujuzi utahusishwa kuanzia shule ya msingi asa kilimo na tehama. Pia ujuzi katika ngazi ya sekondari utahusisha nadharia na vitendo na mitihan itatungwa na kutahiniwa na chuo cha veta. Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

Upvote
3