TANZANIA TUITAKAYO KUTANGAZA UTALII KWA NJIA YA KADI.
Huu ni ubunifu wangu kwenda sekta ya utalii Tanzania kwa kutumia kadi ya mwaliko, Je kadi mwaliko ni nini? Ni kadi maalum itayotolewa au kutumwa kwa familia za watu maarufu duniani kama wanamichezo, wasanii na wana habari wa nje ya Afrika kwa lengo la kuwaalika kuja kutalii Tanzania, kadi hii itasainiwa na Rais au waziri mwenye dhamana ya utalii na itaambatana na mambo matatu yafutayo itambatana na Sababu za mwaliko, Maeneo anayoombwa kuja kutembelea, na Tukio litakalo ambatana na ujio wake nchini.
NINI MALENGO YA KADI?
KUWAPA SABABU WATU MAARUFU KUJA KUTEMBELEA TANZANIA
KWAMBA; kwa kuwapa kadi ya mwaliko watu maarufu kuja kutembelea Tanzania itakuwa ni sababu nyingine ya watu hawa kuiweka Tanzania katika kipaumbele chao wakati wa likizo zao, mapumziko yao na matembezi yao.
KUWAHAMASISHA WATALII KUIPA TANZANIA KIPAUMBELE KATIKA MALENGO YAO YA KUTALII
KWAMBA; Kumekuwa hakuna hamasa Kwa watalii kuja kwetu ingawa na wengine hupita kwetu tu baada ya kutoka nchi jirani.
MFANO: Sarah Anderson raia wa Marekani anafikiria likizo yake kuja Afrika kutalii lakini mpaka sasa hajajua ni nchi gani anaanza nayo Afrika katika nchi 54 za Afrika, ataichagua nchi ya Ethopia na sababu labda wakati huo kulikuwa na tukio maaarufu limetokea Ethiopia, au rafiki zake wamewahi kumueleza kuhusu Ethiopia au anamarafiki wapo Ethiopia au anashirika la nchi yake linafanya kazi Ethiopia kwa maana hiyo Serikali ya Ethiopia haikushiriki kumshawishi Sarah Anderson kwenda Ethopia.
LAKINI JE: kama Sarah Anderson atapewa kadi ya mwaliko na Tanzania angetumia muda mwingi kupata habari za Tanzania kwenye tovuti au ubalozi wa Tanzania, angewauliza marafiki zake kuhusu Tanzania na angetaka kujua zaidi kuhusu ubalozi wa nchi yake uliopo Tanzania.“ kuna watalii wengi kama Sarah Anderson ambao wanahitaji huduma hii.
KUIFANYA SERIKALI KUTAMBUA NA KUHESHIMU MAFANIKIO YA WATU WENGINE DUNIANI
KWAMBA; kila mtu anapenda kutambuliwa kwa mafanikio yake na kazi yake hapa Duniani lakini Je nani anakutambua? Kupitia KADI hii Rais wa jamuhuri ya Tanzania atawatambua watu hawa kisha kuwaalika kuja Tanzania na ujio wao utakuwa na matukio maalumu kwa ajili yao, kwa namna hii watu watataka kuja kuitembelea Tanzania, kuisifia Tanzania kuwa nchi ya amani na ukarimu.
MFANO: LION MESSI mchezaji maarufu toka klabu yaInter Miami anatumiwa Kadi na Tanzania, kadi ambayo imesainiwa na Rais wa Tanzania, kadi ambayo inaambatana na sababu za kualikwa kwake na Rais wa Tanzania, jiulize nini LION MESSI anafanya baada ya kupata kadi hii?
JE, NINI KITATOKEA? wachezaji wenzake, familia yake na rafiki zake watataka kuijua zaidi Tanzania kupitia tovuti na mitandao ya kijamii je bila kadi hii nani angetaka kuijua Tanzania? nani angetaka kupoteza muda wake kutafuta habari za Tanzania? Je hii siyo njia sahihi kwa dunia ya leo kuwafanya watu siyo tu kuja Tanzania bali pia kutambua kuwa kuna Tanzania.
Pia sisi tunaamini ni gharama kubwa kumfanya LIONEL MESSI kuzungumzia Tanzania kwa wanaomzunguka, lakini kwa Kadi hii lazima atawashirikisha wachezaji wenzake, wanafamilia na ndugu wa karibu kuhusu mwaliko, ambao wanaweza kuja kuwa watarii wa Tanzania hapo baadae hata kama LIONEL MESSI hatakuja kwa Muda wa mwaliko
JIULIZE? Kuna watu wangapi maarufu hawajui kuhusu Tanzania na wamekosa sababu za kuijua Tanzania?
