Kihistoria Tanzania ni muunganiko wa nchi mbili uliofanyika mwaka 1964 ukijumuisha (Tanganyika chini ya mwalimu Julius Nyerere na Zanzibar chini ya Amir Abeid Karume ),kwa umoja wao waliweza kuunda serikali ya Jamhuri wa Muunguuno ambayo ndio nchi tuliyoko sasa isiyo na mipaka wala itikadi za namna yoyote ile.
Kutokea mwaka huo hadi kufikia sasa ni takribani miongo sita na nchi yetu ina mabadiliko anuai katika nyanja tofauti tofauti hususani siasa,elimu,afya,uchumi,na jamii kiujumla.
Napenda kuona Tanzania ijayo katika miongo miwili mbele iliyopiga hatua hatua zaidi katika suala zima la rasilimali, maliasili, na utalii kwani ni kichocheo kikubwa kinachofungua mianya ya fursa na kukua kwa sekta zingine maana hamna kitu chochote kitakachoanzishwa katika nchi hii pasipo kuangalia kama kuna uwezekano wa hiyo rasilimali uhusika mfano kama ni biashara rasilimali kuu itakuwa eneo,aina ya biashara na wateja (watu)hivyohivyo nchi yetu kama inahitaji kupiga hatua yoyote lazima rasilimali watu pamoja na vitu ambayo viko ndani ya nchi yetu kwa pamoja vifanye kazi sawia.
Kwa hiyo napenda kuiomba serikali iwe na macho peveku na fikra yakinifu juu ya hili na hii sekta(rasilimali, maliasili na utalii);Tuache nadharia ya kuhamsisha watu waje tu nchini mwetu kwani kwao wao hawamsishi sisi kwenda nchini mwao bali rasilimali tu zilizopo kwao na mazingira yao yanatosha kufanya sisi kuwa na shauku na hiana ya kwenda kwao bila ata ya nguvu ya namna yoyote ile; Si andiki la hasha kuikosoa serikali bali kujaribu kuona ni kwa namna gani serikali yetu itaweza kufunguka kwa upya na kuja na mpango madhubuti ya kuhakikisha nia yetu "kumulika maendeleo, uhuru, na amani",katika nchi yetu kama sehemu ya tunu tulizoimba pindi tuko mashuleni hata kipindi cha kukimbiza mwenge wa uhuru katika kuzindua miradi tofauti tofauti.
Kwa msisitizo mkubwa nakazia ya kwamba sekta hii ndio iliyobeba dhima kuu ya nchi,taswira ya nchi yetu jinsi ilivyo kwa hiyo haipaswi kubedhwa hata kidogo,chukua mfano mzuri wa nchi ya China ambayo kwa sasa inafanya vizuri kuanzia kitaifa, kimataifa na duniani kote utajua ya kuwa walithamini na kujali (rasilimali, hapa ileweke hawakuacha wananchi nyuma ndio maana wakadiriki hata kuweka sera ya ukomo wa idadi ya watoto katika familia, walipanga hivyo vyote kwa kuangalia uwezo walio nao na kamwe hakuweka akili ya kwamba pindi watakapo shindwa basi waombe msaada nje ,hapana mana tayari walijua uwezo wa nchi yao ulivyo.
Nipende kusema kama nchi hatujachelewa bado kikubwa tunahitaji ni utendaji wa kweli kati ya viongozi wetu na sisi wananchi. Na malizia kusema sekta hii itatupa muangaza mzuri wa sisi kama nchi "nini tunahitaji kwa sasa", vitu gani tufanye ili tuweze kwenda mbele zaidi, hii ndio sekta hata wageni wanokuja kutoka nchi nyingine watatujua kiundani kupitia hii sekta kuliko jinsi tunavyofikiri ,hivyo wajibu wa serikali hapa ni kuweka Sera wezeshi kwa ajili ya uwekezaji bila ubaguzi wowote yaani wazawa na wageni pamoja kuwa mstari wa mbele wa kuitaka jamii kuwa balozi namba moja na mstari wa mbele katika kupambania rasilimali zetu, pamoja na utalii hususani wa ndani na nje ya nchi ili kuleta mabadiliko chanya na tija nchini mwetu.
Wakao katika ujenzi wa taifa;
(Letitia)

Upvote
2