SoC04 Tanzania tuitakayo. "Kiswahili kipewe kipaumbele katika elimu"

SoC04 Tanzania tuitakayo. "Kiswahili kipewe kipaumbele katika elimu"

Tanzania Tuitakayo competition threads

winner2024

New Member
Joined
May 24, 2024
Posts
3
Reaction score
3
UTANGULIZI.

Kiswahili kimekuwa kikitumika sambamba na lugha ya kiingereza katika elimu itolewayo Tanzania.Utumizi huo umepangwa katika mfumo ambapo kiswahili hutumika kama lugha ya kufundishia katika shule ya msingi , na kiingereza kikitumika Kama SoMo mojawapo.

Katika ngazi ya sekondari, kiingereza hutumika kamma lugha ya kufundishia huku kiswahili kikiwa Somo mojawapo. Pia katika ngazi ya chuo, lugha ya Kiingereza hutumika Kufundishia isipokua kwa somo la kiswahili.

Kwanini lugha ya Kiingereza imepewa nafasi kubwa kuliko kiswahili?

Naam, Ni kwa sababu ya ushindani uliopo duniani hivi karibuni ambapo, lugha ya Kiingereza imechukua nafasi katika shughuli nyingi ikiwemo mikutano ya kimataifa, biashara za kimataifa , kusaini mikataba, udhamini wa Kimasomo, machapisho ya kusoma na kufundishia, sayansi na teknklojia n.k.

Kwa maana hiyo basi, matumizi ya Kiingereza yanaweza kutupa nafasi ya kujipima ubavu ili tuendane na mbio hizi za ushindani.

Kwanini kitumike kiswahili?

Moja, pata picha wewe mswahili/mtanzania unafundishwa kutengeneza keki kwa lugha ya kichina! Sio rahisi kuelewa kwa haraka kwa sababu Kwanza lugha Ni mpya lakini pia upishi wa keki kwako pia Ni mpya... Sasa turudi katika hoja, ufundishwe kupika keki kwa lugha kiswahili, Ni rahisi kuelewa na rahisi kukumbuka kwa sababu lugha unaifahamu.

Mbili, Kuna historia ilihopita hapo nyuma, juu ya chimbuko la lugha ya Kiingereza hapa kwetu Tanzania. Je, ukirudishwa chini ya wakoloni utakubali? Kama Ni hapana, kwanini unakumbatia vilivyo vya wakoloni? Ni wazi kua Lugha hii ilitumika sambamba na unyang'anyi, uonevu, maumivu, ukupe na ubeberu wa kutisha... Hivyo Basi, kuitumia lugha Ya Kiingereza Ni sawa na kujiweka akili zetu ndani ya ukoloni.

Tatu, Hakuna maendeleo yaliyowezekana katika Kiingereza ambayo hayatawezekana katika kiswahili.. mfano... Katika sayansi na teknklojia. Ni wazi kuwa, misamiati yote ipo katika lugha ya Kiingereza, na inawia vigumu kuipeleka katika kiswahili, katika ufundishaji wa maasomo Kama baiyolojia, kemia na fizikia, je Ni kweli wataalamu wa kiswahili tumeshindwa kukaa na kufasili sayansi hii ikatoshea kwa Wanafunzi wetu? Hakuna lugha iliyozaliwa na sayansi hivyo hata kiswahili chaweza kuibuka kidedea katika sayansi na teknklojia na wachina na wazungu wakatumia machapisho ya Kiswahili kufundishia uhandisi vyuoni kwao.

Nne, wataalamu wa Kiingereza hapa nchini wapo, lakini je, usahihi katika utaalamu wao Ni wa viwango vipi? Tayari tunao wataalamu wakufunzi wa lugha Hii ambao ukiwazingatia kwa Ukaribu nao pia wanahitaj ku"brashiwa" kidogo ili wawe angavu katika Kiingereza.. je, vipi kufundisha watoto kwa lugha Ambayo haijanyooka? Tujae kwenye Kiswahili mambo yawe murua.

Tano, tuwe wazalendo, turinge na vya Kwetu, nchi nyingi zilizoendelea hutumika lugha zao kufundishia na lugha zingine kama Somo tu.. sisi Ni Nani tuhangaike na Vya watu?! Hebu tukazie Kiswahili halafu tuone "tunapigaje". napata walakini wageni wakija kwetu sisi ndio tunapambana kuwasiliana nao kwa lugha zao,ifike mahala, wao, wajifunze Kiswahili ili wakifika hapa wapate namna, vinginevyo wajue wasipojua Kiswahili hawatafanikiwa katika mambo yao hapa nchini!

Hilo litafanikiwa Vipi? Kwa kujenga msingi mzuri katika kiswahili, kwa Kukazia kiswahili, kwa kustawisha Kiswahili...tukikipenda sisi hata wao watakiheshimu, Sasa kama tumekificha mgongoni, vipi wao wakiweke mbele?

