SoC04 Tanzania tuitakayo ni ile yenye Siasa safi

SoC04 Tanzania tuitakayo ni ile yenye Siasa safi

Tanzania Tuitakayo competition threads

Masanja Kisinza

New Member
Joined
May 5, 2024
Posts
3
Reaction score
4
TANZANIA TUITAKAYO.

Tukumbuke jina Tanzania halikuwepo kabla ya 26/4/1964, lakini ardhi na mipaka yake ilikuwepo. Hivyo pamoja na uumbaji wa Mungu, lakini utashi wa mwanadamu uliweza kuamua namna ya kuitawala Dunia kama ambavyo tulivyo.

Tukirejea historia duniani kote, Mungu hakuumba CHAMA CHA SIASA, na hapa kwetu katika kupigania uhuru, watu waliungana kwa mkutadha wa Chama ili kuwa na lengo na nguvu ya kudai uhuru. Tukirejea historia ya kupig niania Uhuru, kuna watu walilipa gharama ya mateso, kupoteza ajira na hata kifo wakipigania uhuru.

Gharama iliyolipwa ilikuwa dhidi ya kundi dogo lililokuwa na nguvu ya kiutawala (kivita), na kiuchumi. Yaani MKOLONI alikuwa sawa na mchungaji wa ng'ombe 1000 na wasiwe na nguvu ya kumshinda.

Je, tutawashawishije vijana wa taifa hili wanaoonewa kwa misingi ya ubaguzi wa kisiasa, kiuchumi, kidini, kikabila, kielimu.!! Ukweli usiopingika ni kwamba HATA SERIKALI ZA KIKOLONI,

Zilijenga barabara, shule, hospitali, reli, na usafiri wa majini (meli) maana na wao walihitaji hizo huduma wakiwa ugenini, kuliko kuzifuata makwao.
Ziliajiri japo kwa misingi ya kibaguzi
Je, UBAGUZI umeisha katika serikali zetu !

Serikali ya kikoloni ilikataza MTUMISHI WA UMMA KUJISHIGHULISHA NA SIASA, sio kweli maana wapo watumishi wa umma waliofanya siasa zenye kuegemea matakwa ya serikali ya kikoloni na watumishi wa aina hii hawakufukuzwa utumishi wao maana walikuwa salama. Kiongozi kama Mwl. Nyerere aliamua kuacha kazi ya kulipwa Mshahara katika serikali ya kikoloni ili afanye mambo yaliyokuwa kinyume na matakwa ya kikoloni. Je, Mwl. Nyerere aliendelea kuwa salama !

Hoja yangu baada ya utangulizi, tuwaelimishe vijana wa taifa hili kuwa ARDHI TULIYONAYO kwa maana ya nchi yetu;
Tunaihitaji zaidi ardhi tuliyopewa na Mungu kuliko vyama vya siasa tulivyonavyo.
Tunahitaji zaidi utu, udugu na kuheshimiana licha ya utofauti TULIONAO.

Vyama vya siasa tulivyonavyo vinatengenezwa na makundi madogo sana ukilinganisha na idadi ya raia wa nchi hii.

Kila tunaempa mamlaka ya kutuongoza sisi tuliowengi hana Uwezo wa kuwa kinyume na hilo kundi dogo lililoko nyuma yake kutuongoza.

Hilo kundi dogo ndilo linaloamua tupewe au tunyimwe nini, lini na wakati gani (Ilani za Uchaguzi).

Hilo kundi dogo kwa nguvu na mbinu zake lina Uwezo wa kuamua nani alindwe ili aishi na nani anyimwe ulinzi bila kujali ataishi au hataishi kwa sababu tu hakubaliani na hilo kundi dogo.

Ikiwa vyama vilivyotupa Uhuru havipo na sasa tuna vyama vingine basi hatuna sababu ya kuvifia hivyo vyama huenda mjukuu wa mjukuu wako atakuwa Rais wa ardhi hii kupitia kundi dogo (Chama) ambacho hakipo sasa na kitakuwepo wakati huo.

Sio kila mtu anaetafuta ridhaa ya kuwakilisha kundi husika anafaa kuongoza, mfano SIO KILA MGOMBEA WA CCM katika nchi hii lazima ashinde uchaguzi, kila kundi la watu lina kiongozi wao na sio lazima awe wa chama fulani tu, hivyo kuna jamii wana kiongozi wao hata kama akihama kwenda chama kingine au kuwa mgombea binafsi bado watampa ridhaa ya kuwaongoza. Hivyo sio dhambi Jimbo la Arumeru mashariki kuwa chini ya CHAUMA, Geita vijijini chini ya CCM na Kigoma mjini chini ya ACT.

Siasa ni utumishi wa kujitoa, lakini pia SIASA IMEKUWA AJIRA. Hivyo haki za kisiasa zinapominywa, NI KUWANYIMA BAADHI YA VIJANA wasipate ajira (kipato) kupitia fursa za kisiasa kwenye vyama vyao.

Tutafakari hili kwamba inapotokea VIJANA WANAKUWA TAYARI KUPOTEZA MAISHA wakati wa uchaguzi;
Kama ni kwa ajili ya Chama, je kimeonea au kimeonewa hivyo tutambue aliyeonea amekiuka misingi ya utu na udugu, na aliyeonewa hakustahili kupoteza maisha hivyo Sheria imuwajibishe aliyeonea.

Kama ni kwa ajili ya mtu kaonea, je kundi dogo lililoko nyuma ya mtu huyu lina nguvu kiasi gani cha kuwalazimisha watu walio wengi kuongozwa na asiyekidhi matarajio yao na hili kundi dogo litanufaika hadi kizazi cha ngapi kwa watu kupoteza maisha.

Ikiwa WACHACHE WALIOONGOZA WENGI KWA MABAVU NA HILA, tulithubutu kuwaita WAKOLONI pamoja na majina mengi ya kufedhehesha. Ikiwa WAAFRIKA wenzetu watakaofanya yale yale tuliyoyakataa enzi za ukoloni TUWAITEJE !

Balozi wa Uswisi Nchini Tanzania, Didier Chassot akiwa katika Kongamano lililoandiliwa na Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD) Th 7/5/2024 alisema “Demokrasia ni ngumu na yenye utata, siyo njia moja iliyonyooka, ni soko lenye shughuli nyingi la mawazo ambapo sauti tofauti hukutana, maoni yanagongana na makubaliano huunda nguvu ambayo inaweza kusababisha kishindo cha sauti zinazopingana.”

Hii nukuu itaishi sana katika fikra zangu, watawala wengi wa kiafrika wameshindwa KUUNDA NGUVU YENYE KISHINDO CHA SAUTI ZINAZOPINGANA. Taifa hili Watanzania walioko CCM wamekuwa na kiburi, upendeleo na hatimiliki ya KUDHANI wao ni bora zaidi kuliko Watanzania walioko nje ya CCM. Na hili linathibitishwa pia na tabia ya baadhi ya Watanzania wenye nia ovu kutumia magari yaliyobandikwa namba za kughushi na kupeperusha bendera ya Chama kumbe ni gari la uhalifu.

Mfano, watumishi wa umma (waajiriwa) waliokuwa upande serikali ya kikoloni walijiona salama na walipendelewa sana ili waendelee kutumika kwa maslahi yao. Leo hii ni nadra kumkuta mtumishi wa umma, mfanyabiashara mkubwa hata mwanamziki mashuhuri kuwa mwanachama wa Chama cha upinzani na akawa na uhuru sawa na aliyeko Chama tawala licha ya KANUNI ZA UTUMISHI WA UMMA kuruhusu mtumishi wa umma KUJISHUGHULISHA na siasa nje ya mda na eneo la kazi.

Huyu mtawala wa sasa tuliyezaliwa nae pamoja, tukakuwa pamoja, tukasoma pamoja, lakini tukaingia kwenye vyama tofauti vya siasa, yeye akawa mwenye haki kuliko mimi.

Hivyo tunahitaji Tanzania ambayo kila kijana wa nchi hii katika wakati wake wa KUISHI awe HURU katika nyanja zote za kimaendeleo bila kuvunja sheria kwa maendeleo endelevu ya taifa hili. Maana tuliwakataa WAKOLONI kwa mambo makubwa mawili, UBAGUZI na KUMINYA UHURU.

Baba wa taifa, Mwl J.K Nyerere aliwahi kusema kuwa maendeleo ya nchi hii yanahitaji Watu, Siasa safi na Uongozi bora. Tunahitaji utii wa kila mtanzania usitokane na HOFU, WOGA na KUJIPENDEKEZA. Raia mwenye hofu na mwoga hataweza kutumia Uwezo wake kujenga nchi yake, bali atafanya mambo yanayoiwezesha tu familia yake kupata mahitaji ya msingi.

Tunahitaji taifa ambalo kila mtu awe na Uwezo wa kumsikiliza ANAYEMKOSOA kama ambavyo mtu huyo humfurahia ANAYEMSIFIA. NAIPENDA NCHI YANGU TANZANIA.
 
Upvote 4
Back
Top Bottom