Mfilipi WaTanzania
New Member
- Jun 20, 2024
- 3
- 6
UTANGULIZI: Rushwa imekuwa na maana nyingi kutokana na jamii tofauti ulimwenguni. Kwa Tanzania tunatafsiri Rushwa kuwa ni Kitu Chochote cha thamani ambacho mtu hutoa au kupewa ili kutoa upendeleo katika huduma au ni matumizi mabaya ya ofisi za umma kwa maslahi binafsi.
Kwa tafsiri hii binafsi ningependa kusema Rushwa ni Jina walilopewa wezi katika ofisi za umma. Ni wazi kuwa hawa wanaopokea au kuhitaji rushwa ili kuhudumia watu wanaiba haki na wanaharibu misingi ya maadili kwa kifupi wangeitwa wezi.
MADHARA YATOKANAYO NA RUSHWA .
Kutokana na kukithiri kwa vitendo vya rushwa nchini kumekuwa na madhara makubwa katika maeneo mengi kijamii, kiuchumi, kiutamaduni na kisiasa. Katika jamii zetu Kuna vifo vinatokea kutokana na uwepo wa rushwa, mafuriko yanatokea kutokana na ujenzi wa miundombinu mibovu, Viongozi wezi wa Kisiasa ambao binafsi ningewaita "Waharifu” kwani wanapatikana kwa hongo, mikataba mibovu katika manunuzi na kudumaza maendeleo ya Taifa.
Madhara yatokanayo na rushwa ni makubwa na inafikia wakati wale wanaoshiriki mapambano haya wanakuwa kwenye hatari kwa sababu rushwa imeonekana kama Chimbo kwa wenye kushiriki, wanavuna pesa na kulipa ada za watoto, kutembelea magari ya kifahari, kutumia rushwa kushinda nafasi za uongozi katika ngazi tofauti na kustarehe. Kwa hiyo ukionyesha uwazi katika kupambana na suala hili utakuwa kwenye hatari ya kifo.
NAMNA YA KUFANYA ILI KUFIKIA TANZANIA TUITAKAYO KWA MIAKA 5 HADI 25 KATIKA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA TANZANIA.
(a)Wananchi wanapaswa kuelimishwa juu ya masuala ya rushwa. Wengi hawajui maana ya rushwa, Madhara ya rushwa, Sheria za rushwa na umuhimu wa kushiriki katika Mapambano dhidi ya Rushwa.
(b)Wananchi wajengewe uwezo na utambuzi ili kuondoa fikra kuwa mapambano dhidi ya rushwa ni ya wote na siyo jukumu la Takukuru pekee.
(c) Sheria ya Kuzuia na Kupambqna na rushwa ipitiwe na kuweka adhabu zenye kutoa funzo ili isionekane kama ni suala jepesi na mazoea. Sheria hii imeainisha adhabu ambazo mara zote ni rahisi watenda makosa kuzimudu na kurudia makosa bila hofu. Ikiwezekana adhabu ya kufungwa jela au kunyongwa iwe ndiyo kipaumbele kuliko faini.
(d) Baadhi ya Makosa ya rushwa kwa mujibu wa Sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa yawekewe ugumu katika utetezi ili adhabu sitahiki zitoe funzo.
(e) Mchakato wa ushahidi uwe rafiki kwa wananchi kuliko kuwa mgumu ili kuweka wepesi wa wananchi kujitoa katika mapambano dhidi ya rushwa, pia kupokea tuhuma ya mtenda kosa ni rahisi lakini kuthibitisha na kuhukumiwa inakuwa ngumu. Sheria izingatie tamati ya Kesi.
(f) Suala la taarifa za hukumu za kesi ziwe wazi kwa Machapisho ya umma, hii itaamsha hali ya Wananchi kuamini kuwa, tatizo linashughulikiwa. Yaani Vyombo husika viwe vinaweza wazi ripoti za idadi za kesi wanazopokea kwa vipindi na kueleza ngapi zimehukumiwa na ngapi zimekwama, kuliko kuishi bila uwazi wa uendeshaji kwa takwimu. Hii itajenga Imani Kwa wananchi na kushirikiana na serikali kikamilifu.
(g) Vyombo vya Ulinzi na Usalama vinavyoshiriki katika mapambano dhidi ya Rushwa viwe huru katika kutimiza Majukumu Yao. Hii ni kwa sababu kuwa wakuu wa vyombo hivi hasa Takukuru, Mahakama na Polisi wanateuliwa na Rais. Kitendo kinachowanyima meno ya kung'ata pale inapotokea mhusika ni mwenye mamlaka ya kuteua au upande wake wa chama tawala, hii inaweza kujitokeza sana nyakati za uchaguzi.
(g) Kuweka Mkakati wa pamoja wa kushirikiana na Asasi za kiraia na Asasi zisizo za Kiserikali ili kuongeza nguvu kazi. Ni wazi kuwa Takukuru pekee haiwezi kufanikiwa katika mapambano dhidi ya rushwa hivyo ni vema wadau na washirika wa Takukuru hasa Asasi za kiraia zikashirikishwa kimkakati ili kufanikiwa katika mapambano haya.
HITIMISHO, Rushwa ni adui mkubwa wa taifa letu na hastahili kuchekewa Wala kuvumiliwa, Rushwa imeua watu wengi kuliko vita ya wenyewe kwa wenyewe, mafuriko au mapinduzi yoyote duniani kwani mapinduzi, mafuriko na vita ya wenyewe kwa wenyewe huwa vinatokea kwa kusababishwa mara nyingi na watu kuchoshwa na vitendo vya rushwa ambavyo huamsha hisia mbaya na kuchukua maamuzi magumu. Kwa hiyo rushwa ni adui mtangulizi wa maadui wote. Lazima tupambane na rushwa kufikia Tanzania Tuitakayo Kwa miaka 5 hadi 25.
View attachment MDAHALO-VII.png

Attachments
Upvote
10