Edgar71
New Member
- Nov 9, 2022
- 2
- 0
Nchi ya Tanzania inaendelea kufanya juhudi kubwa tangu kupata kwake uhuru, inaendelea kupanua wigo na maendeleo makubwa katika sekta mbalimbali za kijamii na ina matarajio ya kuendelea kufanya vizuri zaidi katika miaka ijayo hadi kufikia mwaka 2030.hivo bhasi hapa nitaelezea baadhi ya maeneo ambayo Tanzania inatarajia kuona mabadiliko makubwa katika kipindi kijacho cha miaka 5 hadi 25 ijayo.
1. Sekta ya Elimu, Serikali ya Tanzania imekuwa ikifanya juhudi kubwa katika kuboresha sekta ya elimu chini kupitia wizara ya elimu iliyopo nchini kwa Kupitia sera za elimu bure kwa wanafunzi kuanzia shule za msingi na sekondari au upili, na uwekezaji katika miundombinu ya shule mbalimbali zilizopo nchini katika Maeneo ya mjini na vijijin, mabadiliko ya mtaala wa elimu yetu kutoka mfumo wa zamani kwenda njia ya vitendo na njia ya kupima uelewa wa wanafunzi yaani competence based curriculum, pia Tanzania inatarajia kuona ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaopata elimu bora na ya kiwango cha juu kwa miaka ijayo.
2. Sekta ya AFYA, katika Sekta ya afya nchini Tanzania inaendelea kuboreshwa kupitia wizara yake muhimu ya afya, jinsia, Wazee na watoto kwa kuboresha na KUJENGA miundombinu ya hospitali mbalimbali nchini na vituo vya afya, kuongeza idadi ya wataalamu wa afya, na kuboresha huduma za afya kwa wananchi wote na pia Tanzania inatarajia kupunguza vifo vya watoto na akina mama na kuongeza matarajio ya kuishi kwa wananchi wote kwa miaka ijayo pia hata sasa.
3. Sekta ya Kilimo, pia sekta ya Kilimo ni sekta muhimu sana nchini Tanzania na serikali inaendelea kutoa msaada kwa wakulima mfano kugawa mbolea za ruzuku kwa wakulima wote nchini Lengo la serikali ni kuongeza uzalishaji na kuboresha masoko ya mazao hapa nchini kwa miaka hii na ijayo pia. Hivo bhasi Tanzania inatarajia kuwa nchi yenye kilimo cha kisasa na cha kibiashara katika soko la dunia na afrika mashariki kwa ujumla katika kipindi cha miaka ijayo.
4. Sekta ya mawasiliano na Miundombinu, nchi yetu ya Tanzania inaendelea kuwekeza katika miundombinu ya barabara kwa kushirikiana na wizara ya Miundombinu kwa kujenga barabara za lami na za kisasa zaidi ambazo zitarahisisha mawasiliano kwa wananchi, ujenzi wa reli za kisasa mfano standard gauge (SGR) ambayo pia zitarahisisha usafirishaji, kujengewa na kuboresha bandari zetu, na nishati ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya wananchi wa Tanzania. Hivo Tanzania inatarajia kuwa nchi yenye miundombinu bora na ya kisasa katika kipindi cha miaka ijayo yaani kufikia 2050.
5. sekta ya madini na utalii, serikali ya Tanzania inaendelea kuboresha sekta hizi kwa kuweka usimamizi ulio mzuri ili kuzuia wizi unaofanyika katika hizi sekta ambao napeleka kudorola kwa pato la taifa kutoka sekta hizi hivo kufikia 2050 matarajio ni kuona sekta hizi zinakua kwa kasi na kuongeza ajira kwa vijana wa Tanzania.
6. Pia sekta ya habari na mawasiliano, serikali inaendelea kuboresha mitandao kwa manaufaa ya wananchi kwa kukatibisha watu na mashirika BINAFSI kufanya uwekezaji katika sekta hii Hivo pia katika idara ya habari tunaendelea kuboresha kwa kuweka vifaa vya kisasa zaidi hivo Kwa ujumla, Tanzania ina matarajio makubwa ya kuendelea kufanya maendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii katika miaka ijayo hadi kufikia 2050, Kwa kupitia ushirikiano wa serikali, sekta binafsi, na wananchi wote wa Tanzania, Tanzania inaweza kufikia malengo yake na kuwa nchi yenye maendeleo endelevu na ya kipekee kupitia sekta zake zote zilizopo nchini.

Upvote
0