SoC04 Tanzania Tuitakayo katika sekta ya elimu

SoC04 Tanzania Tuitakayo katika sekta ya elimu

Tanzania Tuitakayo competition threads

Hisha

New Member
Joined
May 18, 2024
Posts
1
Reaction score
0
Elimu ni Kitu cha msingi sana ili kuipata Tanzania Tuitakayo, Kuna baadhi ya mambo yakiboleshwa katika Elimu kuanzia ngazi ya msingi hadi Elimu ya juu:-

1. Ufuatiliaji wa mitaala kwa shule za msingi na serikali: wadau wa Elimu pamoja na wazazi inabidi tuwe tunafatilia,mitaala kama wanayopewa wanafunzi mashuleni inafundishwa sawia. Je Elimu inayotolewa kwa wanafunzi wale wa shule za serikali inatolewa sawasawa.

2. Kubadilisha Elimu kuwa ujuzi: Wanafunzi wanatakia kupata Elimu ya ujuzi ,tusisubiri mpaka mwanafunzi amalize Kidato cha nne ndio ajue Kompyuta,Mapambo au ujuzi mwingine wowote, bali awe anapata huu ujuzi mapema iwezekanavyo kwa njia ya vitendo. Kwasababu ili kuipata Tanzania tuitakayo tusibaki pale binadamu wa kwanza alikuwa nyani, bali tunahitaji Elimu ya ufanisi na ujuzi wa Hali ya juu.

3. Elimu kuwa Fedha: Mazingira yanayo tuzunguka yanahitaji pesa na ndio maana wanafunzi wengi wanatoka nje ya msingi Ambao wamewekewa, hivyo basi tunajukumu la kuwafundisha wanafunzi wa Kidato cha kwanza na kuendelea, Jinsi gani wanaweza badilisha Elimu yao walipo hapo kuwa Fedha, kuwafundisha Elimu ya ujasiriamali, si ujasiriamali wa kuuza mandazi au genge pia ujariamali wa kuunda vitu ili wakati wake wa likizo awe anautumia vizuri.

Kwa kumaliza bila kuwa na Elimu yenye kutupatia mariifa vizuri ni sawa na kubeba mzigo kichwani usiokuwa na kitu, Tanzania tuitakayo inahitaji Elimu Bora na si Bora Elimu kwaajili ya Tanzania yetu.

Mungu Ibariki Tanzania.
Asante jamii forums kwa stories of change.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom