SoC04 Tanzania tuitakayo inaletwa na kuimarisha ulinzi kwa watoto ambao ndio taifa la kesho

SoC04 Tanzania tuitakayo inaletwa na kuimarisha ulinzi kwa watoto ambao ndio taifa la kesho

Tanzania Tuitakayo competition threads

MAMOPRODUCT

New Member
Joined
May 5, 2024
Posts
2
Reaction score
2
UTANGULIZI
Watoto ndio taifa letu la kesho, kila sekta ambayo iko ndani ya nchi kwajili ya maendeleo ya nchi madhumuni yake ni kukua na kudumu kwa muda mrefu. Watu pekee ambao wanatakiwa kuendeleza taifa na misingi ya nchi ni watoto wa Tanzania ambao wanatakiwa kupokea na fundishwa kuenzi kile ambacho tumekipokea kutoka kwa waasisi wa taifa letu. Ukweli ni kwamba kama waasisi wa taifa letu wasinge simama na kuweka misingi bora kulinda watoto wa kipindi hicho tusingekua na viongozi imara wanaoweza kusimama na kuitetea nchi tulionayo leo. Moja ya vitu vinavyo thibitisha kuwa taifa la kesho halilindwi ni pamoja na maongezeko ya vitendo vya kikatili vinavyo ongezeka siku hadi siku. Vitendo hivi vya kikatili nikama vifuatavyo;

1 Kulawitiwa kwa watoto; kitendo hiki kinazidi kishika kasi siku hadi siku kwenye nchi yetu, jambo ambalo ni hatari kwa taifa kwasababu linauwa taifa la kesho. Jambo hili lisipo pingwa vikali baada ya miaka mitano hadi ishirini na tano idadi kubwa ya vijana watakua wamepitia kitendo hiki. Ambao vijana hao tunawategemea wawe wazalendo katika nchi. Ningumu sana kupata wazalendo katika nchi ambao nchi yao yenyewe imeshindwa kuwa na uzalendo kwao. Mbali na kuharibu saikorojia ya taifa la kesho watoto wanapitia hali ngumu ya kukosa amani katika nchi yao wenyewe wengine wanapata magonjwa yanayopelekea hata vifo.

Screenshot_20240604_224720_Chrome.jpg
Chazo: Mwananchi.co.tz
● Kubadili sheria hii tulio nayo na kuundwa kwa sheria kali, ni wazi kwamba sheria tulionayo haikidhi kushughulikia jambo hili na ndio maana pamoja na kuwepo kwa sheria bado hali inazidi kuwa mbaya kwa watoto wa nchi yetu. Itungwe sheria kari ambayo inatekelezeka kwa uharaka baada tu ya ushahidi kukamilika kwa wahusika wa jambo hili pia iwashughulikie raia wote wanao jihusisha na kuwalinda wahalifu wa kosa hili.

● Nchi kuwa na misimamo yake binafsi, kwamfano baadhi ya sheria zinapoundwa shirika la haki za binadamu linaingilia kati. Ubinadamu ni kuwatendea binadamu wengine ubinadamu, binadamu wanao watendea unyama binadamu wenzao wanawezaje kulindwa na binadamu? Nchi ifikirie juu ya hawa watoto ambao pia ni binadamu ambao hawana uwezo wa kujitetea wanao tagemea kwa kiasi kikubwa kulindwa na taifa la leo.

● Kuwepo na wapelelezi wa siri kwa kila idara ambayo inawahusisha watoto, mfano idara ya elimu ni idara pekee ambayo taifa limewekeza katika kutengeneza wataalam wake mbalimbalina viongozi wa badae lakini pia ndio idara ambayo inalea watoto wengi. Pamoja na hayo yote bado vitendo vya ulawiti wa watoto vinatokea mashureni mahali ambapo taifa linatakiwa liwajengee watoto ujasiri, linatumika kuwaondolea watoto kujiamini na kuwanyanyasa. Kwa kuwa na wapelelezi kutasaidia kupata ushahidi wa kutosha baada au kabla ya vitendo hivi.

Screenshot_20240604_230633_Chrome.jpg

Chanzo: Mwananchi.co.tz​

2. Kubakwa kwa watoto, ukatili huu umekua ukiendelea katika jamii yetu ya Tanzania, jambo ambalo limesababisha magonjwa ya virusi vya ukimwi kwa watoto, magonjwa mbalimbali ya zinaa, na wengine hadi kupelekea vifo kwa watoto. Baada ya miaka mitano hadi ishirini na tano nchi itakua na vijana ambao wamejaa uchungu ndani ya mioyo yao vijana ambao watakua wameshindwa kupiganiwa na taifa lao hawataweza kulipigania taifa lao, vijana ambao watakua na uchungu watafanya maamuzi ambayo sio ya amani katika nchi watafanya maamizi ya uchungu jambo ambalo litaua taifa.

Screenshot_20240604_231636_Chrome.jpg

Chanzo: bbc.com​
Mambo yafuatayo yanaitajika katika kushughulikia tatizo hili;

● Kuhimarisha sheria juu ya uhalifu huu pamoja na adhabu, katika kushughulikia jambo hili mara tu baada ya kukamilishwa kwa ushahidi hatua kali zichukuliwe ndani ya muda mfupi, pia makosa kama haya yasiwe na mdhamana kwa wahalifu.

● Elimu zitolewe kwa watoto na kwa jamii, maana jambo ili limekuwa likifanyika na watu wa karibu kabisa na watoto hawa mfano mtu ndani ya familia. Na muda mwingine familia imekua ikiwaficha au kuwalinda watu hawa. Kwahiyo selikari kwa kushirikiana na dawati la jinsia wahakikishe elimu inawafikia wahusika ili kuilinda Tanzania tuitakayo.
Screenshot_20240604_231452_Chrome.jpg

Chanzo: Mwananchi.co.tz​

3 Adhabu kali kwa watoto zinazo pelekea ulemavu wakati mwingine ata kifo, adhabu izo ni Kama kuchomwa moto, kuchanwa na viwembe na kuzibwa kwa sehemu sa Siri. Baadhi ya watoto wamepata madhala makubwa kwa kuzibwa kama vile kupasuka kwa vibofu vya mkojo kwasababu ya kuzibwa sehem za siri na walezi wao.

Screenshot_20240604_233520_Chrome.jpg

Chanzo: bbc.com​
Yafuatayo yanaitajika;
●Ianzishwe siku ya kuadhimisha siku ya watoto nchini, ambayo itaeleza zaidi umuhimu wa kuwalinda watoto.
● Kuwepo na chombo husika kitakacho saidia kuwafuchua wahalifu na kipewe mamlaka ya kuhakikisha adhabu kali zinatolewa kwa unyanyasaji wowote wa watoto na sio kuwalinda.
Screenshot_20240604_233023_Chrome.jpg

Chanzo: mobile.Tanzabiaweb.live​
● Selikali itenge fungu kwajili ya kuwasaidia watoto wenye mahitaji mbalimbali, kwasababu kuna kuna waharifu wanaotumia shida mbalimbali za watoto kuwanyanyasa. Hivyo kwakua tunataka taifa bora nilazima tuingie garama kulijenga na kulisimamia ili kufikia Tanzania tuitakayo

HITIMOSHO
Kama nchi yetu itashindwa kuwalinda watoto amabo ndio taifa la kesho hatuwezi kuifikia tanzania tuitakayo, kwasababu uwekezaji wote ambao nchi inaufanya unategemea kwa kiasi kikubwa taifa bora la kesho yaani viongozi bora na wataalamu bora kwajili ya kuendeleza yale ambayo nchi inawekeza. Lakini pia kama nchi yetu ni huru basi serikali ihakikishe kila mtu ndani ya nchi anakua huru. Uhuru tunao wafundisha watoto wetu kuwa Tanzania ni nchi huru tuuhakikishe kwao kwa kuhakikisha wanaishi kwa amani katika nchi yao wenyewe. Ile tanzania ambayo waasisi wetu waliipigania kwa kutunza maadili yalio walinda watoto hivyo hivyo taifa la leo linatakiwa liyafuate ili kuhakikisha kuwepo kwa tanzania ya kesho.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom