SoC04 Tanzania tuitakayo katika Sekta ya Madini

SoC04 Tanzania tuitakayo katika Sekta ya Madini

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
Apr 19, 2024
Posts
7
Reaction score
4
Utangulizi
Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizo na utajiri wa madini, tanzanite, dhahabu, rubi, fedha (silver), chuma, almasi, na nikeli. Hoja hii inagonga vichwa tuishie kuorodhesha utajiri tulionao au utumike kwa maslahi mapana, ili keki ya taifa iwafikie watanzania wote.

Screenshot_20240612-130331_1.jpg

Madini ya Tanzania chanzo habari leo​

Toka mwaka 1978 serikali imeboresha miundo mbinu ya sekta kwa kuhakikisha uanzishwaji wa shirika la madini la taifa STAMICO, mwaka 1981 chuo cha madini kilianzishwa MRI, chini ya mwamvuli wa wizara, tume ya madini na soko la dhahabu geita, na mikataba ya uchimbaji kwa kampuni za nje.

Makala hii itaangazia mikakati kufikia Tanzania tuitakayo kwenye sekta ya madini katika maono ya miaka 25 mbele.

Marekebisho ya Sheria na sera za madini kwa kuruhusu mijadala ya madini ya kitaifa na wadau. jamii ya wachimbaji, wanajiolojia, wanauchumi, wasomi, vijana, wanawake, kuchangia maono yao Katika maboresho ya sekta, na kuwapa wananchi fursa kuchangia maoni yao na kuondoa sintofahamu ya manufaa ya sekta hii.

Sheria za madini za kimataifa ziangaliwe upya ili kulinda hakimiliki ya nchi yanakochimbwa madini. kuepuka wizi wa madini.( Utoroshaji na uuzaji holela) Serikali ifanye jitihada uanzishwaji sheria za kimataifa za ulinzi wa madini ya kimkakati kama dhahabu na tanzanite itakayoleta manufaa kwa nchi

Serikali Kuwekeza Katika rasilimali watu, mitambo ya kisasa na fedha za uendeshaji migodi, hivyo kua mwendeshaji mkuu (doer) kwa kuimarisha uwajibikaji weledi na uzalendo. Ili kupata faida ya moja kwa moja kama taifa.

Uanzishwaji sheria ya kuwalinda waanzilishi wa migodi (wachimbaji wadogo). Kwa Kuwawezesha kupata leseni ya uchimbaji, Kutofukuzwa baada ya kupatikana mchimbaji mkubwa. Kuwawezesha mitambo na elimu ya madini na kupunguza utitiri wa Kodi.

Matumizi ya teknolojia ya satellite kamera, ndege zisizo na rubani (drones). Zitakazo nakiri picha za shughuli za mgodi, kubainisha hitirafu katika mitambo, kuimarisha ulinzi na usalama, kuzuia utoroshaji madini, na uharifu mwingine.

Screenshot_20240612-181307_2.jpg

Drones katika mgodi. Makala ya madini, Australia

Kufunga mifumo ya kiteknolojia ya usalama migodini kutumia vifaa vya mawasiliano ya kidijitali chini ya ardhi pamoja na vifaa vya kuweka mfumo wa uingizaji hewa itakayotoa sauti(alarm) pale inapohisi hitilafu.

Screenshot_20240612-193934_2.jpg

Kifaa cha mawasiliano ndani ya mgodi. Makala ya madini Australia​

Matumizi ya roboti kwa shughuli zenye viashiria vya hatari kwa binadamu. hasa uchimbaji, ulipuaji na ubebaji wa mizigo ndani ya mgodi ili kuleta usalama na ufanisi na kuongeza uzalishaji


Screenshot_20240608-172415_1.jpg

Picha ya roboti mgodini. makala ya madini Australia​

Elimu ya geolojia na miamba kwa wachimbaji wadogo na kujenga uelewa wa mazingira ya migodi ili kupunguza gharama za uendeshaji na kuondoa dhana ya uchimbaji kuhusishwa na imani za kishirikina.


