MURUSI
JF-Expert Member
- Jun 25, 2013
- 4,537
- 8,824
TANZANIA IJAYO ISAIDIA WATANZANIA KUPATA KAZI NJE YA NCHI ILI KUKUZA PATO LA TAIFA.
Diaspora ni moja ya wachangiaji wakubwa sana wa GDP ya nchi zingine hapa Duniani, Kenya wana kitengo ndani ya wizara ya mambo ya nje kinachowatafutia Wakenya kazi nje ya nchi ziwe za kuduma au za muda mfupi, hii hawafanyi kwa bahati mbaya ila ni kwa sababu wanajua umuhimu wake.
Wizara ya Mambo ya Nje inapaswa sasa kuja na kitengo maalumu kabisa kinachokuwa na jukumu moja tu kusaka kazi au Biashara Duniani huko kwa ajili ya Watanzania, Duniani kuna kazi na biashara shida kubwa iliopo ni connection au nani anawasaidia, Taifa kama Kenya wao wana wasaidia Wakenya wao ingawa pia kuna wakenya wanao pambana wenyewe.
Ili kupunguza tatizo la ajira ni lazima pia tuangalie nje ya nchi ni lazima Serikali iwe na mkakati wa kutafuta ajira huko Duniani ili Watanzania wasaidiea kwenye kukuza uchumi wa nchi. Idadi ya Watanzania walioko nje ni ndogo sana ukilinganisha hata na nchi ndogo kama Burundi.
Umuhimu wa Diaspora kwa uchumi wa nchi?
Mataifa mengi yanayoinukia yanathamini sana Diaspora na wanajua mchango wao kwenye uchumi wa Nchi zao. Nchi kama India ina Wizara ya Diaspora kabisa ambayo kazi yake kubwa ni kusaidia Wahindi walioko nje ya taifa la India. India ikiwa kama baba wa Diaspora Duniani yeye hupokea takriban Dola billion 70 kwa mwaka hii ni sawa na shilling za kitanzania trilon 161.
Tukiachana na India Kenya ni moja ya nchi inayonufaika vilivyo na wakenya wanaofanya kazi au biashara nje ya Taifa lao, Wakenya wanao ishi nje ya Taifa la Kenya kwa mwaka hutuma takriban Dola za kimarekani Bilion 4.19 kwa mwaka 2023 hii ni sawa na Shilingi za Kitanzania zaidi ya trilion 9. Hizi ni pesa nyingi sana na kumbuka zinaingia kupita Mabenki ya Kenya hivyo Serikali inapata kodi huko.
Kwa ukanda wa Afrika Mashariki, Kenya ndio inaongoza kwa kupokea pesa nyingi sana kutoka nje ya nchi ikifuatiwa na Uganda,Tanzania, Rwanda na Ehiopia, ila Kenya ameziacha mbali sana nchi zote za Africa mashariki.
Picha kutoka mtandao Kenya
Kwa Afrika Nigeria ndio inaongoza kupokea kiwango kikubwa sana cha pesa kutoka kwa wa Nigria wanao ishi nje ya nchi ambapo kwa mwaka wa 2022 tu Nigeria ilipokea Dola za kimarenakin Bilion 20.9 hizi ni sawa na fedha za Kitanzania Trlion ziadi ya 48.
Picha kutoka Bank ya Dunia
Ni Mbinu ipi Taifa kama Kenya hutumia?
Kenya wamekuwa wanaingia mikataba na Mataifa mbalimbali kwa ajili ya kuajiri Wakenya, Kenya imeingia mikataba na Ujerumani, Uingeleza na mataifa mengine ya Kiarabu pia. Wakati wa Kombe la Dunia kule Qatari Serikali ya Kenya ilipeleka walinzi zaidi ya 10,000 kusaidia ulinzi wakati wa kombe la Dunia, hizi zilikuwa ni kazi za muda kwa vijana wa Kenya walio hitimu mafunzo yanayo fanana na ya JKT.
Picha kwa mujibu wa NTV Kenya.
