AMOS MADUHU
New Member
- May 19, 2024
- 1
- 2
Naitwa Amos maduhu magembe kutoka ubungo manicipal kata ya kibamba.
Uchumi ni swala la msingi na UTI wa mgongo Katika maendeleo ya taifa letu la Tanzania Katika maswala ya kiuchumi, tunahitaji kufanya Mambo yafuatayo Ili kuifikia Tanzania tuitakayo baada ya miaka 25.
1. Viongozi kuwa wazalendo na nchi yao.
-mara nyingi viongozi wamekuwa wakiingia madarakani Kwa lengo la kujipatia kipato na sio Kwa lengo la kuwatumikia wananchi, mfano baadhi ya viongozi kufanya mamzi yasiyokuwa ( kupokea rushwa, kuja na tozo zisizorafiki )na tija kwa jamii- husika, na wakati mwingine kutokutekeleza Yale yote yaliyoahidiwa kwenye majukwaa, endapo kama viongozi wakijitoa kwaajili ya Tanzania yetu basi tunauhakika wa kufika mbali
2. Kuboresha uwekezaji wa ndani.
-wananchi wa Tanzania wanatakiwa kuwa wawekezaji namba Moja na kuwa wasimamizi wa rasilimali zao
- kuwepo na masharti nafuuu kwaajili ya wawekezaji, ikiwa ni pamoja na kuwepo na Sheria Bora zitakazo walinda wawekezaji
3. Somo la uzalendo liwekwe kwenye mitaaala mashuleni, Ili kutengeneza viongozi watakaoiongoza nchi yetu kwa moyo
4. Kuwepo na vigezo vya kisheria kwaajili ya wagombea, mfano ELIMU ya juu, awe vizuri kiuchumi, utimamu wa akili, Hali na ukomavu wa dini, hiyo pia itasaidia.
5. Kuboresha maslahi ya wafanyakazi Ili waweze kufanya kazi Kwa moyo, mfano kada ya afya, kazi wanayofanya na mshahara ni tofauti Kabisa, hivo hufanya watu kufanya kazi Kwa viwango vya chini.
6. Upendo thabiti na kumuogopa MUNGU Katika swala Zima la kuilinda nchi yetu na rasilimali zetu kwa ujumla. Ikiwa ni pamoja na kufanya kazi Kwa bidii Ili kuongeza Pato la taifa letu, na masomo ya uchumi yasambazwe kwa vijana Ili waweze kufanya kazi na matumizi sahihi ya pesa walizonazo.
7. Kuepuka mikopo isiyo lazima katika nchi yetu, maana hili limekuwa chanzo Cha kusaini mikataba isiyo na maana, na itakayokuja kuua maendeleo na kupoteza rasilimali za taifa letu.
8. Kuamsha vijana katika swala Zima la maendeleo ya taifa letu, vijana wanatakiwa kutiwa hamasa na kuhusishwa katika kuchangia mawazo, kushiriki katika uendeshaji wa maswala ya kiuchumi ya taifa letu, hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuiendeleza nchi yetu
9. Kuboresha dawati la kijinsia Ili kuendelea kutoa fursa kwa wanawake katika swala Zima la maendeleo ya nchi yao, na pia kupinga ukatili wa kijinsia na kuimalisha mahusiano sawia kati ya wanawake na wanaume katika swala Zima la kuchangia maendeleo ya taifa letu.
10. Kuendelea kusimamia sekta zote katika taifa kulingana na njozi na maono ya kila sekta na kufanya tathmini Ili Kuona kama malengo ya kila sekta kama yamefikiwa na.
11. Uwajibikaji, kila mtu anatakiwa kuwajibika pasipokuwa na upendeleo, awe kiongozi au Raia wa kawaida, kila mmoja anatakiwa na kuwa na wajibu na kila tendo jema ya baya alilolifanya kwaaaji ya maendeleo ya nchi yetu, ikiwa Kuna kiongozi wa sekta furani kashindwa kufikia malengo ya sekta husika ni Bora kupumzika kuliko kuendelea kuwa mzigo.
12. Tuache unafki. Kila mtu asimame kwenye zamu yake kuhakikisha tunayafikia yote tukiyojipangia baada ya mda Fulani, ikiwa hatutofika lazima tuwe na maswali yatakayotupeleka kwenye hitimisho ya Nini kifanyike Ili kuridi kwenye mstari.
13. Maadili yasimamiwe katika taifa letu kwa kuanzia ngazi ya familia, tunapata viongozi wezi ni kwa Sababu kuanzia ngazi ya familia wazazi hawakuwa makini kwenye malezi ya watoto wao.
14. Kusimamia ubunifu na kuendeleza vipaji vya vijana wetu, tujitahidi kuendeleza kila wazo la ubunifu kwenye taifa letu kwaajili ya kutengeneza taifa letu
15. Kuwa na umoja, wenye usemi mmoja na muelekeo mmoja, muelekeo wa Tanzania unazingatia muelekeo wa viongozi na wananchi wenyewe.

Upvote
2