SoC04 Tanzania Tuitakayo katika soka haipo

SoC04 Tanzania Tuitakayo katika soka haipo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Seb Jr

New Member
Joined
May 3, 2024
Posts
2
Reaction score
0
Katika jambo linalowasumbua watanzania wengi kati ya mengi yaliyopo, soka letu linaendelea kututia Shaka kila kukicha, sis kama wadau WA mchezo huu pendwa na wenye chachu ya kuona mafanikio kwenye soka la taifa letu. Kwa wengi tunafatilia klabu zetu pendwa za Simba, Yanga, Azam na nyinginezo, wachezaji wengi, hasa wa Simba, Yanga na Azam ni wa mataifa mengine. Yamkini hii imefanya timu zetu zionekane, lakini maumivu yake yanaonekana kwenye uchaguzi wa wachezaji kwa ajili ya michuano mablimbali kama AFCON, CHAN na kufuzu kombe la dunia.

Hii hupelekea shirikisho la taifa kufikia kufanya maamuzi magumu, jambo ambalo linatuumiza mashabiki na wapenzi wa Taifa Stars. Lakini klabu hizi zina akademia na team B za kuchukua vijana wenye vipaji na morali ya kucheza mpira. Lakini mwisho wa siku, inaonekana vijana hawa hujipambania kuwa na maisha mazuri na sio kujiendeleza kwenye hicho alichokifanya. Na wengine huona kujiunga na akademia za vilabu vyetu vya nyumbani ni kujididimiza hivyo wanawasihi wazazi wao kuwapeleka kwingineko ili wapate nafasi ya kutumikia vilabu vya Ulaya kama Man City, Real Madrid, Barcelona au hata Liverpool na Juventus.

Hii hupelekea wao kubadilisha uraia na kutumikia mataifa hayo waliyojiunga ili wasirudi Tanzania kwa sababu hawaoni fahari kujitambulisha kama raia wa huku. Tukiangalia takwimu za Taifa letu kwenye soka katika michuano kama AFCON kwa mfano, tumekuwa kundi la kuchukua uzoefu kila mara, kila tukitoka kwenye michuano hiyo tunasema tunachukua uzoefu. Sasa hatuelewi tutachukua uzoefu mpaka lini. Haya kucheza kwao, hatuoni watu wenye morali na timu ya taifa Yao kwa ujumla. Kwa Hali hii, Taifa letu linaendelea kuwa nyuma katika mengi ya kimpira na tutaendelea kulalamika kila siku bila kuchukua hatua yoyote.

Na pia hata makocha wa timu ya taifa nao si wa kudumu, kwa maana timu yeti ya taifa imekuwa kama klabu ndogo, kwamba kocha anayeonekana anafaa, anaingia na kutoka. Kwa kipindi cha hivi karibuni tumeona jinsi timu ya taifa umekosa kocha mmoja wa kueleweka na kuleta manufaa kwa timu. Lakini tuangalie mfano wa Taifa kama Senegal ambayo imekuwa na Bwana Aliou Cisse tangu 2015 na amefanikiwa kuipa Taifa lake heshima kwenye hatua kama kombe la dunia na kuisaidia kununua taji la AFCON mwaka 2022. Nina Imani machache nitakayogusia hapa yataleta tija kwa vijana na wakuu kwenye nafasi za uongozi na hata wanafunzi wanaosomea ukocha ndani na nje ya nchi;

1. Kuwajengea morali wachezaji vijana na makocha chipukizi ya kuleta mafanikio kwa Taifa lao.

Kama nilivyotangulia kusema, kuna wanafunzi wanaosomea ukocha Tanzania na nje ya Tanzania. Na hata wao ukiachana na masomo Yao, Wana mawazo binafsi ya namna timu yake angependa icheze. Naamini hawa wakipewa nafasi kuonyesha walichonacho wanaweza kuleta mkubwa kwenye soka letu. Lakini morali sahihi inakosekana kwao na hii hupelekea wao kuishia kwenye ngazi ndogondogo. Kwa upande wa vijana chipukizi kwenye kucheza, hawa nao wanaamini katika uwezo wao WA kufanya mkubwa uwanjani, lakini katika akademia wanazohudhuria, vigezo vyao vinawakatisha morali ya kujiendeleza katika fani hii. Hivyo basi, naamini kuna wazoefu wapo katika tasnia hii na kupitia wao, ni maamuzi Yao kuangusha kizazi kijacho au kukipeleka mbali zaidi. Ninaamini kuwa makundi haya mawili yakipewa morali ya kujiendeleza zaidi kimpira, wanaweza kufanya mkubwa katika soka letu kiujumla.

