SoC04 Tanzania tuitakayo miaka ya hivi karibuni

SoC04 Tanzania tuitakayo miaka ya hivi karibuni

Tanzania Tuitakayo competition threads

Edson Eagle

Member
Joined
Apr 20, 2024
Posts
30
Reaction score
12
Kwanza kabisa komasavaa wadau wote wa SOC 2024. Sauti tunazopaza katika makala hizi ziwe sauti zenye kuleta mabadriko kweli na zisiwe sautibubu zakuishia hapahapa jf. Mapendekezo yangu ni kama ifuatavyo kwa leo.

Wajibu na haki: serikali kupitia wizara husika ihakikishe sasa inatoa elimu na kila Mtanzania anatambua wajibu wake pamoja na haki zake kama raia, na pia kulisimamia hilo, Kuanzia viongozi mpaka wananchi wa kawaida, kwa kuielimisha jamii kupitia vyombo vya habari na mikutano mbalimbali. Hii itasaidia kuongeza uwajibikaji wenye kuleta maendereo na mabadriko chanya.
InCollage_20240523_104616774.jpg


Kutokomeza rushwa: niwakati sasa wakubadiri njia za kutokomeza rushwa inchini ikiwa ni pamoja nakuwa na mawakala wa siri na waaminifu kwa kushirikiana na PCCB. Lakini pia kuhakikisha taasisi husika inawajibika vilivyo bila ubaguzi, maana sababu yakubagua watu wenye madaraka na wananchi wakawaida na namna yakuchukua hatua imefanya mpaka sasa janga la rushwa linaenderea nchini, serikali ifanyie kazi hilo pia.
InCollage_20240523_104911490.jpg


Bajeti tosherevu: kila sekta iwe inapangiwa bajeti tosherevu yenye kuleta mabadriko na maendereo nchini hii itasaidia kukamilisha nakuanzisha mipango mbalimbali ya maendereo katika nchi yetu. Lakini pia kuhakikisha kila mwaka sekta husika imekamilisha majukumu yake kwa asilimia 100 kutokana na bajeti iliyopewa tena viwango vinavyotakiwa kinyume na hapo kuwe na sababu maalumu kutoka kwa viongozi husika inayokubalika lasivyo hatua zichukuliwe.
InCollage_20240523_104520104.jpg


Ajira na kujiajiri:
serikali ihakikishe inatengeneza mazingira ambayo yatatoa nafasi nyingi za ajira lakini pia uwezo wa vijana kujiajiri, tutoke kwenye ulimwengu wa kijana anamaliza chuo cha uhasibu then anaambiwa ajiajiri wakati huo hana hata mia mfukoni na elimu ya ujasriamali hana. Sasa elimu ya ujasriamali na ufundi stadi iwe kwa kila kijana na pia mikopo yenye riba nafuu iwepo kwa wingi na iwafikie walengwa sio kuambiwa kuna mikopo halafu haijulikani ilipo.
InCollage_20240523_104546605.jpg


Viongozi KUsikiliza kero za wananchi na kuzitatua. serikali ihakikishe Kuna utaratibu wa viongozi kusikiliza kero za wananchi nakuzifanyia kazi ama kuzitatua. Kuna baadhi ya viongozi wakishachaguliwa ndo basi tena, hana kabisa muda wakupita nakusirikiza kero za wananchi hatimaye maendereo yanadolola na wananchi wanateseka. Viongozi watambue wajibu wao na kama kiongozi anaonekana kushindwa basi avuliwe madaraka hafai.
InCollage_20240523_104838704.jpg


Kuacha kufumbiana macho kisa madaraka kila mtu awajibike: ni wakati wa serikali kuhakikisha kwamba viongozi hawafumbiani macho ili kila mtanzania haijalishi ni kiongozi ama raia wa kawaida awajibike sawasawa na nafasi yake. Tukienderea na hali yakujuana kindugu ambapo unakuta kiongozi fulani wa serikali hawajibiki ipasavyo lakini kwakuwa ni kiongozi hachukuliwi hatua yoyote basi maendereo tutabaki kuyasikia tu kwa wenzetu jarani.
InCollage_20240523_104651142.jpg


Baada ya kupendekeza hayo ni hitimishe kwa kusema kuwa maendereo yameshikiriwa na wajibu, haki, sheria isiyo bagua na uongozi bora. Maana vyote hivi ndivyo vitaweza kuendesha sekta zote inchini katika njia iliyobora na yenye kuleta mafanikio. BAADA YA HAYO YOTE NISEME TU KAZI IENDELEEEEEEEEEEEE.
 
Upvote 2
Ajira na kujiajiri: serikali ihakikishe inatengeneza mazingira ambayo yatatoa nafasi nyingi za ajira lakini pia uwezo wa vijana kujiajiri, tutoke kwenye ulimwengu wa kijana anamaliza chuo cha uhasibu then anaambiwa ajiajiri wakati huo hana hata mia mfukoni na elimu ya ujasriamali hana
Kwenye kujiajiri na ujasiriamali: sio sayansi ya maroketi hata ila soko. Ikifikia wakati fundi seremala wa mtaani anatengeneza bidhaa kama sofa na analiuza milioni mbili tatu bila wasi kama tunavyonunua yaliyotoka nje. Hatutahitajika hata kusubiri serikali itoe elimu ya useremala.
VIjana watajifunza hadi kwa youtube wenyewe, lakini bila soko lenye tija na thamani halisi ya jasho tutatafuta visingizio kila kona.

MAzingira ya nchi inayoruhusu kila mmoja kufikia uwezo wake halisi ndiyo haswa yatatusaidia

Kuacha kufumbiana macho kisa madaraka kila mtu awajibike: ni wakati wa serikali kuhakikisha kwamba viongozi hawafumbiani macho ili kila mtanzania haijalishi ni kiongozi ama raia wa kawaida awajibike sawasawa na nafasi yake
Hakika, kila mmoja na kazi yake apate haki atimizapo wajibu zake kihaki ova.
 
Back
Top Bottom