SoC04 Tanzania tuitakayo ni ile ambayo itatuleta pamoja watanzania bila kujali itikadi za vyama vyetu

SoC04 Tanzania tuitakayo ni ile ambayo itatuleta pamoja watanzania bila kujali itikadi za vyama vyetu

Tanzania Tuitakayo competition threads

Mashenene Robert

New Member
Joined
Dec 4, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Tanzania tuitakayo ni tanzania ambayo itatuleta pamoja watanzania bila kujali itikadi za vyama vyetu,dini au kabila. Na Tanzania hiyo itawezekana kuipata kwa juhudi zetu wote watanzania wenye mapenzi mema na taifa hili na ili kuipata Tanzania tuitakayo kuna vitu tunatakiwa tuvifanye kama taifa kwa kupenda au kwa kutopenda huku tukiweka mbele utaifa wetu na mambo hayo ni kama yatuatayo;

1: Katiba mpya
Kwa kuwa msingi wa taifa lolote ni katiba basi kwa kuwa na sisi Tanzania ni taifa tunatakiwa tuweke au tubadili mwongozo wetu utakaoendana na Tanzania tuitakayo. Hii ni kwa sababu katiba tuliyonayo sasa hivi bila kupepesa macho imejaa dosari nyingi na bila kurekebisha hatuwezi kuipata Tanzania tuitakayo mfano katiba tuliyonayo sasa haijaweka wazi mgawanyo wa kimamlaka kwa mihimili ya serikali na bila kumung’unya maneno mhimili mmoja unaonekana kuwa na nguvu kuliko mingine hivyo kupelekea kuathiri baadhi ya maamuzi ya mihimili mingine.

2. Tume huru ya uchaguzi
Kwa kuwa tume ya uchaguzi ndio msimamizi na mratibu wa chaguzi zote nchini na ambayo inapelekea kupata viongozi watakaoliongoza taifa hili. Bila kufumba macho na ni ukweli usiopingika tume yetu tuliyonayo sasa hivi tunaweza sema haiwezi tufanya tupate Tanania tuitakayo. Nini kifanyike ili kupata tume itakayotupatia viongozi watakao tuongoza kuipata Tanzania tuitakayo
Ni mwenyekiti pamoja na wajumbe wa tume huru ya uchaguzi wapatikane kwa kukubalia kwa vyama vyote vya siasa,makundi ya kiraia na wananchi kwa ujumla hii itaondoa upendeleo kwa wagombea na kupelekea kupata viongozi ambao ni hitaji la wananchi

3. Mfumo huru wa haki jinai
Hii pia ni sababu muhimi itakayotufanya kuipata Tanzania tuitakayo tunatakiwa kuboresha mfumo wa utoaji haki jinai ili kumfanya kila mtanzania kupata haki yake bila kujali tajiri au maskini amesoma au hajasoma kiongozi au sio kiongozi. Na hii inawezekana kwa kufanya marekebisho ndani ya mifumo huu kama vile kubadili namna ya kuwapata watumishi wa vyombo vya haki jinai ambayo wapatikane kwa kuomba na si kuteuliwa, kubadili miongozo na kanuni za mifumo hii ya utoaji haki jinai. Hii itatupatia Tanzania tuitakayo

4. Elimu
Elimu ni kitu muhimu katika ustawi wa taifa lolote duniani. Na sisi Tanzania kama taifa hatuna budi kuangalia elimu yetu na kuifanyia mabadiliko makubwa yatakayoendana na Tanzania tuitakayo na pasipo kufumba macho elimu yetu ilipo sio pazuri maana wasomi wetu makumi kwa maelfu wametumbukia kwenye kundi lisilo na ajira sababu elimu waliyonayo haiendani na soko la ajira.

Wengine wamekuwa watu wa kusifia watawala (machawa) na wengine wameingia kwenye michezo ya bahati nasibu . Nini kifanyike ili kuendana na Tanzania tuitakayo juu ya elimu yetu;

Moja ni kufanya mabadiliko ya kina ya mitaala ya ufundishaji na udahili utakaoendana na soko la ajira
Pili matumizi ya teknolojia ambayo yamejikita kwenye matumizi ya tehama ndio itumike kufundishia ili kuendana na kasi ya teknolojia.

5. Sera bora za kimaendeleo
Sema bora za kimaendeleo piah ni chachu ya kuipata tanzania tuitakayo sababu itakuwa sera ambayo imebeba hatima ya taifa letu na itazingatia makundi yote na uchumi jumuishi na sera nzuri za kikodi

Hitimisho kwa hayo machache tunaweza kuipata Tanzania tuitakayo ndani ya miaka mitano na kuendelea.
Na bila kufanya mabadiliko ya kina juu ya taifa hili hatuwezi pata Tanzania ambayo tunaitaka hivyo itabaki kuwa ndoto tu. Na ili kuyapata kila mmoja wetu awe tayari kuipambania Tanzania tuitakayo.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom