Kilimo ni shughuli ya kibinadamu inayohusika na uzalishaji wa mazao yanayotokana na wanyama pia mimiea.
Kutokana na ongezeko la idadi ya watu na mahitaji ya chakula cha binadamu na wanyama pia malighafi kwa ajili ya bidhaa za viwandani mtindo mpya na wa kisasa wa kilimo na kizazi kipya cha wakulima kinahitaji kuandaliwa na kuendelezwa.
Kunahitajika mabadiliko na maboresho ya mbinu, zana za kilimo na watendaji wa kilimo. Katika ulimwengu wa kisasa ambao una mahitaji ya hali ya juu ya ubora na idadi ya bidhaa za kilimo hakuna budi kuwa na wakulima ambao wana ujuzi wa hali ya juu katika nyanja mbalimbali ikiwemo kujua matumizi sahihi ya teknolojia na nishati, ufahamu wa masoko na uchumi wa kilimo, utoaji wa elimu ya kilimo na jinsi ya kuudumia wanyama na mimiea katika maeneo ya mashambani.
Picha kutoka: UN women.com
Ili kuwa na wakulima wa kisasa yafuatayo ni ya kuzingatiwa katika Taifa letu na jamii ya kitanzania;
ELIMU YA KILIMO
Elimu ya kilimo itahusisha kujifunza na kutumia ujuzi wa kilimo ili kuandaa kundi la watendaji wa kilimo wenye ujuzi na uelewa mpana wa sekta hii ya kilimo hasa upande wa uzalishaji. Elimu itakayotolewa italenga kumuwezesha mkulima kufanya uzalishaji kwa kuzingatia hali za kijamii, mazingira na jiografia na rasilimali zilizopo eneo la uzalishaji
Kuongeza uelewa wa jamiii za Kitanzania;
Katika taifa la Tanzania tumebarikiwa kuwa na jamii za wafugaji, wakulima wa mazao na wakulima mchanganyiko, wakulima wa kisasa wanatakiwa kuwa na uelewa wa shughuli za kilimo zifanywazo na jamii husika au jamii zao ilikuwa na uwezo wa kutumia mbinu na ujuzi ambao utaleta uzalishaji mkubwa zaidi na ulio na ubora mkubwa, ilikuwezesha jamii za wafugaji mbinu ya kufuga wanyama wachache wanaovumilia magonjwa na wanaotoa nyama na maziwa mengi zaidi ambao wataleta faida na kutumia nguvu kidogo kulinganisha na njia za kizamani kuweka wanyama wengi wenye faida kidogo pia kuchanganya kilimo cha mimea na mifugi ilikupata chakula cha kutosha cha mifugo na mbolea kwa ajili ya mimea.
Kufahamu mazingira na jiografia za uzalishaji;
Jiografia ya Tanzania na mazingira ya asili ya Tanzania yanauwezo wa kuhudumia shughuli tofauti za kilimo tumuandae mkulima mwenye ufahamu wa kutambua mazingira yake na kuweza kuwekeza kwenye mazao na wanyama ambao watampa matokeo na mazao bora hii inasaidia kutumia nguvu na gharama kidogo za uzalishaji wa bidhaa za kilimo kwa sababu mazingira wezeshi yenye hali ya hewa na tabia ya nchi inayoendana na wanyama na mazao.
Ufahamu kuhusu rasilimali wezeshi zilizopo eneo la uzalishaji wa kilimo;
Rasilimali kama mito, mabonde, misitu na udongo wenye rutuba ndio msingi wa uzalishaji wa mazao ya kilimo. Kutokana na uelewa wa nyanja mbalimbali ikiwemo utunzaji wa mazingira wakulima wa kisasa wa Tanzania watajenga uwezo wa kuwa maendeleo endelevu na kukuza uwezo wa kulinda rasilimali kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Elimu ni msingi wa maandalizi ya maendeleo haya ya kilimo yatakayoletwa na wakulima wa kizazi kipya. Kulingana na aina ya elimu mbayo watendaji hawa wa kilimo watapata, tutakuwa na watendaji ambao ni wakulima wanaohusika moja kwa moja na kazi za shambani, wahandisi wa kilimo watakao unda na kusimamia miundombinu na mitambo ya kilimo, wataalamu wa kilimo-biashara kwa ajili ya usimamizi wa masoko, biashara na uwekezaji, madaktari wa wanyama na mabibi na mabwana shamba.
Picha kutoka: jagranjosh.com
KUENDANA NA TEKNOLOJIA YA KISASA.
Teknolojia inawezesha matumizi ya mbinu na uelewa wa sayansi ya kilimo ili kuleta ufanisi katika shughuli za uzalishaji, usafirishaji, utunzaji, uandaaji pia masoko na mauzo ya mazao na bidhaa za kilimo.
Picha kutoka: senzagro.com
Ufahamu wa teknolojia za kisasa kama tehama, uzalishaji wa mbegu mpya za wanyama na mazao, matumizi ya mitambo ya ki-automatiki utawaweka wakulima wa kisasa wa kitanzania katika kiwango kikubwa cha kiushindani katika soko la ndani na la kimataifa.
UEWEPO WA MAMLAKA, TAASISI NA MASHIRIKA YA KILIMO ILIKUSIMAMIA SHUGHULI ZA KILIMO.
Ili kufikia maendeleo ya kilimo cha kisasa kunahitajika mfumo wa uongozi na usimamizi ambao utahakikisha kanuni na taratibu zilizowekwa kitaifa katika sekta ya kilimo zinafuatwa ili kuhakikisha utendaji wenye weledi kwa mfano kuwa na sheria ya utunzaji wa mazingira ya ili kulinda bayo-anuai pia kuzuia matumizi ya kemikali hatarishi ili kulinda afya za walaji, pia kuepusha matumizi mabaya ya fedha za umma na kuzuia rushwa
Ni matumaini yangu makubwa kwamba kizazi kipya cha wakulima kitakuwa na uwezo mkubwa wa uzalishaji na ubora wa hali ya juu wa mazao ya kilimo ili kuongeza thamani na ushindani katika soko la ndani na kimataifa la bidhaa za kilimo hivyo kuongeza pato la taifa na pato la wakulima, pia itasaidia kuleta maendeleo ya kiteknolojia na uzalishaji wa kiviwanda na kuendeleza miundombinu ya usafirishaji, nishati na mawasiliano.
#Tanzania tuitakayo

Upvote
2