Nabii Nathan
New Member
- Jun 27, 2024
- 2
- 13
1. Ukweli Mchungu
2. Madhara ya Ufisadi hasa ni Yapi?
3. Tufanye Nini Sasa?
4. Hatua za Muda Mfupi (Miaka 0-10)
Tuwe na viongozi wakali dhidi ya ufisadi, wazalendo na waadilifu kabisa kabisa, viongozi ambao wanauchukia ufisadi kama ukoma na wako tayari kuukemea kwa vitendo. Mwalimu Nyerere anafafanua hapa chini.
Chanzo: Katuni za Masoud
Chanzo: Katuni za Kingo
Chanzo: Africa Facts Zone (Facebook)
Chanzo: Transparent International
5. Hatua za Muda Mrefu (Miaka 10+)
Kubadilisha mtazamo na falsafa ya jamii kuhusu ufisadi
Chanzo: Google
Chanzo: Tovuti ya CCM 2010
Katika shindano la Stories of Change 2024, mawazo mengi ya kibunifu kuhusu Tanzania tuitakayo yatatolewa. Mengine yatakuwa ya kinadharia; na mengine yatakuwa ya kiutendaji (pragmatic). Yote haya yatakuwa ni bure kama tatizo la ufisadi halitatafutiwa ufumbuzi wa kudumu na endelevu. Ukweli mchungu ni kwamba Tanzania kamwe haitakaa ipate maendeleo ya maana kama hali ya ufisadi itaachwa kuendelea kama ilivyo sasa. Kwa maoni yangu, kupambana na ufisadi ndiyo unapaswa kuwa mkakati-mama kwa Tanzania tuitakayo.
2. Madhara ya Ufisadi hasa ni Yapi?
Kuna uhusiano wa moja kwa moja na wa kiusababishi kati ya kiwango cha ufisadi na maendeleo ya nchi. Ndiyo maana kwenye ripoti za shirika la Transparent International (TI), nchi zilizoendelea zina viwango vidogo vya ufisadi. Nchi za Afrika zina viwango vikubwa vya ufisadi; na umasikini. Kiufupi ni kwamba ufisadi na maendeleo haviambatani! Pesa za miradi ya maendeleo huibwa na kufichwa au kutapanywa hovyo, mafisadi na washirika wao huishi peponi wakati umma ukiwa hauna hata mahitaji ya msingi, haki hufifishwa maana wenye pesa huishi kama wako juu ya sheria, ukusanyaji wa kodi husuasua na nchi hujiendesha kwa kutegemea mikopo; huku kinachokusanywa na kukopwa kikiishia kuingia katika mzunguko ule ule wa kuibwa na mafisadi; na kufichwa ndani na nje ya nchi. Matokeo yake deni la taifa huongezeka, maisha huzidi kuwa magumu, miradi ya maendeleo hukwama, huduma mbovu za kijamii hutamalaki na nchi hudumaa kimaendeleo huku ufa kati ya matajiri wachache na umma likizidi kupanuka - hali ambayo hatimaye inaweza kuhatarisha amani ya nchi.
3. Tufanye Nini Sasa?
Ukweli ni kwamba hakuna uchawi au njia ya mkato ya kuweza kupambana ili kupunguza na hatimaye kuutokomeza ufisadi. Mapambano haya yanapaswa kuwa mkakati endelevu na wa muda mrefu ambao utahitaji mabadiliko ya msingi katika falsafa na mitazamo ya jamii kuhusu dhana za msingi kama uwajibikaji, dhima ya elimu, madaraka, heshima, ukumbufu (legacy), ubinadamu, utajiri na hata uzalendo. Huu ni wajibu wa jamii nzima.
4. Hatua za Muda Mfupi (Miaka 0-10)
Tuwe na viongozi wakali dhidi ya ufisadi, wazalendo na waadilifu kabisa kabisa, viongozi ambao wanauchukia ufisadi kama ukoma na wako tayari kuukemea kwa vitendo. Mwalimu Nyerere anafafanua hapa chini.
- Tuwaige Wachina. Walipoamua kujiondoa katika umasikini, waliamua pia kupambana na ufisadi kwa kutunga sheria kali na zisizo na simile. Ili kuwatisha mafisadi, inabidi sheria kali zitungwe na ni lazima zihusishe maumivu binafsi kwa wahusika. Sheria hizi kali zisiishie katika vifungo vikali tu bali mtu aliyethibitika mahakamani kufisadika ni lazima arudishe pesa zote alizoiba kama inavyofanyika huko Angola na Ushelisheli. Adhabu hizi kali dhidi ya mafisadi ikibidi zitajwe kabisa katika katiba. Katiba itamke wazi kuwa adhabu ya fisadi, bila kujali cheo chake, iwe ni kifungo cha kuanzia miaka 30 mpaka maisha (bila uwezekano wa msamaha) na kurudisha mali zote alizoiba.
Chanzo: South China Morning Post. 1/3/2024
Chanzo: Katuni za Masoud
Chanzo: Katuni za Kingo
Chanzo: Africa Facts Zone (Facebook)
- Tutumie teknolojia katika malipo yote ya huduma za serikali mf. ugavi na utoaji wa tenda, ajira, ulipaji wa nauli, vibali vya umiliki wa ardhi na viwanja, mikopo na misaada na hata upigaji wa kura vyote vifanyike kidijitali. Mifumo ya kidijitali iliyoboreshwa na yenye kiwango cha juu kisichoruhusu wizi kirahisi itasaidia kupunguza mianya ya ufisadi. TAKURURU inabidi iwekeze katika matumizi ya tekinolojia ili iweze kufanya uchunguzi kubaini mianya ya wizi katika mifumo ya kidijitali ya serikali pamoja na kubaini maficho ya pesa zote za mafisadi husika na kuzirudisha serikalini hata kama fedha hizo zimefichwa nchi za nje au kufunguliwa miradi haramu kwa kutumia majina ya watu wengine. Tuwe na mfumo usioingilika (encrypted) ambako wafichua maovu (whistle blowers) wanaweza kufichua taarifa za kifisadi bila kujulikana. Teknolojia za Blockchanis na Akili Mnemba zinaweza kusaidia pia.
- Tuimarishe maslahi ya wafanyakazi wetu serikalini na mafao yao baada ya kustaafu. Pia kusiwe na longolongo wala danadana katika kupatiwa mafao yao baada ya kustaafu.
- Tuwe na waandishi wanaoweza kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi kwa kufanya uandishi-chokonozi (investigative journalism) kwa kuibua kashfa za ufisadi.
- Tuunde mfuko maalum ambao utatumika kama kitia hamasa kwa viongozi wetu kuwa waadilifu. Kiongozi au mfanyakazi mwadilifu anayekataa rushwa apandishwe cheo na atambuliwe kwa kupewa nishani ya utumishi bora inayoambatana na zawadi ya pesa. Mfuko huu ambao utafadhiliwa na baadhi ya pesa zitakazokuwa zinatokana na kufilisiwa kwa mafisadi unaweza pia kutumika kama kimotishaji kwa wafichua maovu (whistle blowers).
- Tushirikiane na Mataifa Mengine. Mafisadi ni wajanja. Baadhi yao huficha pesa walizoiba katika mabenki na makampuni ya nje. Kwa hivyo ni lazima tushirikiane na nchi zingine pamoja na taasisi za kimataifa kama INTERPOL, Transparency Internatioanal na mashirika mengine yanayoweza kutusaidia kurudisha mabilioni ya pesa zetu yaliyofichwa huko nje. Tuige Angola na Ushelisheli.
5. Hatua za Muda Mrefu (Miaka 10+)
Kubadilisha mtazamo na falsafa ya jamii kuhusu ufisadi
Jamii yetu ina mkanganyiko. Kwa upande mmoja inaweza kuua masikini mwenzao aliyeiba maparachichi lakini ikaabudu fisadi lililokwapua mabilioni ya shilingi. Mkanganyiko huu ni ushahidi kwamba mapambano dhidi ya ufisadi ni lazima yaanzie katika kuielimisha jamii ili iwe na msimamo na falsafa moja katika mapambano yake. Huu unapaswa kuwa ndiyo mkakati-mama katika vita vyetu dhidi ufisadi. Hii itajumuisha kujenga upya moyo wa uzalendo. Hizi zitakuwa ni jitihada za pole pole na za makusudi zitakazochukua miongo na hata vizazi kadhaa. Masomo ya uraia na uzalendo mashuleni, umuhimu wa kufanya kazi halali, kujivunia uadilifu, mitaala ya kizalendo ni baadhi ya mbinu zinazoweza kusaidia.
Chanzo: Kundi sogozi WhatsappMapambano haya ni lazima yaende sambamba na uimarishaji wa taasisi zetu na kujenga mifumo imara na huru. Tunaweza kuanzia kwenye katiba yetu mpya. Madaraka ya rais yapunguzwe na asiwe mungu-mtu kama ilivyo sasa ambapo mfumo wetu unatufanya tunaabudu watu badala ya kuunda taasisi imara. Hakuna njia ya mkato ya kupunguza na kutokomeza ufisadi. Hizi zitakuwa ni jitihada za muda mrefu (pengine vizazi kadhaa), zenye kuleta maumivu; na zinahitaji dhamira ya kweli, juhudi za pamoja na za makusudi kutoka serikalini, taasisi za umma, sekta binafsi na jamii yote kwa ujumla.
Chanzo: Google
Chanzo: Tovuti ya CCM 2010
Upvote
7