SoC04 Tanzania tuitakayo lazima tuweke misingi Bora na endelevu katika kilimo

SoC04 Tanzania tuitakayo lazima tuweke misingi Bora na endelevu katika kilimo

Tanzania Tuitakayo competition threads

halima_ chikota

New Member
Joined
May 21, 2024
Posts
2
Reaction score
2
UTANGULIZI
Tanzania tuitakayo lazima tuweke misingi Bora na endelevu katika kilimo. Hii ni sekta nyeti ambayo inamchango mkubwa katika uchumi wa nchi zaidi ya asilimia 25 na kuajiri nguvu kazi zaidi ya asilimia 75. Lakini sekta hii inachangamoto mbalimbali kama mabadiliko ya tabianchi, miundombinu mibovu ya kilimo na ufinyu wa elimu kwa elimu kwa wakulima.

Ili kufikia Tanzania tuitakayo katika kilimo lazima tuwekeze katika mageuzi ya kilimo yatakayoboresha uzalishaji endelevu, kuongeza thamani za mazao na mifugo yetu.

RAMANI YA TANZANIA YA KILIMO
maps_crops_suitability.jpg

Chanzo: ukurasa wa serikali ya wizara ya kilimo Tanzania​

MALENGO MAKUU
1. Kuongeza ufanisi wa kilimo na uzalishaji. Wakulima waboreshewe mazingira mazuri ya uzalishaji kwa kutumia mbinu za kisasa, mbegu Bora na viuatilifu pia matumizi ya teknolojia mfano (GIS_ geographic information system) ili kutambua aina ya udongo na kilimo sahihi kitakachofaa katika eneo husika. Kwa kufanya hivyo itasaidia kuokoa muda na gharama za kilimo kwa maana endapo wakulima watalima bila kujua aina ya udongo mwisho wa siku hawatapata chochote pia itasaidia wakulima kujua namna sahihi ya ulimaji ili mazao yasiweze kuteketea na mafuriko.

DRONE ZA KILIMO
precision-agriculture-1920x1080_tcm78-162278.jpg

chanzo: Shirika la kilimo Arusha
2. Kupanua masoko ya mazao ya kilimo. Kupitia teknolojia tunaweza kuanzisha mfumo wa wakulima kujua masoko na kupata habari na mawasiliano kuhusu bei sahihi ya bidhaa lakini pia tunaweza kuongeza masoko ndani na nje ya nchi hii pia itasaidia kukuza uchumi wetu, tunapanuaje masoko? Kwa kuboresha mazo yetu na kuongeza thamani za kimataifa lakini pia kwa kutumia fursa zilizopo kwenye mazingira yanayotuzunguka kwa usahihi.

EImfEhUWkAAEAAd.jpg
3. Elimu na mafunzo endelevu kwa wakulima. Wakulima wapewe elimu na mafunzo mbalimbali juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu, mbinu nzuri ya kustawisha kilimo, vilevile kuboresha mtaala wa elimu kuhusu kilimo na elimu ya kilimo ianzwe kufundishwa kuanzia shule za misingi, sekondari na vyuo vikuu, pia kwa upande wa taasisi wapate programu nyingi zinazolenga kuongeza elimu kwa jamii.
WAKULIMA WAKIPEWA ELIMU YA KILIMO
img-20210503-112537-1024x576.jpg
Chanzo, gazeti la wananchi
4. Kuhimiza kilimo endelevu na kinachostahimili. Msimu wa mvua tunaona athari nyingi zikitokea za mafuriko kutokana na kutowepo na mazingira mazuri ya kuhifadhi maji ya mvua ambayo yangeweza kutumika wakati wa kiangazi kwa kilimo cha umwagiliaji au matumizi mengine.

5. Uwepo wa mikopo. Taasisi za serikali na binafsi za fedha zitoe mikopo kwa wakulima kwa masharti yasiyomuumiza mkulima na watoe elimu ya mikopo hiyo ili iweze kuleta tija kwa jamii na sio kudhoofisha Kama ilivyotokea maeneo mengi nchini hasa vijinini.

MATARAJIO YA MALENGO
1. Ongezeko la kipato, uzalishaji wa mazao endelevu zaidi na yenye ubora wa juu itasaidia kuongeza kipato cha wakulima na Pato la taifa kwa ujumla. Hii utatokea kama tutapata masoko ya mojakwa moja.

ELsPAavXYAAXGE5.jpg

2. Kuongezeka kwa mazao, kutokana na elimu wakulima wataweza kununua mbolea na mbegu za kisasa ambazo zinauwezo mkubwa wa kujizalisha lakini pia kuendelea kwa teknolojia za machine ya ulimaji, kupandia na mashine ya kuvunia mazao lazima yataongezeka ukitofautisha na matumizi ya vifaa vya jadi kama jembe na shoka.

3. Kuongeza usalama wa chakula, uhifadhi wa mazingira na kupunguza mabadiliko ya tabianchi. Tukihifadhi maji ya mvua kwa ajili ya kilimo tutahifadhi mazingira na chakula na kupanda miti ili kukabiliana na hali ya hewa, vilevile kuwepo kwa nutrienti na kupunguza kiwango cha sumu kwenye chakula.

4. Kupata bei Bora na upatikanaji wa soko la nje. Kupitia masoko mapya tutakayoyapata wakulima watauza mazao Yao kwa bei nzurii na yenye kukidhi ambayo itasaidia kutatua baadhi ya changamoto katika shughuli ya kilimo, pia wataweza kuuza mazao Yao na mifugo kimataifa na kuongeza kipato na fedha za kigeni nchini mwetu.

