OPG
New Member
- Jan 8, 2023
- 1
- 1
STORIES OF CHANGE SEASON 04
TANZANIA TUITAKAYO
(Let's talk about our Country?
Tuzungumzie Nchi Yetu, Nchi ambayo ina safari Ndefu sana ya mafanikio,Mafanikio ambayo sisi watanzania tunataka kuyafikia na sio tu kuishia kuyaota. Mafanikio ambayo tutayapata kama tukiamua kuyapigania kwa uwazi na uwajibikaji,
Mafanikio ambayo yamegawanyika kwenye sekta mbalimbali ambazo tukizitilia mkazo basi tutatoboa na kufika kulee tutakapo katika miaka 5-25.
Mimi leo nimeamua kuvunja ukimya ili Nchi yangu ifike kule ambapo wengi wetu tunatamani tufike kimafanikio hasaa kwenye Sekta ya Afya. Na nianze kwa kusema Afya ni mtaji na Nchi bila kuwa na watu wenye Afya bora basi haifiki popote kwani bila afya hakuna utendajikazi wowote mzuri utakao fanyika. Kutokuwa na afya Bora kunasababisha uwajibikaji na ubunifu katika kufikia malengo ya mafanikio yetu kwenda taratibu kama Kobe na kufa kabisa, Hapa nazungumzia Afya katika maeneo ma nne tu ambayo Serikali ikiweza kutilia mkazo na kuwekeza nguvu kubwa hapo basi tutafika mbali sana.
1•Nazungumzia Bima Ya Afya (NHIF)
Nianze kuipongeza serikali kwa mpango mzuri walionao kuhusu utoaji Bima kwa kila mtanzania, Japo bado Serikali inatakiwa kuangalia Kwa jicho la tatu eneo hili ili kuboresha kabisa kwani Afya ni mtaji. kwenye Bima hapa nitazungumzia mambo ma wili ambayo Serikali ikiyaboresha zaidi basi kwenye Sekta ya Afya tutafika mbali sana, na nianze kuzungumzia Time Frame.
•Time Frame-Ninapozungumzia time frame namaanisha muda wa ukataji na upatikanaji wa huduma za Bima, kwamba Serikali isimamie uboreshaji wa upatikanaji wa huduma za Bima mapema tu baada ya mwananchi husika kukata bima hiyo yaani asisubiri ile miezi mitatu ndo apate bima kwani hapa ndani ya miezi hiyo mitatu anaweza kuugua na kujigaramikia mwenyewe wakati akisubiri bima. Na kingine Serikali inatakiwa isimamie utoaji wa elimu mara kwa mara kabla ya upatikanaji wa bima haswa kwa watu wanye ulemavu mfano ( watu wenye matatizo ya usikivu na wenye uwoni hafifu). Pia kwa wale wasio jua kusoma na kuandika.
•Huduma Za Bima- Pia Serikali iboreshe huduma zinazopatikana ndani ya bima kwa mlengo wa kuongeza huduma muhimu za matibabu ili mtu anapoenda kutibiwa apate kutibiwa magonjwa yote na sio kukuta baadhi ya magonjwa hayapo kwenye utumiaji wa bima husika, kama ilivyo sasa magonjwa mengi muhimu kutibiwa ndio yanalipiwa cash lakini magonjwa ya kawaida yanakuwepo kwenye Bima kitendo ambacho kinapelekea mtu kuona hakuna umuhimu wa kuwa na bima maana bima sikuizi inageuka kuwa pambo tu kusubiri mtu augue Malaria.
2•TAFITI(RESEARCH)
Katika kuzungumzia tafiti hapa ninazungumzia hasa kuhusu vibali Serikalini ambavyo ni muhimu sana katika sekta ya Afya Nchini. Maana kumekuwa na taasisi mbalimbali za kiserikali na binafsi ambazo zimekuwa zikifanya vizuri sana katika maswala ya tafiti kwenye Sekta ya Afya hapa Nchini. Na mfano wa baadhi ya miradi hiyo ni pamoja na National Bureau of statistics (NBC), Tanzania Food and Frugs Authority (TFDA), The National Institute for Medical Research (NIMR), Commission for science and technology (COSTECH).
Taasisi hizi zote zinajihusisha na maswala ya tafiti mbalimbali kuhusu sekta ya Afya na baadhi ya tafiti nyingi zinachelewa kufanyiwa kazi kwasababu ya ucheleweshwaji wa vibali hivyo basi Mimi niiombe Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iweze kukaa kitako pamoja na kamati ya maadili ya usimamizi wa Afya Nchini ili iweze kurahisisha upatikanaji wa vibali kama taasisi zimefanya kila kilichotakiwa .
3•VIFAA VYA UTOAJI HUDUMA HOSPITALINI
Hapa nitajikita kwenye vifaa kwaajili ya wakina Mama kujifungua kwani vimekuwa vya shida sana. Maana kuna baadhi ya vitu vya muhimu sana ambavyo wakati wakujifungua vinatakiwa kuwepo lakini unakuta muhusika anatakiwa kununua mwenyewe kwani havipo hospitalini.
4•Elimu Ya Afya Kwa Jamii
Elimu ya Afya kwa Jamii inatakiwa sana hasa kwa magonjwa haya ya milipuko na magonjwa yasio ambukiza mfano magonjwa ya Moyo, Presha, Damu, Figo, na mengine mengi. Kwahiyo kuwepo na elimu ya kutosha
HITIMISHO
Tanzania tuitakayo ni Tanzania ambayo inatoa fursa kwa watanzania kutoa maoni yao kwa uhuruna na ushauri juu ya ubora wa Nchi yao, Tanzania ambayo inasikiliza na kufanyia kazi yale mambo ya muhimu kwaajili ya mabadiliko ambayo Wananchi wake wanayatazamia na kuyazungumzia, Tanzania isiyoogopwa na wananchi wake kuwa ukifungua mdomo kuzungumzia haki na maendeleo ya Nchi yako basi umekwisha, Tanzania tuitakayo ni Tanzania yenye wananchi wenye Afya bora na sio Bora Afya.

Upvote
3