Sita, Utambulisho wetu Ni upi? Tukisimama Kati ya Watu kumi wa mataifa mbalimballi Ni vipi tutatambulika kwa haraka bila kutumia Nguvu ya kujitambukisha? Jibu Ni rahisi, si kwa muonekano Wala sauti ,Ni kwa Lugha na sio lugha nyingine Bali lugha Ya kiswahil, kama jibu Ni rahisi hivyo, Kuna haja gani ya Kufundisha watoto kwa lugha Isiyowatambulisha popote? Tukazie maarifa. Kwa lugha ya KISWAHILI!

KWA UJUMLA; Hakuna Kisichowezekana kwenye nchi yenye Mali na utajiri wa asili Kama Tanzania,

1. Vitabu vichapishwe kwa Lugha ya Kiswahili!

2. Semina zitolewe kwa wakufunzi kwani kuchanganya lugha..yaani Kiingereza Na kiswahili (code mixing and code switching) sio sahihi katika ufundishaji.

3. Mfumo ubadilike hata katika nyanja nyingine za nchi ikiwemo ofisi za Kiserikali, mahakama za juu, mikutano n.k ambapo lugha ya Kiingereza ilikua ndio njia kuu ya Mawasiliano na badala yake kitumike kiswahili.
 
Upvote 3
Moja, pata picha wewe mswahili/mtanzania unafundishwa kutengeneza keki kwa lugha ya kichina! Sio rahisi kuelewa kwa haraka kwa sababu Kwanza lugha Ni mpya lakini pia upishi wa keki kwako pia Ni mpya... Sasa turudi katika hoja, ufundishwe kupika keki kwa lugha kiswahili, Ni rahisi kuelewa na rahisi kukumbuka kwa sababu lugha unaifahamu.
Je? Hata baada ya kumaliza elimu ya msingi darasa la kwanza hadi kidato cha nne bado tu kiingereza cha kupika keki kitushinde? Je uzwmbe utakuwa wa nani kwa mwanafunzi kumaliza kidato cha nne bila kuelewa kiingereza. Na kama hakufika form four uzembe ni wa nani? Sizungumzii kichina sababu hakipo kwenye masomo yetu, kiingereza kipo kwenye masomo ya msingi na hakidropiki!!
Sita, Utambulisho wetu Ni upi? Tukisimama Kati ya Watu kumi wa mataifa mbalimballi Ni vipi tutatambulika kwa haraka bila kutumia Nguvu ya kujitambukisha? Jibu Ni rahisi, si kwa muonekano Wala sauti ,Ni kwa Lugha na sio lugha nyingine Bali lugha Ya kiswahil
Hapo sawa Kiswahili tukipe umuhimu kwa ajili ya utambulisho, kisherehe zaidi kama vazi la Taifa. Lakini kutegemea lugha ndio itutoe kimataifa ni ngumu. Tunapotafuta maarifa mtandaoni mengi yapo Kiingereza. Kama ni kweli Kiswahili kitatutoa tuanze na utafiti mdogo wa mtu anapotaka kujifunza ujuzi wowote sasa hivi je yupi atapata madini fasta? Wa kiswahili au wa kiingereza?

Soko la lugha yetu halitaletwa na sheria, bali zaidi ni thamani tunayowapatia haoo watu wa ndani na nje
 
Je? Hata baada ya kumaliza elimu ya msingi darasa la kwanza hadi kidato cha nne bado tu kiingereza cha kupika keki kitushinde? Je uzwmbe utakuwa wa nani kwa mwanafunzi kumaliza kidato cha nne bila kuelewa kiingereza. Na kama hakufika form four uzembe ni wa nani? ...
Asante.. MAARIFA HAYAKUZALIWA KATIKA KIINGEREZA... hata sisi twaweza kujijengea MAARiFA kwa Kiswahili na mwisho na wengineo pia wakayapata MAARIFA kwa Kiswahili.. Nikisema kiswahili kiinuliwe namaanisha kianzie kwetu na kifike kimataifa.. mpaka huko mtandaoni
 
Je? Hata baada ya kumaliza elimu ya msingi darasa la kwanza hadi kidato cha nne bado tu kiingereza cha kupika keki kitushinde? Je uzwmbe utakuwa wa nani kwa mwanafunzi kumaliza kidato cha nne bila kuelewa kiingereza. Na kama hakufika form four uzembe ni wa nani?...
Nataka na Hiki Kiswahili kipande na kisidropike...
 
Asante.. MAARIFA HAYAKUZALIWA KATIKA KIINGEREZA... hata sisi twaweza kujijengea MAARiFA kwa Kiswahili na mwisho na wengineo pia wakayapata MAARIFA kwa Kiswahili.. Nikisema kiswahili kiinuliwe namaanisha kianzie kwetu na kifike kimataifa.. mpaka huko mtandaoni
Ni kweli kabisa. Tunakubqliana kipande kiumuhimu kiotomati kitasambaa tu
 
Back
Top Bottom