SoC04 Tanzania tuitakayo katika nyanja mbalimbali

SoC04 Tanzania tuitakayo katika nyanja mbalimbali

Tanzania Tuitakayo competition threads

Samwel malisa

New Member
Joined
Jul 22, 2023
Posts
3
Reaction score
0
Kwanza kabisa nichukue nafasi hii kumpongeza Mh Raisi Mama Samia pamoja na viongozi wote wanaopambana usiku na mchana kwa kuhakikisha Taifa hili linajengeka vyema nakuwa imara kila leo, uku tukidumisha amani aliyo tujengea Baba wa taifa Hayati Mwl Nyerere, hivyo basi yatupasa ya sisi wananchi kusukumana bega kwa bega na Serikali yetu ili tuweze kuijenga Tanzania iliyo bora hasa linapokuja suala la kulipa kodi yatupasa kila mfanyabiashara anapouza atoe risiti na kila mnunuzi anayenunua adai risiti, hii inasaidia kuinua pato la taifa ikiwemo na kuboresha miundombinu ya maji, barabara, hospitali, shule ,nk kupitia kodi zetu bila kukwepa tutajenga Taifa nzuri na imara kila sehemu.

Pia watanzania yatupasa kuwa wawakilishi wakubwa hasa kwenye sualala kutunza miundombinu yetu na mazingira kwa ujumla hii ikiwemo na kutunza vyanzo vya maji, kuto kukata miti ovyo na hivyo basi tuwe mabalozi wazuri wa kupanda miti na kuipendezesha nchi yetu nzuri.

Ombi langu kwa serikali haswa kwa Waziri wa elimu ni kuhusu katika shule zetu za sekondari na msingi kungekuwa na vipindi vya stadi za kazi kwa vitendo mfano kuleta cherehani kwaajili ya kushona, mbao, matofali, mchanga, ikiwezekana na mashamba kwa ajili ya kilimo hii itasaidia wanafunzi angalau kuwa na ujuzi ambao ita kuwa na manufaa kwake badae na hata kwa Taifa kwa kipindi cha likizo au cha kutafuta ajira atakuwa kashapata mwanga wa kutamani kujiajiri katika kipindi hiki ambacho ajira zimekuwa ngumu kwa wasomi waliohitimu chuo.

Nichukue nafasi hii pia kuiomba serikali kupitia wizara yake ya afya wote tunajua ili kujenga nchi imara tunatakiwa tuwe na afya bora kwanza tuwapongeze kwa kazi nzur mnayofanya na mnayoendelea kufanya. Kiukwel bado vijijini tunapata changamoto kutokana na wataalamu wa afya haswa madactari au Dactari yupo vifaa haswa vya maabara havipo hivyo kufanya wananchi wa vijijini kwenda mjini kutafuta huduma hiyo.

Tunaiomba serikali kupitia sekta husika kuangalia kwa jicho la pili kuhusu hili maana ili tuwe na uchumi bora yatupasa tuwe na afya nzuri ya kufanya kazi hivyo basi yapaswa kuweka huduma nzuri mjini na vijijini. Pia kwenye kuijenga Tanzania bora badae inapaswa serikali kuchukua hatua ngumu haswa kwenye kubinafsisha baadha ya kampuni/mashirika yake na hii itasaidia kuleta ushindani baina ya wawekezaji mfano nchi zilizoendelea zimebinafsisha mashirika yanayojihusisha na umeme na ndio maana umeme kwao haukatiki kila mwekezaji anakuja na umeme wake mwingine maji, mwingine upepo, mwingine takataka kuozeshwa, na inakuwa nadra sana umeme kwao kukatika kwa nchi hizo kwakuwa awategemei chanzo kimoja cha uzalishaji.

Umeme ukija kwenye dunia ya sasa teknolojia inakuwa kwa kasi sana na hii inatokana na nishati ya umeme kwa asilimia kubwa. Hivyo basi serikari inapaswa kuliangalia suala hili kwa upana sana kutokana na hali ya umeme nchini kuwa ya mashaka sana ili uchumi ukuwe inatakiwa umeme wa uhakika ili viwanda vifanye kazi ipasavyo.

Kwenye hili swala la viwanda pia serikali inapaswa kujenga viwanda vingi maana ili uchumi ukuwe unahitaji kuzalisha zaidi kuliko kununua mfano mzuri ni nyumbani ukununua mahindi na ukilima kipi kinafaida, ukinunua mahindi kwa ajili ya nyumbani uwezi uza tena ila ukilima ukapata mahindi mengi unaweza uza tena, hivyo basi serikali ijenge viwanda kwa wingi ili tuzaaalishe vitu kwa ajili yetu na vingine tuuze nje ya nchi na kufanya nchi yetu itambulike zaidi kama nchi ya kibiashara mfano china.

Vikijengwa viwanda vitasaidia ata kwenye suala la madini maana kunachangamoto sana juu ya kuchakata madini na ndio maana kila kukicha yanasafirishwa nje ya nchi kwenda kuchakatwa na mwishowe huuzwa hukohuko na kukosesha Taifa mapato.

Tanzania ni nchi iliyo barikiwa ardhi nzuri yenye rutuba serikali kupitia wataalamu wake kwenye wizara ya kilimo ingefanys utafiti juu ya mazao ya kibiashara yenye soko ndani na nje ya nchi na kutoa elimu yake kwa wananchi haswa vijana ikiwezekana na kutoa mikopo yenye riba nafuu ili watu wengi watamani kujiunga na fursa hiyo na wakati wa kuvuna serikali ndio inunue na kuuza haswa nje ya nchi kupitia fursa hii serikali itakuwa imeinua pato lake na kipato kwa wananchi kwa kipindi hichi abacho ajira zimukuwa ngumu na kupelekea vijana wengi waliohitimu masomo yao kukosa kazi na mwishowe kuzurura mitaani bila kazi yoyote na mwishowe kudumbukia kwenye vitu viovu na visivyo kuwa na maadili mazuri na Taifa linategemea vijana sana kwenye ishu ya kujenga nchi bora baadae.

Ukiangalia nchi za wenzetu wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwekeza nguvu kubwa kwa vijana haswa pale wakiwa wadogo na kugundulika na vipaji maalumu kwa kugundua vitu au kutengeneza vitu, wanaamini ukiwekeza kwao unakuwa na hazina kubwa ya baadae hivyo basi kama tunahitaji mafanikio kuna muda hatuna budi kuiga kwenye nchi zilizoendelea na kujifunza kitu ikiwezekana ata kuwasomesha vijana wenye vipaji kuwapatia vifaa ili watengeneze kitu bora na hata kuwatafutia soko la bidhaa zao na hapa tutajenga taifa lenye uzalishaji bora kuliko kununua kutoka nje.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom