SoC04 Tanzania tuitakayo kwenye sekta ya elimu miaka ijayo

SoC04 Tanzania tuitakayo kwenye sekta ya elimu miaka ijayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Hopper lyfer

New Member
Joined
Aug 31, 2022
Posts
4
Reaction score
4
Elimu ni Moja ya sekta nyeti sana na yenye umuhimu sana Kwa Taifa lolote lile linalohitaji kupiga Hatua ya kimaendeleo kutoka Hatua moja kwenda Hatua nyingine,na elimu hiyo inatoka kizazi kimoja kwenda kizazi kingine Kwa kutumia maarifa waliyoyapata au kufundishwa kwa kuyasambaza maarifa hayo Kwa kizazi kingine.

Licha ya Kuwa na Idadi kubwa ya shule na Vyuo pamoja na idadi kubwa ya watu wanaopata elimu kuanzia elimu ya awali mpka elimu ya Ngazi ya Chuo kikuu bado elimu imeonekana kuwa Haina Msaada ule ambao tulioutarajia Kwa kuwa bado tuna idadi kubwa ya watu ya wasiojua kusoma Wala kuandika Licha walipita shuleni kusoma,tuna Wasomi wengi ambao elimu zao hazijawakomboa Kwa kuwa mizigo Kwa familia na jamii Kwa kutoweza kujiajiri au kutumia elimu walizonazo kutatua shida na kuleta maendeleo katika jamii na Kwa Taifa Kwa ujumla.

Ili tuweze kufikia Tanzania Bora tuitakao zifuatazo ni baadhi ya mambo ambayo wadau wa elimu na serikali Kwa ujumla waweze kuzizingatia na kuzifata katika kuboresha sekta ya elimu iweze kuwa msaada Kwa vijana wa Sasa na kizazi kijacho.

1:Ubadirishaji wa sera na mitaala ya Elimu isiyokuwa na faida Kwa Taifa letu

Elimu yetu ya Tanzania Iko katika mfumo wa 2+7+4+2+3 Kwa maana Mtu anaanza Elimu ya chekechea Miaka miwili(2),elimu ya Msingi Miaka Saba(7),Elimu ya sekondari miakaminne(4),elimu ya advance Miaka miwili(2),elimu ya chuo kikuu Miaka mitatu mpka mitano(3-5),Hivyo Msomi anatumia Miaka yote hiyo lakini bado anashindwa kujikimboa kwasababu elimu anayoipata ni ya kukariri.

Hivyo katika kubadirisha sera na Mitaala ya elimu basi serikali na wadau wa elimu wazingatie mambo yafuatayo

i. Upunguzaji wa miaka ya kusoma Kwa mwanafunzi ili asiweze kutumia muda mwingi shuleni na kushindwa kupata aina nyingine ya elimu kama elimu ya fedha na elimu binafsi itakayomsaidia kuboresha maisha yake.

ii. Ufutaji wa baadhi ya maudhui na masomo yasiyo na tija Kwa wanafunzi.

Mfano usomaji wa Historia za nchi nyingine ambazo wao hawasomi Historia za nchi yetu,pia kwenye masomo ya sayansi kusoma vitu ambavyo hatuwezi kuvitumia popote.

iii.Ufutaji wa kozi za Vyuo kikuu zisizohitajika katika soko la ajira

Hii ni kutokana na Watanzania wengi wanatagemea elimu kupata ajira hivyo haitopendeza kuanzisha kozi ambazo hazihitajiki katika soko la ajira na kusababisha upotevu wa muda Kwa vijana.

iv. Ufutaji wa mitihani ya machaguo kwasababu upunguza Uwezo wa mwanafunzi kufikiria.

v. Upangaji mzuri wa Grade katika kutengeneza kizazi Cha watu wenye upeo Mpana wa kufikiri na sio kuleta huruma za kuwabeba watu wasio na sifa Kwa kigezo Cha Kila mtoto afaulu ili ionekane sekta ya elimu imeboresha na kupandisha elimu jambo ambalo litatuletea matatizo na kujichimbia kaburi wenyewe kwa kizazi kijacho.

2: Uanzishwaji wa shule za Ubunifu na kurejesha masomo ya kujikimu shuleni .

