sba
New Member
- Jun 16, 2024
- 4
- 2
Ili kuweza kufikia maendeleo Mazuri kama taifa afya ni kitu ambacho kinapaswa kuangaliwa kwa upana zaidi yafuatayo ni mawazo yangu juu ya maendeleo ya taifa kwa miaka kumi katika sekta ya afya
1. Kuajiri wataalam wengi wa afya kwenye vituo vyote vya serikali kuanzia dispensary hadi hospital lengo kutoa mwanya kwa watumishi kuwa na zamu na kupata mda wa kupumzika
2. Kuhakikisha vifaa tiba na Madawa yanapatikana lengo likiwa ni kuwarahisishia kazi wataalam wa afya
3. Kuwezesha mazingira rafiki kwa watoa huduma ili wawe karibu na eneo la kazi
4. Kuziba mianya ya matumizi ya mitandao ya kijamii wawapo eneo la hospital lengo ni kuwezesha privacy za wagonjwa na watoa huduma
5. Kutengani siasa na sekta ya afya kwani watumishi wengi wa afya wanafanya kazi kwa pressure ili kuwafurahisha wanasiasa na si kwa kufuata miiko ya kazi na maadili ya kazi yenyewe
6. Kuhakikisha upatikanaji wa Bima ya afya kwa watu wote na kwa malipo stahimilivu kwani watu wengi wanapata shida kutokana na upatikanaji mbovu wa Bima ya afya na huduma itolewayo na Bima husika
7. Kutengeneza mpango mkakati wa kudhibiti magonjwa ya mlipuko kwani bado nchi yetu hatuna mkakati mzuri wa kudhibiti magonjwa pindi yalipukapo
8. Kuboresha huduma ya mama na mtoto ili kuzuia vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na labda uzembe wa watoa huduma au uelewa mdogo wa jamii yenyewe
9. Matumizi sahihi ya tehama katika utoaji wa huduma ya afya iwapo huduma ya matumizi sahihi ya Tehama katika huduma za afya utaboreshwa tunaweza fika mbali sana
10. Kuwashirikisha wadau mbalimbali katika kupanga mipango mikakati ihusiyo uboreshaji wa huduma ya afya na kuyafanyia kazi mapendekezo na ushauri watakao utoa na kwa wale wenye uwezo wa kuwekeza kwenye miundo mbinu basi waruhusiwe kwa masharti yaliyo wekwa na nchi kwa kushirikiana na wizard
Mwisho iwapo tutaboresha afya kama taifa maendeleo ya taifa yatakua sana ndani ya miaka kumi kwani watu watakua na afya bora na Kuwawezesha kushiriki kwenye uzalishaji mali kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu

Upvote
2