SoC04 Tanzania tuitakayo: Namba maalumu ya huduma za utalii

SoC04 Tanzania tuitakayo: Namba maalumu ya huduma za utalii

Tanzania Tuitakayo competition threads

Johdoy2022

New Member
Joined
Jun 30, 2024
Posts
2
Reaction score
0
KWA NJIA YA NAMBA MAALUMU YA HUDUMA ZA UTALII.
Hii ni njia ya kisasa zaidi katika kuleta mapinduzi na upekee katika kutangaza utalii nchini, bila shaka kumekuwa na changamoto nyingi katika kukuza utalii na kuongeza idadi ya watalii nchini lakini je wanapokuja watalii kumi nchini tunawatumia watalii hao kuwaleta watalii kumi wengine? Tukiwa ni nchi inayoongoza kwa amani na ukarimu kwanini watalii wachague kwenda nchi ambazo hazina uhakika wa amani? tena pengine kwa sababu ya kufuata huduma ambazo sisi pia tunazo. JE TUNAKOSEA WAPI? TUNAWEZA WAPI?

NAMBA YA HUDUMA ZA UTALII?
hii ni namba maalumu ya simu ambayo mtalii wa ndani au wa nje ataipiga bure na kupata maelezo yote kuhusu wapi zilipo huduma za utalii, vituo vya afya, vituo vya usalama, huduma za jeshi la wanyama poli, huduma za waongoza watalii, huduma za hoteli, huduma za fukwe, vituo vya mabasi ya mikoani, huduma za viwanja vya ndege n.k

MFANO WA KUJIFUNZA: huduma za simu kupitia kampuni husika huwa na namba za dharura kwa wateja wao ambao zinasaidia kutatua changamoto za wateja, kutoa matangazo ya huduma zao, kupokea malalamiko ya wateja na kuboresha huduma zao.

JE SEKTA YA UTALII HAIWEZI KUIGA MFANO HUU?
Kwamba sasa watalii wa ndani na wa nje watapiga namba maalumu ya kiutalii kujua juu ya:-
Huduma za karibu za hoteli.
Vivutio vya utalii vilivopo karibu.
Kupata msaada wa dharura.
Kupata Msaada kwa askari wa wanyama poli.
Kupata msaada wa askari wa usalama.
Kupata huduma ya kituo cha karibu cha polisi.
Huduma ya usafiri wa kukodi.
Huduma za kampuni za utalii.
Kujua namnaa ya kufika kwenye ubalozi wa nchi husika.
Kujua matukio yanayotokea sasa ya kiutalii.
Kutoa malalamiko katika sekta ya utalii.
Kujua maduka makubwa ya bidhaa.
Kujua hospitali za karibu.
Kujua kumbi za starehe zilizopo karibu.
Kujua maduka makubwa ya kubadilisha fedha za kigeni.
Kujua namna ya kujihusisha na matukio ya kijamii nchini kama kuchangia makundi maalumu, kutoa msaada kwa mashirika yasiyo ya serikali, kufanya matukio la kitalii.
Kujua namna ya kukutana na vyombo vya habari.
Kujua taasisi za kigeni zilizo nchini n.k.

NB: JIULIZE MARA NYINGI ZAIDI KUTAKUWA NA RAHA GANI KAMA NAMBA YA SIMU YA HUDUMA ZA UTALII KAMA ITAKUFANYA KUJUA YOTE HAYO YALIYOTAJWA HAPO?

Mfano unapiga simu ya huduma ya utalii na kukutana maelezo haya;
1. Kuchangua lugha bonyeza Moja na kuendelea na lugha ya kiswahili bonyesha sifuri.
.. Kujua juu ya mlima Kilimanjaro na maeneo kitalii Tanzania bonyesha 1, kupata maelezo ya wizara ya utalii bonyeza 2, kujua hotel za nyota Tano ambazo zinatoa huduma kitalii Tanzania bonyeza 3, kujua juu ya vituo vya waongeza watalii bonyeza 4, kupata taarifa ya huduma za usalama kama vile zima moto, vituo vya Polisi na vituo vya wanyana poli bonyesha 5, kupata maelezo ya safari za ndege za ndani na nje ya nchi bonyesha 6, kutoka taarifa juu ya mtalii aliyepotea na changamoto ya kitalii bonyeza 7 na kuongea na mhudumu wetu bonyeza 9.

Huu ni mfano tu maelezo ya muhimu ambayo mtu atapata kwa kupiga simu kwa namba ya utalii.
MALENGO LA HUDUMA YA NAMBA YA UTALII.

KUWAFANYA WATALII KUJISIKIA SALAMA NA HURU WAKIWA TANZANIA.
Kupitia namba hii ya huduma kwa watalii kutawafanya watalii kujiona kuwa salama na karibu kupata msaada wa haraka inapohitajika.

KUTANGAZA HUDUMA ZA UTALII NA BIDHAA ZA UTALII
Kutangaza huduma za hoteli, huduma za usafiri wa kukodi, maeneo ya vivutio vya utalii kutasaidia sana mtalii kuwa na chaguo pana la kuchagua atakacho.


KUPUNGUZA NA KUONDOA WASIO WAAMINIFU KWA WATALII.
Kumekuwa na Watu wasio waminifu kwa watalii nchini ambao hutoa taarifa za uongo kwa watalii kwa lengo la kujinufaisha zaidi wao lakini kupitia mradi huu angalau mtalii atapata sehemu salama ya kujua juu ya huduma mbalimbali kuhusu utalii na watalii.
KUWASAIDIA WATALII KUPATA HUDUMA WANAZOHITAJI KWA HARAKA ZAIDI
Kwa kupiga namba ya huduma za utalii kutawasidia watalii kupata au kujua huduma za utalii zilizopo eneo husika kwa haraka.

KUKUZA NA KUTANGAZA UTALII
Bila shaka kupitia huduma hii watalii watafurahia na kuwafanya ndugu zao na marafiki zao kuja Tanzania kutalii siku za usoni.

Mwisho, Binafsi naamini huduma ya namba ya utalii imechelewa sana kuwepo na Sasa ni mda sahihi wa kuwekeza kwenye mradi huu, nimekuwa nikijaribu mara kwa mara kupata nafasi ya kuonana na Waziri mwenye dhamanna utalii my kumueleza jambo hili lakini nimekuwa ngumu kweli kweli hata hivyo nafurai kupata jukwaa la kutoka mawazo yangu ambayo naamini Waziri mwenye dhamanna ya utalii yatamfikia. Asante
 
Upvote 2
Back
Top Bottom