change is inclusive
New Member
- May 27, 2024
- 3
- 2
Serikali ya Tanzania,
Lini tutaweka nia
Kuhakikisha tunachodhamilia, kinatokea?!
Rushwa ni adui wa maendeleo
Anaitesa Tanzania mawio mpk machweo
Waulize mama ntilie wakujibu kwa kilio,
Halafu huwezi amini inawapendelea wenye vyeo.
Rushwa ni janga
Hatutaweza kujenga
Tukiendelea kujiganga
ninahakika tutashinda
linaathiri ngazi zote za jamii yetu.
Ni muhimu tuweke mikakati thabiti na bunifu ili kutokomeza, Hapa chini, kwetu.
Taasisi za kupambana na rushwa Ni nini mmekikosa? rasilimali? Ama uhuru wa kutosha?
kutekeleza majukumu yenu kikamilifu.
Bila nguvu na uhuru,
hamuwezi kushughulikia kesi kubwa kama kesi za Ushuru?
Serikali na taasisi zake zinakosa mifumo madhubuti ya uwazi! WanaNnchi tunashindwa kuhoji uwajibikaji.
Mikataba inasainiwa kimya kimya bila mahujaji?
Kukosekana kwa uwazi
kunafanya kupambana na rushwa inakuaja kazi
iwe rahisi kwa maafisa wafisadi kujificha nyuma ya pazia.
Rushwa imekuwa tamaduni yetu
Tunalipia hadi kupata haki zetu
kama sehemu ya utamaduni ambapo watu wengi wanaukubali kuitumia kwenye kila kitu.
Hii inafanya kuwa vigumu kuushughulikia bila mabadiliko makubwa ya kijamii labda ashuke Kristu.
Rushwa imewapa Ulinzi wa Watu Wenye Nguvu
Hawana wasiwasi wanauza hadi pembe za ndovu
wanapata kinga dhidi ya sheria sisi wengine tumekalia kuti kavu.
Hii inavunja moyo wale wanaotaka kupambana na Rushwa bila uvivu
Lakini, kuna Suluhisho....
Hakuna tatizo lisilo na mwisho
Kutengeneza njia bora za malisho,
Kila mtu anataka kilicho bora kwa
kwa Tanzania ya kesho.
Kuimarisha Taasisi za Kupambana na Rushwa
Takukuru wanahitaji rasilimali mfano, camera za kidigitali,
Zitakazo wasaidia kupata taarifa halali,
Tunahitaji kuwapa uhuru wa kutosha
Wapewe mafunzo ya kina na vifaa vya kisasa.
Hii itawezesha taasisi hizi kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kushughulikia kesi kubwa za rushwa usiku kucha.
Mifumo yetu ya Uwajibikaji
Ni kama mifumo ya maji
Tunahitaji mifumo madhubuti
Inayotupa hari ya kukaza buti
Kuhakikisha maafisa wote wa umma wanawajibishwa na hakuna short cut,
Barabarani imekua kawaida
Kuacha elfu tano kila muda
Tunahitaji ripoti zisomwe kila mwezi
inaweza kujumuisha ukaguzi
wa mara kwa mara na ripoti zenye uwazi.
Uwajibikaji kwa vyombo vya dola
utazuia vitendo vya ufisadi na kuhakikisha maafisa wanatoa huduma bora.
Tunahitaji mijadala ya kitaifa kampeni na madarasa ya kuelimisha
kuhusu athari za Rushwa
Kwasababu ndizo zinatuchelewesha
Kuifikia Tanzania bora ilioboreshwa
Shirikisha shule na vyuo
Toa elimu kwa mtaala wao
Hawa Ndio Tanzania ijayo
Uwajibikaji liwe ndilo darasa lao
Elimu itasaidia kubadilisha mtazamo
wa jamii, na watu wa makamo, kuhusu ufisadi na Rushwa na kuunda utamaduni wa uadilifu, kwa vijana wenye nia na maono.
Tuwekeze mifumo ya kidigitali katika huduma za umma
ili kupunguza mawasiliano ya nyuma nyuma
Na kupeana pesa kimya kimya
Matumizi ya e-governance yanaweza kuongeza ufanisi
Na kufanya mambo yawe rahis
Teknolojia itaweza kupunguza nafasi za rushwa,
na kuimarisha ufuatiliaji wa huduma za umma bila kupotoshwa.
Serikali iwape watu binafsi
Nawa wao wapate nafasi
uchunguzi ufanywe kwa kasi
Wapewe leseni bila ubishi,
Hii inaweza kujumuisha makampuni binafsi ya uchunguzi,
Yaliobobea kwenye kazi,
ambayo yanaweza kusaidia serikali kufuatilia na kushughulikia kesi,
Kampuni binafsi vinaweza kuleta utaalamu na ufanisi, wataleta
shinikizo kwa maafisa wa umma kuwa waadilifu kwa kujua kuwa wanachunguzwa kwa karibu. Hivo kufanya kazi kuwa Rahisi.
Tuachane na namba za simu hewa
Nyingi unapiga bila kupokewa
Ni kama zimewekwa kuchezewa
Anzisha namba ya simu ya dharura, Watu waweze kurepoti bila hila,
Mifumo iwape watu utambulisho usiojulikana
Waweze kutoa taarifa kwa mapana
Hakikisha simu hizi ni za siri na zinalindwa ili kutoa usalama
Simu ya dharura itawezesha wananchi kuripoti vitendo,
Vinavyofanywa kuchelewesha jambo
Na hivo kusaidia utatuaji na upatikanaji wa ushahidi wa vitendo vya ufisadi.
Tanahitaji nafasi salama
Yanayoturuhusu sisi kusema
Na majadiliano yenye maana ambapo wananchi wanaweza kujadili
Na kuweka wazi kila dili
Rushwa inapoteze maadili
Yakazi na utu na vile vizawadi zawadi,
Ndio vinafanya mtanzania asie na dozi
Kushindwa kupata utetezi.
Tuwape wananchi Nafasi za kuelezea matatizo yao na kusaidia kuchochea mabadiliko ya kijamii vita dhidi ya rushwa.
Kuna waandishi wa habari?
Wamenyamazishwa kweli?
Serikari ikiwapa ulinzi
Wasikamatwe kama nzi
Wapate nafasi za uchunguzi
Kwenye mazingira yalio wezeshi
KuToa taarifa kwa usalama
Kuna mengi wanaweza sema
Kuhusu mihadarati, rushwa na usalama wa wanyama,
Wachunguzi wa kiserikali na wa kibinafsi wanapaswa kupewa ulinzi wa kutosha.
Kutuweza na kutuaminisha,
hii vita haijatushinda.
Usalama wa wachunguzi utahakikisha kwamba wanaweza kufanya kazi yao bila hofu ya kulipiziwa kisasi,
hivyo kuongeza ufanisi na kutokuogopa Risasi.
Ni muhimu kuchukua hatua hizi kwa haraka,
Rushwa tuione kama talaka,
Ina nia ya kututeka
Rushwa inachangia umaskini, inasababisha tukose pesa ya sabuni,
ukosefu wa huduma bora,
Kote visiwani na bara,
Inakwamisha maendeleo ya taifa. Serikali inapaswa kuonyesha Taarifa,
katika kupambana na rushwa na kuweka mbele maslahi ya wananchi.
Kuruhusu vitengo binafsi vya uchunguzi, Mashirika binafsi ya Uslama pamoja na mikakati mingine, kunaweza kuleta mabadiliko makubwa. Kwa pamoja, tunaweza kujenga Tanzania isiyo na ufisadi na yenye maendeleo endelevu.

Upvote
1