Edson Eagle
Member
- Apr 20, 2024
- 30
- 12
Niongelee mapendekezo machache leo.
1. Serikali iboreshe barabara kwa kiwango chenye uimara zaidi toka ngazi ya mkoa hadi kata. Na sio barabara ambazo wakati wa mvua hazipitiki.
2. Mifumo ya usambazaji maji ya bomba iboreshwe na iwe imara, tuachane na bomba ambazo zinapasuka kirahisi, kushika kutu nakuleta changamoto ya maji mitaani.
3. Serikali iongeze kasi na juhudi za usambazaji maji na uchimbaji visima vya kisasa katika maeneo ambayo bado tunauhitaji wa maji.
4. Kujenga madaraja yenye ubora mkubwa ili kuepusha vifo na kuharibika kwa barabara mbalimbali zinazokatisha mito.
5. Kujenga masoko ya kisasa na yenye mpangilio mzuri katika maeneo yasiyokuwa na masoko mazuri ili kuchochea maendeleo ya biashara mbalimbali ktk maeneo husika.
6. Utaratibu wa mpango mji katika maeneo ambayo ndo yanaanza kuendelea uwe unafanyika mapema kabla ya watu kuwa wengi ili kuepusha mararamiko ya watu kujikuta wamejenga kusiko stahili.
7. Kuangaria ubora wa nguzo na maeneo zinakowekwa kwaajiri ya umeme, ili kuepusha changamoto ya nguzo kudondoka na kuinama kitendo ambacho ni hatari zaidi.
8. Bajeti inaporuhusu serikali ijenge miundo mbinu ya kisasa zaidi mfano barabara za juu kwa juu(fly over), majengo ya biashara, maofisi, hoteli za kitalii n.k, lengo ni kuhakikisha Tanzania inakuwa katika sura nzuri yenye kuvutia kwa maendeleo zaidi hata katika mataifa mengine.

Upvote
1