2. Vilabu vyetu mablimbali viwape nafasi vijana chipukizi nafasi ya kuonyesha talanta zao uwanjani kwenye ngazi kubwa.

Vilabu vyetu mablimbali vinaangaza mafanikio ya sasa na baadae huanza kutapatapa kwenye mechi zijazo kutokana na wachezaji wao kuwa na makamo yasiyowaruhusu kutekeleza majukumu kisawasawa. Na klabu hizo zina akademia za kukuza vipaji vya vijana hawa. Lakini cha ajabu ni kwamba vijana hawa hatuwaoni wakifanya mambo katika vilabu hivi, hata kuwasikia ni shughuli. Na kinachotokea kwenye vilabu hivi na kwamba wanasajili wachezaji wa mataifa mengine, tukiamini wataleta matokeo chanya kwa haraka. Badala yake inakuwa tofauti na mategemeo. Hivyo ninaamini kuwa kila kitu ni hatua, na katika hatua hizi, mambo mengi hutokea. Hivyo klabu zetu zipende kuwekeza kwa ajili ya baadae, hasa kwa vijana hawa. Tunaona jinsi wenzetu wa Ulaya, Amerika ya Kusini na maneno mengine wanavyofanya. Klabu kama Liverpool, Man City, Arsenal, Chelsea, Barcelona, Real Madrid na nyingine nyingi zinafanya mambo makubwa hasa katika vijana. Mfano mazuri kabisa ni Real Madrid, walioanza kuwekeza tangu mwongo uliopita na consistency na heshima Yao uko palepale. Tunaona umahiri wa timu uko palepale lakini wachezaji si walewale, Bali wameibuka wengine wakubwa. Yamkini wanaweza kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza, basi wawapeleke kwa mkopo kwenye vilabu vingine ili wawe na ukakamavu WA kucheza kikosi cha kwanza na kupata uzoefu wa kukabiliana na shinikizo la kucheza kwenye ngazi kubwa.

3. Shirikisho lianze kuwaamini makocha wazawa kwenye timu ya taifa.

Kwa vipindi tofauti, timu yetu ya taifa imekuwa na makocha tofauti katika michuano mablimbali hasa AFCON. Kwa mfano, AFCON ya 2019, tulikuwa naye Emmanuel Amuneke, na AFCON ya 2023 iliyofanyika Ivory Coast, tulikuwa naye Adel Amrouche. Lakini nanukuu mfano wangu wa mwanzo wa Aliou Cisse ambaye alikuwepo tangu 2015. Na tukiangalia mafanikio yaliyokuwepo kwetu na kwao ni tofauti kabisa. Aliou Cisse ameleta kombe la AFCON kwenye Taifa lake na Sisi hatuna hata moja, hata kufuzu kutoka kwenye makundi ni kimbembe. Suala la uvumilivu kwetu limeonekana kuwa tatizo. Hivyo ninaamini tukiwapa nafasi wazawa, wanaweza kuleta mambo makubwa kwenye soka letu.

4. Makocha wa timu ya taifa wahudhurie baadhi ya mechi za ligi kuu na nyinginezo ili kuona jinsi wachezaji wao wanavyotekeleza majukumu yao.

Ningependa kutoa mfano wa kocha mmoja wa mataifa ya Ulaya. Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate, huwa anahudhuria baadhi ya mechi za ligi kuu Uingereza kuona jinsi wachezaji wa taifa lake wanavyocheza. Hii hupunguza bugudha kwenye kufanya maamuzi ya kuchagua wachezaji wa kushiriki michuano mablimbali, na pia huondoa malalamiko ya kwamba kocha hakupewa mamlaka ya kuchagua wachezaji aliowaona wanafaa kwake. Na katika kuchagua wachezaji hawa, shirikisho la mpira WA miguu lisiingilie kati, kwa sababu wamemuamini kumweka hapo katika nafasi hiyo, hivyo wampe uhuru WA kufanya maamuzi kama hayo.

Kiujumla, mambo mengine kama viwanja na rasilimali zingine zinaweza kutekeleza na washikadau wengine wenye moyo wa kuiona timu ya taifa inafika mbali, lakini msisitizo wangu upo kwenye suala la wachezaji na makocha, hata kama wachezaji wenye profile na uwezo kama mataifa ya Misri, Morocco, Senegal au Ivory Coast, ila tunaweza kufanya jambo lenye manufaa kwetu kwenye nyanja hii.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom