SoC04 Tanzania tuitakayo iwe ya mfano duniani

SoC04 Tanzania tuitakayo iwe ya mfano duniani

Tanzania Tuitakayo competition threads

Sking zone

Member
Joined
Jun 20, 2024
Posts
12
Reaction score
7
NATAKA TANZANIA IWE YA MAFANO DUNIANI (USHAIRI)
---------------------------------------------------

maono yalo moyoni, kichwani mwangu akili
asilimia Imani, naona hiyo fahali
Miji paka jijini, niona nzur Hali
naona nchi ijayo, mfano kwenye dunia

hii ndoto yangu pevu, kuona ikichipua
na tuli kwa utulivu, ndo ndpo tutafikia
mbeleni upo wokovu, endapo tutawania
naona nchi ijayo, mfano kwenye dunia

vinara nao wajenzi, ngazini nao wakwezi
utunzi wenye simanzi, baridi yake ni mwezi
Bando tuweke mabanzi, imara bati wekezi
naona nchi ijayo, mfano kwenye dunia

na sio pande za shilingi, maono kubashilia
maono haya misingi, kwa njozi kuifikia
siasa njema sipingi, katiba kuifungua
naona nchi ijayo mfano, kwenye dunia

elimu Bora kwa kina, vitendo ndio dhahabu
sayansi ikaze Sana, nchi tupate tabibu
Sanaa nayo kwa Sana, Sheria iwe irabu
naona nchi ijayo, mfano kwenye dunia

amani yenye utija, kuvuta watu kwa Nia
ni wapi panapo vija, nizibe bila Julia
wekeza nchi kwa tija, jifunze wako fikia
naona nchi ijayo, mfano kwenye dunia

panua zote fasihi, ondoa rushwa nchini
maono yangu naaihi, fisadi weka kwa chini
uchama sio sahihi, utija nchi mbeleni
naona nchi ijayo, mfano kwenye dunia

dondosha walo makupe, inua na wazalendo
hapo pongezi nikupe, Tanzania ya upendo
uchumi na unenepe, kusanya Kodi kwa pendo
naona nchi ijayo, mfano kwenye dunia

miundo mbinu imara, mijini na vijijini
uzalendo ndo kafara, kuweka nchi hewani
nasio wake vipara, shauri yetu Imani
naona nchi ijayo, mfano kwenye dunia

umeme kote nchini, hususa Ni vijijini
na maji kwetu thamani, uhai wa mishipani
ondoa Mila fitini, itatutoa relini
naona nchi ijayo, mfano kwenye dunia

maono yangu upendo, umoja mshikamano
furaha iunge pendo, mbeleni nchi Ni nono
usawa ukaze mwendo, tufike haya maono
naona nchi ijayo, mfano kwenye dunia
************************************"" "" "" "" ""
 
Upvote 2
Back
Top Bottom