waryoba charles
New Member
- Jun 27, 2014
- 1
- 0
Sera ya elimu itaje na kusimamia ujuzi wa watoto kuanzia ngazi ya msingi hadi chuo kikuu.
Elimu ilenge kutoa wataalamu na wajuzi, watoto watambuliwe uwezo mapema katika ngazi za awali kielimu ili waanze kupewa mafunzo kulingana na sekta elekezi. Mfano, mwenye kipaji cha mpira apewe elimu ya utambuzi (Basic education) akishaelewa apewe mafunzo ya mpira. Mwenye mwelekeo wa kijeshi aelekezwe hayo, mwenye mtizamo wa ualimu aangaliwe masomo gani ana ufanisi obobee huko, mwenye mwelekeo wa sheria, udaktari, na kilimo na mengine mengi wote wapewe msingi wa mambo hayo.
Tupange kuzalisha wabunifu na wataalamu kila idara na tutoe watu wenye uelewa na wenye mapenzi toka moyoni kuhusiana na kazi husika, na mtu huyo ataijali na kuifanya kazi hiyo kwa uweledi maana ndipo ndoto zake zipo na akipoteza kazi hiyo hatakuwa na mlengo mwingine maana nchi nzima na mifumo ya nchi inamtambua huyo mtu kuhusika kwenye shughuli za idara hiyo tu. Tusipeleke watoto shule kusoma bila kujua cha kufanya baada ya masomo. Wengi huchagua cha kufanya wakifika vyuoni, yani anachagua vitu vitano tofauti tofauti kwamba kimoja kikigoma basi kingine na kingine hata ambavyo hana ufanisi wake.
Lengo kuu liwe kila mtu kutimiza ndoto na wajibu ili Wajasiriamali wazalishwe nchi nzima kuanzia mwanzo kabisa.
Nb.Mfumo tambuzi wa vipaji uwekwe kuanzia darasa la awali, wazazi washirikishwe na washiriki kutambua uwezo wa watoto tangu majumbani na serikali isimamie hilo. Baada ya miaka 25 ijayo nchi hii itakuwa na uchumi mzuri sana, michezo itakua kwa kasi, uwekezaji wa viwanda, biashara, wataalamu wa kilimo na ujenzi, walinzi wa taifa watakuwa wananchi wote wenye roho ya uzalendo, wanasiasa watakuwa watu mahili, wanasheria , walimu, madaktari, marubani, na mafundi wote watakuwa watu wazuri.

Upvote
0