Na Serikali ya Kenya wana mpango wa kupeleka nje ya Taifa lao zaidi ya Wakenya 250,000 kila mwaka.
Picha kwa mujibu wa mtandao.
Nini tufanye Tanzania ili na sisi kukuza Diaspora ili isaidia katika kukuza pato la Ttaifa?
Serikali kupita Wizara ya Mambo ya Nje ni lazima sasa waje na mikakati imara na sera zinazofanya kazi za kuwasaidia Watanzania kupata kazi nje ya nchi, Kuna mataifa mengi sana yanayotafuta wafanyakazi, ila tatizo linakuja jinsi ya kuwapata, mataifa mengi yanataka uhakika kutoka Serikalini husika. Tumekuwa tunapigwa fimbo na Kenya hata kwenye ajira za walimu wa Kiswahili.
Ukienda Uganda au Rwanda Wakenya ndio walimu wa somo la Kiswahili wakati sisi ndio wazungumzaji wakuu wa kiswhili, hapa kuna tatizo kubwa sana kwa mamlaka kushindwa kuwashika mkono Watanzania.
Serikali ije na kitengo cha kutafuta kazi nje ya nchi tu na huzo kazi zitangazwe kwenye hicho kitengo na Watanaia waombe na wasaidiiwe pia, tunaweza fanikiwa endapo tutakuwa na vitengo vinavyo tafuta kazi nje ya nchi.
Serikali inapaswa kuanza kuongea na Serikali za mataifa mengine hasa yalioendelea sana ili waingie mikataba ya ajira, Mikataba ya ajira itasaidia Watanzania kupata kazi nje ya nchi kiulahisi kulivyo ilivyo sasa ambako ni wachache sana wanao pata tena kwa kupambana wenyewe na sio kushikwa mkono na Serikali ya Tanzania.
Passport iwe ni ya lazima kwa kila Mtanzania hasa walioko vyuo vikuu, Ilivyo sasa kupata passport ni sawa na kutafta kibali cha kulimiki Silaha, Serikali iachane na mawazo ya kijamaa kwamba ili upate passport lazima uwe una safari, hii imekosesha watu wengi furusa z kazi kwa sababu muda wa kufuatilia passport umekuwa ni mrefu sana na hivyo mtu kujikuta amekosa kazi. Pasport iwe ni ya lazima kwa Watazania kama ilivyo kitambukisho cha Taifa. Ili kusaidia Watanznia kupata kaz nje ni lazima pia hili swala la mashariti ya kupata passport liangaliwe upya.
Kuweka ufuatiliji, Afrika Kusini ilitangaza kipindi fulani kwamba inataka walimu wa Kiswahili, hii ilikuwa ni awamu ya Tano, wakati Hayati Raisi Magufuli amefanya ziara Afrika Kusini, baada ya hili taarifa kuoka Afrika Kusini hakuna ufuatiliaji ilifanyika au kuna ilisha anyika watu wakaajiliwa juu kwa juu au ndio pia Kenya wameisha tupiga bao? Tunapaswa kuanz akufuatilia vitu kama hivyo.
Picha kwa mujibu wa gazetu la habari leo.
Kuwatumia Watanzania walioko nje tiyari, Hii sijajua sababu ni nini hasa ila kuna ugumu Fulani kwa Watanzania walioko nje kuwatafutia Watznania wenzao kazi huko, hii ni tofauti na Wakenya ambao wanaitana sana huko nje au wa Ehiopia, Wasomali na pia Warundi. Watanzania waliko nje wasaide Watanzania wenzo kupata kazi au kufanya biashara.
Tunaweza punguza kwa kiasi kikubwa sana tatizo la ajira endapo tutaanza sasa kuwa na haya mawazo na kuyafanyia kazi ili kuwasiaida Watanzania kupata kazi nje ya Tanzania au hata kufanya biashara basi, zote kazi na Biashara zinamchango mkubwa sana kwenye pato la Taifa.
KARIBU KWA MAONI

Attachments
Upvote
2