SoC04 Tanzania Tuitakayo ni ile itakayojengwa juu ya misingi ya elimu, kujiamini, na ubunifu

SoC04 Tanzania Tuitakayo ni ile itakayojengwa juu ya misingi ya elimu, kujiamini, na ubunifu

Tanzania Tuitakayo competition threads

Said Shagembe

Member
Joined
Jan 25, 2019
Posts
23
Reaction score
35
Tanzania Tuitakayo ni ile ambayo inajengwa juu ya misingi ya elimu, kujiamini, na ubunifu.
Ni Tanzania ambapo vijana wanatumia elimu yao kama nyenzo ya kuleta mabadiliko chanya, wakihoji na kushiriki kikamilifu katika siasa na maendeleo ya jamii.

Tanzania yenye vijana waonajiamini na walio tayari kusimama kidete kwa yale wanayoamini ni sahihi.
Katika Tanzania ya kesho, tunatarajia kuona maendeleo ya haraka katika sayansi na teknolojia, yakichochewa na vijana walio na kiu ya maarifa na ubunifu. Uchumi wa nchi utakua kwa kasi kwa sababu ya mchango wa vijana hawa, ambao wataleta uvumbuzi na mawazo mapya katika biashara na viwanda.

Viongozi wa Tanzania Tuitakayo ni wale wanaotambua na kuthamini mchango wa vijana. Hawa ni viongozi wanaoondoa vikwazo na kutoa nafasi kwa vijana kufikia uwezo wao kamili. Wanapunguza mzigo wa kodi na urasimu usio na msingi ili kuwapa vijana nafasi ya kushindana kibiashara na kufanikiwa.

Tanzania tunayoitaka ni ile ambayo inaheshimu na kusapoti jitihada za kila mwananchi, hasa vijana, kwa kuwa ndio nguvu kazi ya taifa. Ni Tanzania ambayo inaondoa vizingiti na kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kuchanua katika kila sekta, ikiwa ni pamoja na elimu, biashara, sanaa, na teknolojia. Hii ndio Tanzania tunayoitamani, Tanzania yenye nuru na matumaini kwa kila mmoja.

🙏 Nawasilisha
 
Upvote 2

Hakika, Tanzania tuitakayo.
 
Back
Top Bottom