Matumizi ya program za kikanuni za kihisabati (AI alogarith)Katika kutatua tatizo la mfumo mitambo,hitirafu za mgodi kwa kompyuta. Ili kuepuka kutokea kwa majanga vifo, kuporomoka kwa mgodi kufungwa mgodi hivyo teknolojia itaokoa muda, rasilimali watu na fedha

Screenshot_20240612-181812_1.jpg

Matumizi ya kanuni za kihisabati . Makala ya madini Australia​

Taasisi za fedha kutoa elimu ya usimamizi wa fedha kwa wachimbaji wadogo ili waweze Kuwekeza faida kwa kutambua mapato na matumizi ili kubadilisha maisha yao na kuondokana na umaskini

Kuboresha miundo mbinu na mazingira ya jamii zinaozunguka. Uanzishwaji wa miji midogo ya kisasa kwa Kutengeneza barabara zinazopitika vipindi vyote, uwepo wa vituo vya afya, upatikanaji wa maji safi na salama, umeme wa uhakika uwepo wa mtandao (network) ujenzi wa masoko madogo ya madini, uwepo wa taasisi za fedha na ujenzi wa shule za msingi na sekondari za bweni.

Uwepo wa mkataba wa Utunzaji wa mazingira (land reclamination) kwa makampuni ya uchimbaji. baada ya shughuli za madini kuisha matengenezo ya mazingira na kurudi katika hali yake ya mwanzo kwa kufunika mashimo, kupanda miti ya asili na kuzuia utiririkaji wa vimiminika hatarishi hasa maji machafu kwa jamii kwa kujenga bwawa na kuyatibu tena kwa matumizi mengine.

Screenshot_20240612-052543_1.jpg

Ardhi iliyoathiriwa na ardhi iliyotengenezwa,Chanzo: Tanzania digest.

kuwapatia nafasi za kazi wahitimu wa fani ya madini, uandisi mitambo ya kidijitali na mfumo laini kwenye migodi mikubwa ya serikali ili watumie utaalamu walioupata kuleta ufanisi wa kazi na kuongeza uzalishaji.

Ushirikishwaji wa wanawake wachimbaji katika matumizi ya teknolojia . kuwapatia elimu juu ya matumizi ya mitambo ya kisasa kwenye shughuli za uchimbaji, uchenjuaji, kupasua mawe ( makinikia) kuwaunganisha na taasisi za fedha na kupata mkopo wa kuendesha biashara, na usimamizi wa fedha.

Uanzishwaji wa viwanda vya kutengeneza bidhaa za madini kwa kuyapa thamani na kuimarisha soko mtandao ( digital market)
kwa kutumia teknolojia na kuongeza bidhaa za madini

Matokeo ya uwekezaji
  • Kupungua kwa wawekezaji wa nje katika sekta ya madini ambayo huja na wataalamu wao na vijana wa kitanzania kupata nafasi za chini.
  • Kuimarika kwa usalama na kuepuka majanga kama ajali, vifo kuporomoka kwa mgodi, na kufungwa kwa mgodi
  • Kukua kwa uchumi
  • Nafasi za ajira kwa vijana
  • Kuondokana na migogoro kati ya wachimbaji wazawa(wadogo) na wawekezaji kutoka nje.
  • Kulinda mazingira na kuepuka madhara ya uharibifu wa mazingira.
  • Ukuaji wa uchumi kwa mtu mmoja mmoja hasa wachimbaji wadogo.
  • Ubunifu wa mitambo, robot na matumizi ya akili bandia kutoka kwa wazawa.
  • Kuimarisha uwajibikaji na kupunguza urasimu.
Nahitimisha kwa kusema Tanzania tunayoitamani ni yenye kujenga uchumi wake wenyewe na ustawi wa watanzania hasa wachimbaji wadogo.
 

Attachments

  • Screenshot_20240612-130331.jpg
    Screenshot_20240612-130331.jpg
    394.2 KB · Views: 11
  • Screenshot_20240612-130002_1.jpg
    Screenshot_20240612-130002_1.jpg
    211.8 KB · Views: 13
Upvote 4
Back
Top Bottom