SoC04 Tanzania tuitakayo ni ile uwiano wa kisiasa na kiuchumi

SoC04 Tanzania tuitakayo ni ile uwiano wa kisiasa na kiuchumi

Tanzania Tuitakayo competition threads

Akili Biyengo

Member
Joined
Aug 17, 2023
Posts
13
Reaction score
10
Napenda kutoa ponzi na shukrani kwa uongozi wa jamiiForums kisha natoa salam kwa watanzania wenznagu pamoja na viongozi wetu,hakika Mungu atuzidishie afya.

Hakika kwa mtazamo wangu.Tanzania tuitakayo ni ile yenye uwiano wa kisiasa na kiuchumi.

Haya ndiyo mambo makuu yatkayobadilisha hali ya nchi yetu kama ifuatavyo;

SIASA
Nchi yetu imetawaliwa na amani sababu ya siasa safi na za utulivu lakini tunachelewa kufika kwenye nchi ya ahadi sababu ya kuwa na chama kimoja tawala ambacho kwa mtazamo wangu kinazorota kiutendaji haswa baada ya uchaguzi hali hii inapelekea nchi yetu kuwa nchi ya barabara ya uchumi wa kati wakati dunia ikifukuzia uchumi wa juu. Hii hali inatokana na kujisahau kwa chama tawala kiutendaji.Watanzania tumekuwa watu wa kulalamika na kulaum hali ambayo inasababishwa na udhaifu wa chama tawala kiutendaji.

Hivyo kwa ushauri wangu tukiwexesha mchakato wa kuwa na kikomo wala cha miaka 10-20 kwa kila chama kuachia kijiti ingesaidia sana kutufikisha katika uchumi wa blue au kungekuwa na uchaguzi wa haki kwamba chama tawala kikishindwa kipishe hii ingetufikisha mbali sana kimaendeleo.

UCHUMI
Kwa upande wa uchumi napendekeza sekta mbalimbali kuweka ubunifu katika maeneo husika kuanzia kuwawezesha wananchi, kukusanya kodi rafiki, mipango mbadala ya maendeleo n.k.

Nitoe mfano wa sekta ya elimu, uvuvi na afya

Katika sekta ya elimu kuwe na mpango mbadala utakaowaandaa wanafunzi kujiajiri (kuwa wabunifu) pindi wanapohitimu bila kujali wanasubiri ajira husika au wamesomea masuala fulani,yaani hapa namanisha lile somo la stadi za kazi lifufuliwe upya, likuzwe na kuendelezwa kuanzia shule za msingi hadi kidato cha sita.Hapa nazungumzia technical school walau kila wilaya.

Sekta ya uvuvi itoe elimu ya uvuvi, faida na hasara za uvuvi haramu, kutengeneza mazingira rafiki kwa wavuvi, kukuza soko la samaki, kugfungua mifuko ya wavuvi hasa ikiwezekana kutoa mikopo kwa wavuvi kama ilivyo kwa sekta za biasara.

Sekta afya nayo iboroshe uwezekano wa kila mtanzania kupata huduma ya afya wakati wowote na mahali popote bila kujali hali ya kipato. Wanzania wengi wanakwama au kupoteza maisha sababu ya kutomudu matibabu.

Sekta ya biashara iwajali wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo. Tukumbuke sekta ya biashara ina kundi kubwa la watanzania lakini wengi hawaridhishwi na misingi iliwekwa katika biashara hii ndiyo inapelekea migogoro ya wafanyabiasara na migomo baridi

Kwa ufupi sekta zote zifanye marekebisho kwa kuzingatia misingi ya uchumi wa kati tuachane na misingi ya nchi maskini ambayo babu zetu waliweka kuringana na hali ya uchumi wa muda huo.
 
Upvote 3
Back
Top Bottom