Ni suala lisilopingika kuwa watoto wanazaliwa na vipaji mbalimbali,hivyo upungufu wa shule za Ubunifu imepelekea watoto wengi kupoteza vipaji vyao kwasababu hakuna sehemu wanapoonyesha vipaji zao zaidi ya kukutana na mitaala inayowataka waweze kukariri na kujibua mitihani siku ya mwisho.

Pia kurejesha masomo ya kujikimu kama stadi za kazi na sayansi kuku itaweza kuwaandaa wanafunzi kuwa na Uwezo wa kuweza kujitegemea mara baada ya kumaliza shule na kuwa msaada Kwa familia zao na jamii zinazowazunguka na Taifa Kwa ujumla kutokana na Uwezo walionao mbali na elimu ya kukariri tunayofundishwa darasani.

3: Kuwa na katiba na Mpangilio mzuri wa elimu ambao hautoathiriwa na siasa

Elimu yetu ya Tanzania imekuwa na shida sana hii ni kutokana na wanasiasa na viongozi wa serikali kuona kwamba wanaweza kusema chochote na kuamua chochote katika sekta ya elimu jambo ambalo linahatarisha Usalama wa sekta hii ya elimu.

Mfano.Kiongozi anaweza kusema kuanzia Sasa hakutokuwa na masomo ya ziada “Tuition” Kwa wanafunzi au walimu waweze kufundisha masomo yote hata kama hajasomea masomo hayo mengine.

Hivyo katiba na Mpangilio huo unaweza kuandaliwa na serikali Kwa wizara inayohusika,wadau wa elimu na ushirikishwaji wa wazazi ambao Muongozo huo utapitishwa na kubadirika kutokana na Uhitaji Kwa jamii Kwa muda huo na sio kuruhusu mtu mmoja Kwa manufaa au hisia zake aweze kubadirisha.

4: Uboreshaji wa miundombinu na matumizi ya teknolojia mashuleni .

Dunia ya Sasa inaongozwa na sayansi na teknolojia Kwa kiasi kikubwa ahivyo katika sekta yetu ya elimu hatuna budi kubadirika na sisi kuendana na utandawazi ili kuifanya elimu ilete maslahi chanya katika jamii yetu na kuendana na wakati.

Hivyo Ujengaji wa madarasa ya kisasa yanayoruhusu matumizi ya teknolojia ,uachaji wa matumizi ya njia za kufundishia zilizopita na wakati,Kuwa na walimu wataalamu wanaoweza kutumia teknolojia kwakupatiwa semina na mafunzo.

5: Uzingatiaji wa Maslahi ya Walimu Kwa kuzingatia Aina ya masomo wanayofundisha.

Si jambo la kushangaza kuona shule walimu wa kiswahili wako wengi lakini mwalimu wa hesabu yupo mmoja ambalo anafundisha masomo mengi tofauti na wale wa kiswahili lakini mishahara wanapokea sawa jambo ambalo limekatisha Hali ya kujitoa na kujituma Kwa walimu wa sayansi na kufanya kulipua kazi wanapofundisha na kuleta shida ya uelewa Kwa wanafunzi.Hivyo kuifikia Tanzania tuitakayo ni vyema tukaongeza idadi ya walimu wa sayansi na pia kutofautisha uzito wa kazi anayofanya na maslahi yake kama yanaendana.

6: Kuichukulia Kwa Uzito sekta ya Elimu .


Imezoeleka kuwa Anayepata daraja la chini ndiyo huyohuyo anayekwenda kusomea ualimu jambo ambalo linahatarisha sekta ya elimu kwasababu tunapunguza ubora wa elimu Kwa kuandaa kizazi dhaifu,hivyo ni vyema tukabadiri utaratibu kuwa hata waliopata daraja la kwanza la ufaulu wanaweza kuingia sekta ya elimu na kufundisha ili tuweze kuandaa kizazi kilicho Bora na Cha wasomi.Hii utaweza kufanikiwa kama walimu watazingatiwa Maslahi Yao kama sekta zingine Kwa kuongezea mishahara ili isionekane kuwa ni sekta ya watu maskini na watu wavivu wa kufikiria.

Imeandaliwa na kuandikwa na
JOHN ELIYA HAULE
 
Upvote 2
Back
Top Bottom