SoC04 Tanzania tuitakayo: Maboresho katika nchi yetu miaka 5-25 ijayo

SoC04 Tanzania tuitakayo: Maboresho katika nchi yetu miaka 5-25 ijayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

qutiepie

New Member
Joined
Jun 24, 2024
Posts
1
Reaction score
0
Tanzania inaweza kuwa nchi yenye mafanikio makubwa miaka 5-25 ijayo kutokana na sababu kadhaa ambazo zikifanyiwa maboesho kidogo zinaweza kuleta maendeleo makubwa sana hapa nchini.

Kwanza kabisa tunazo rasimali asilia kama vile madini, gesi, ardhi yenye rutuba. rasilimali hizi endapo zitatumika vizuri basi itakuwa rahisi kwetu kuifanya nchi yetu kubalika na kukuza uchumi wa nchi yetu kwa ujumla ambapo tutapata fursa za wawekezaji na kukuza sekta ya uchimbaji na uchakataji rasilimali.

Pia, Tanzania ni kitovu cha utalii duniani; hapa nchini tuna vivutio vingi vya utalii kama vile mbuga za wanyama sehemu za maonesho, fukwe za kuvutia, ambapo kama nchi yetu ikiboresha zaidi maeneo hayo ya utalii hii itapelekea kupata watalii wengi kutokea nchi mbalimbali ambapo tutapata fedha za kigeni na hii itakuwa faida kwetu kwakuwa pato la nchi yetu linazidi kukua lakini pia tunaweza kuwapatia ajira vijana wetu wakitanzania kama watu wanaowasimamia watalii hao.

Lakini pia serikali inaweza kuweka sera za uwekezaji na kuendeleza sekta mbalimbali kama vile kilimo, viwanda na nishati. Kwa kuwekeza katika miundombinu bora, elimu na afya, tunaweza kujenga mazingira mazuri ya biashara na kukuza uchumi wetu.

Pia serikali ifanye uwekezaji katika miundombinu kwa kuoresha barabara, reli, bandari, na viwanja vya ndege kama ilivo sasa tayari kuna sehemu mbalimbali zimefanyiwa marekebisho na matatizo yamepungua jambo hili likiendelea ndsni ys misks mitano ijayo itatusaidia nchi yetu kuwa bora hapa duniani kwasababu hakutakuwa na changamoto tena za miundombinu, lakini pia biashara zitazidi kukuwa na kufika mbali kimataifab zaidi.

Kuendeleza sekta ya kilimo; pia sisi watanzania tunatakiwa kutumia vyema ardhi yetu kwa kufanya kilimo zaidi kwakuwa tuna ardhi yenye rutuba katika maeneo mengi hapa nchinilakini pia serikaliinabidi ichangie kwa kutoa mafunzo kwa wakulima namna ya kutumia njia za kisasa katika kilimo hii itapelekea uzalishaji kuwa mkubwa zaidi na kupata wawekezaji wengi zaidi.

Kukuza sekta ya viwanda; Kwa kuwekeza katika viwanda, tunaweza kuongeza thamani ya malighafi zinazozalishwa nchini na kuunda ajirazaidi. Viwanda vya nguo, vifaa vya ujenzi, na usindikizaji wa mazao ya kilimo ni baadhi ya maeneo yanayoweza kuimarishwa hususani maeneo ya vijijini ambapo kilimo hufanyika zaidi kutokana na kuwepo kwa maeneo mengi ya kilimo.

Kupambana na ufisadi; kwa kuimarisha mfumo wa sheria ambao utakuwa mgumu na kuwafanya watu kuhofia kufanya vitu vya ufisadi , kuwa waaminifu katika manunuzi ya umma, na kuchukua hatua kali dhidi ya fisadi utakaofanyika, kwa kufanya hivo tunaweza kujenga mazingira ya biashara yenye uadilifu na kuwavutia wawekezaji.

Kupambana na umaskini; Kwakuwekeza katika miradi ya maendeleo ya jamii, kutoa misaada kwa familia za kimaskini, na kukuza shughuli za kiuchumi za watu wasio jiweza kifedha, tunaweza kuounguza pengo la pato na kuboresha hali ya maisha kwa watu inaweza ikawa kwa kuwasaidia kupata nafasi za kazi lakini pia zile familia ambazo hazina uwezo wa kufanya kazi kuwapatia msaada wa vitu vya kukidhi mahitaji yao muhimu mfano chakula, makazi pamoja na mavazi kwa kufanya hivi kutasaidia nchi yetu kuweza kukua nakuwa nchi bora duniani kwa kuwa imewweza kupambana na umaskini kwa nafasi kubwa ncini.

Yapo mawazo mbalimbali ya kuifanya Tanzania iwe miaka mitano ijayo, lakini ili haya yote yatimie inabidi sisi kama watanzania tunaoipenda nchi yetu tunatakiwa tuwe na ushirikiano mzuri lakini pia kuwa ni mipango madhubuti kikubwa zaidi ni kuwa na uongozi imara zaidi hii itatusaidia kufikia malengo yetu sisi kama Watanzania.
 

Attachments

  • tz-flag.jpg
    tz-flag.jpg
    596.1 KB · Views: 3
Upvote 4
Back
Top Bottom