KUIPA HESHIMA SEKTA YA UTALII NA SERIKALI KWAMBA; Kadi hii imekusudia sana kuipa heshima sekta ya utalii na Serikali yake, kufanikiwa kwa kadi hii kutaipa heshima kubwa Tanzania sababu watu wengine wenye heshima duniani, maarufu watakuja Tanzania au watauliza zaidi kuhusu Tanzania hata kama hawata kuja, kutaifanya Tanzania kuwa nchi yenye ubunifu katika utalii na kuigwa na nchi zingine.
FAIDA YA KADI HII KWENYE UTALII
Itaongeza idadi ya watalii Nchini.
KWAMBA; idadi ya watalii itakuwa kubwa hasa watalii maarufu ambao huambatana na watu wao hali hii pia itawagusa watalii wengine kufikiria kuja Tanzania.
ITAONGEZA IDADI YA WATU WANAOTAKA KUJUA KUHUSU TANZANIA
Watu maarufu baada ya kupewa kadi watakuwa na hali na mwamko wa kuitaja na kujua zaidi kuhusu Tanzania.
ITASAIDIA BALOZI ZA TANZANIA KATIKA NCHI HUSIKA KUWA KARIBU NA WATALII AU WATU WANAOTAKA KUJA TANZANIA
Kadi hii itakuwa inatolewa na balozi wa Tanzania katika nchi husika au wakala wa balozi wa Tanzania kwa niaba ya Raisi wa Tanzania hivyo kuwafanya watalii waliolengwa kuwa karibu na Balozi za Tanzania.
ITASAIDIA SANA KUONGEZA SHUGHULI ZA KIUCHUMI NCHINI, UWEKEZAJI NA USAIDIZI WA JAMII FULANI TOKA KWA WATU MAARUFU DUNIANI.
Watu maarufu watakuja kutalii baada ya mwaliko lakini pia wakija watasaidia jamii zenye uhitaji kupitia taasisi zao, wanaweza kushawishika kuwekeza kwenye miradi mingine ya kiuchumi kama mahoteli, madini, gesi na kilimo.
MUONEKANO NA MAUDHUI YA KADI HII
KADI HII ITAKUWA NA MUONEKANO WA KIUTALII AU THAMANI SAWA NA MLENGWA.
Kwamba sababu itaambatana na sababu za kutolewa kwa mwaliko.
Kadi hii itaambatana na tukio la kitalii kwa mwalikwa au yeye kumpa nafasi kufanya tukio la kitalii akiwa Tanzania.
lazima kadi hii iwe na jina la Rais na saini yake kama sehemu ya mwaliko wa raisi kwa niaba ya watanzania pia kuipa heshima kadi yenyewe.
Kadi hii itakuwa na mawasiliano ya bodi ya utalii,wizara ya utalii, balozi wa tanzania katika nchi husika, anuani ya balozi ya nchi anayotoka.
Kadi hii itakuwa na jina la mlengwa au taasisi au shirika au majina ya walengwa.
WAPI NI WADAU KATIKA MPANGO HUU?
Wizara ya Utalii na Maliasili.
Balozi za Tanzania au Wakala Katika Nchi Husika.
Ubalozi wa Nchi Ya Mlengwa(Mtu Maarufu) au Walengwa Waliopo Nchini.
Taasisi za Watu Maarufu.
Bodi ya Maliasili na Utalii.
Ofisi ya Raisi Uwekezaji na Uwezeshaji.
Timu ya Ubunifu ya Mradi Huu.
WALENGWA KATIKA MRADI HUU WA KADI
Watu Maarufu Kama:-
WANAMICHEZO
*WACHEZA FILAMU
*WANAMZIKI
*WANASANAA
*WANAMITINDO
*Watu Maarufu Katika Maendeleo Uchumi na Siasa
Taasisi za Kijamii za Kimataifa
*Kampuni za Kimataifa za Matukio, Picha na Filamu.
*Taasisi za Elimu Na Utafiti
Hitimisho langu, natumai kuwa mawazo haya yataongeza ubunivu katika sekta ya utalii na pia gharama za kuyatekeleza ni dogo sana.

Upvote
1