SoC04 Tanzania tuitakayo: Mitaala bora ni chanzo cha kufuta upungufu wa ajira uliopo sasa na miaka ijayo

SoC04 Tanzania tuitakayo: Mitaala bora ni chanzo cha kufuta upungufu wa ajira uliopo sasa na miaka ijayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

IamChris255

New Member
Joined
Jun 10, 2024
Posts
1
Reaction score
0
MITAALA BORA NI CHANZO CHA KUFUTA UPUNGUFU WA SOKO LA AJIRA TANZANIA

Habari za mdq huu ndugu zangu, Kama kichwa kinavyojielezq Mimi NI mwalimu wa shule ya msingi ambae nimefundisha mikoa tofauti tofauti nilichogundua katika utendaji wangu wa kazi ni kwamba Taasisi ya Elimu Tanzania imekuwa ikitoa mitaala ya kufundishia kila baada ya kipindi fulani cha miaka lakini mitaala hiyo haikidhi mahitaji ya walengwa kulingana na mazingira waliyopo.

Serikali ilipaswa kutoa mitaala inayomjenga mlengwa ambae ni mwanafunzi anapomaliza daraja la elimu ya msingi awe kamili kuweza kuyahimili mazingira yake. Pia kutokana na kukua kwa sayansi na teknolojia mtaala ulitakiwa utumie vifaa vya tehama zaidi kuliko kuandika sana ubaoni yani mtoto atende zaidi kuliko kuandika sana.

Katika Shule za maeneo ya Pwani ya bahari ya hindi kama vile maeneo ya kigamboni kata ya Pemba Mnazi na kimbiji watoto wengi hawasomi na pia kutomaliza masomo yako kutokana na kujihusisha na uvivu ambao wanaona unawalipa kuliko kwenda kupata elimu darasani sasa serikali ingekuwa imejikita kutengeneza mtaala kwa kuzingatia mazingira basi watoto kama hawa wangekuwa na somo linalohusu uvuvi salama ili kumjengea mtoto huyo hamu ya kufika shule kusoma kitu anachokifanya pia wanaoishi mazingira ya mjini kama vile Mwenge, kinondoni piq nao waandaliwe mtaala utakaohusisha mambo ya biashara kulingana na mazingira anayokulia na jamii inayomzunguka hivyo hvyo kwa wanaoishi mikoa ambayo shughuli kuu ni kilimo piq nao wawe na mtaala unaowezesha wao kukitumia kile wanachokisoma darasani.

Taasisi ya Elimu Tanzania inapofanya marekebisho ya mtaala izingatie pia kupata maoni ya walimu wanaofundisha shule hizo za msingi angalau kila kata walimu 50 ili kuwa na taarifa zinazojitosheleza kipi cha kuongeza au kupunguza katika mtaala wetu, pia mabadiliko hayo yazingatie uwezeshaji wa kina sio kulipua juu juu tu kwa mfano mtaala huu wa mwaka 2024 unaotumika kwa wanafunzi wa darasa la kwanza na la tatu haukuwa na maandalizi yanayomjenga mwalimu kuweza kutimiza malengo yaliyopanga na kufanikisha ufaulu unaotakiwa kwa watoto yani semina siku mbili na haijajitosheleza maana ukiuliza unajibiwa ingia mtandaoni kwenye link tuliyokupa utapata taarifa zote ambayo kimsingi haipo sawa walitakiwa wawezeshaji wawe na taarifa zote za kina.

Kulingana na hayo mtaala wetu uliopo ni sawa na kiongozi cha mwalimu tu au muongozo havina tofauti haubebi maana kamili ya mtaala wa kupunguza upungufu wa ajira kwa vijana wetu wanaopita katika elimu tofauti tofauti hivyo TET ifanye marekebisho sahihi kwa kuzingatia mambo hayo.

Asanteni
 
Upvote 0
Back
Top Bottom