5. Kuongezeka kwa ujuzi na uzalishaji Bora wa mazao. Kutokana na elimu na utekelezaji wa ujuzi walioupata itaongeza mbinu mbalimbali za kilimo ambazo zitaongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara.

6. Kupunguza upotevu wa mazao. Kutokana na upatikanaji wa pembejeo za kilimo, dawa za kuuwa wadudu na mbolea itamsaidia mkulima kulinda mazao ambayo yanaweza kushambuliwa na wadudu na kuweza kupoteza thamani ya zao hilo, vilevile ukuaji wa teknolojia itasaidia kupunguza upotevu wa mazao kwa kutambua maafa ambayo yanaweza kutokea mahsambani na kuweza kuyazuia mapema ili kuepukana nayo na kupunguza upotefu wa mazao na mifugo.

7. Matumizi Bora ya rasilimali. Ufanisi utaongezeka kwa kutumia rasilimali kama maji yaliyovunwa ya mvua kwa ajili ya umwagiliaji na kunywesha mifugo au hata maji hayo kuzalisha nishati ya umeme itakayoweza kutumika kwenye viwanda vya kusindika mazao vilevile rasilimali ya ardhi itatumika kutokana na uhitaji uliopo na kulinda mahitaji ya vizazi vijavyo bila kuathiri mahitaji yao.

8. Ongezeko la uwekezaji.kutokana na mikopo itakayotolewa kwa wakulima na wafugaji itawawezesha kupata zana imara za kisasa na teknolojia ya kilimo, mfano wataweza kununua trekta, kuongeza ardhi kwa kununua na kadhaalika, hivyo wakulima na wasio wakulima wataongeza uwekezaji katika kilimo na matokeo yake kupelekea kupata wageni kutoka nchi za nje watakaokuja kuwekeza na kuweza kuingiza fedha nchini.

HITIMISHO
kuanzia miaka mitano na kuendelea Tanzania inapaswa kuwa taifa lenye sekta ya kilimo iliyoboreshwa yenye uzalishaji mkubwa, inayotumia teknolojia za kisasa, na inayohakikisha ustawi wa wakulima na uhifadhi wa mazingira. Mafanikio katika sekta ya kilimo yatatoa mchango mkubwa katika kupunguza umasikini, kuongeza ajira na kuimarisha uchumi wa nchi. Ni jukumu la kila mtu kushirikiana na serikali katika katika kutimiza azma hii.
 
Upvote 2
kufikia Tanzania tuitakayo katika kilimo lazima tuwekeze katika mageuzi ya kilimo yatakayoboresha uzalishaji endelevu, kuongeza thamani za mazao na mifugo yetu.
Sawa kabisa.

na viuatilifu pia matumizi ya teknolojia mfano (GIS_ geographic information system) ili kutambua aina ya udongo na kilimo sahihi kitakachofaa katika eneo husika. Kwa kufanya hivyo itasaidia kuokoa muda na gharama za kilimo
Kisasa na kisayansi kabisa.

Kupanua masoko ya mazao ya kilimo. Kupitia teknolojia tunaweza kuanzisha mfumo wa wakulima kujua masoko na kupata habari na mawasiliano kuhusu bei sahihi ya bidhaa lakini pia tunaweza kuongeza masoko ndani na nje ya nchi hii pia itasaidia kukuza uchumi wetu, tunapanuaje masoko? Kwa kuboresha mazo yetu na kuongeza thamani za kimataifa lakini pia kwa kutumia fursa zilizopo kwenye mazingira yanayotuzunguka kwa usahihi.
Naipenda hii point, yaaani hapa tukipaweza tu mbona tumepiga hatua.
S
. Kupata bei Bora na upatikanaji wa soko la nje. Kupitia masoko mapya tutakayoyapata wakulima watauza mazao Yao kwa bei nzurii na yenye kukidhi ambayo itasaidia kutatua baadhi ya changamoto katika shughuli ya kilimo, pia wataweza kuuza mazao Yao na mifugo kimataifa na kuongeza kipato na fedha za kigeni nchini mwetu.
Husha nondo. Endelea kushusha nyundo bibiee👏

Matumizi Bora ya rasilimali. Ufanisi utaongezeka kwa kutumia rasilimali kama maji yaliyovunwa ya mvua kwa ajili ya umwagiliaji na kunywesha mifugo au hata maji hayo kuzalisha nishati ya umeme itakayoweza kutumika kwenye viwanda vya kusindika mazao vilevile rasilimali ya ardhi itatumika kutokana na uhitaji uliopo na kulinda mahitaji ya vizazi vijavyo bila kuathiri mahitaji yao.
Exactly ahsante sana.

DRONE ZA KILIMO
Haukuizungimzia hii lakini wacha tu nikuulize mawazo yako. Je ni sahihi kuwekeza katika drone katika haya mazingira yetu ambayo watenda kazi ni wengi na wenye gharama nafuu?
 
Sawa kabisa.


Kisasa na kisayansi kabisa.


Naipenda hii point, yaaani hapa tukipaweza tu mbona tumepiga hatua.
S

Husha nondo. Endelea kushusha nyundo bibiee👏


Exactly ahsante sana.


Haukuizungimzia hii lakini wacha tu nikuulize mawazo yako. Je ni sahihi kuwekeza katika drone katika haya mazingira yetu ambayo watenda kazi ni wengi na wenye gharama nafuu?
Ahsanteeee kwa swali hii drone nimeweka kama mfano wa teknolojia ambayo itatusaidia kuokoa muda kwa kufanya kazi kwa muda mfupi na eneo kubwa hii inakuwa tofautii na watenda kazi hivyo basi wakulima wakiwezeshwa na kupewa ujuzi wa teknolojia kama hizi zitaongeza uzalishaji
 
Back
Top Bottom