SoC04 Tanzania tuitakayo ni kitovu cha sayansi na uvumbuzi barani Afrika

SoC04 Tanzania tuitakayo ni kitovu cha sayansi na uvumbuzi barani Afrika

Tanzania Tuitakayo competition threads

Muza madafu

Member
Joined
May 2, 2024
Posts
8
Reaction score
8
Picha kutoka kwenye mtandao.


Linapokuja suala la sayansi na uvumbuzi tunakubaliana kwamba, ni fursa kubwa na yenye soko kubwa na la uhakika duniani kwote.licha ya Tanzania kutokuwepo kwenye orodha ya nchi zinazoongoza kwa ubunifu na uuzaji wa teknolojia duniani ,lakini Bado nchii hii Ina nafasi ya kuwekeza na kuwa nchi inayofanya vizuri na kuongoza Afrika katika ubunifu na uuzaji wa teknolojia kwenye sekta mbalimbali.
illustration-of-military-base-landscape-landscape-silhouette-of-military-base-gate-military-la-jpg.2979341

Ili kufikia hatua ya kuwa kinara katika teknolojia barani Afrika tunahitaji kuweka mikakati ya kitaifa, mageuzi makubwa ya ki sera na elimu.Pia sekta ZOTE za uzalishaji mali yafaa kufanyiwa mageuzi makubwa ya kuhamasisha ubunifu na uvumbuzi wa teknolojia mpya ili kuongeza ufanisi na kufanya vizuri kimataifa.

Sekta zote za umma na binafsi zinahitaji uwekezaji zaidi,motisha katika suala la matumizi ya teknolojia na uvumbuz. Licha ya ukweli kwamba mchakato huu una gharama kubwa za kifedha, endapo tutawekeza nguvu za kutosha kwa kuwajumuisha wadau wote wa ndani na nje ya nchi na kufanya kuwa ajenda na maono ya kitaifa tutapiga hatua na kufikia mafanikio.

Katika andiko hili nimefafanua ni jinsi gani Tanzania tutaweza kuibuka vinara wa teknolojia ndani na nje ya bara la Afrika kwa miaka michache ijayo.

Sekta ya elimu.
Ili kufikia Tanzania yenye mafanikio ya teknolojia ya juu,hatuna budi kuhakikisha tutawekeza nguvu na rasilimali zote zinazohitajika pamoja na miundombinu katika mfumo wa elimu hapa nchini, kama vile uhamasishwaji wa masomo na mitaala ya sayansi na teknolojia, kuhakikisha upatikanaji wa muunganiko wa mtandao wa mawasiliano na (TEHAMA) nchi nzima ili kurahisisha ufundishaji na matumizi ya vifaa vya kukuza ubunifu kama vile kompyuta katika ngazi zote za elimu nchini.

Hii itasaidia kujenga kizazi kinachojiamini katika uvumbuzi na matumizi ya teknolojia na hii ndio rasilimali muhimu zaidi katika kufikia maono ya Tanzania ambayo ni kitovu Cha Teknolojia barani Afrika.
Kuanzishwa kwa vituo atamizi (executive stations)kwa ajili ya watoto wenye vipaji vya kipekee katika uvumbuzi wa teknolojia ili kuwaandaa kufikia maono yao na ya taifa kiujumla.

Sekta ya kilimo.
Licha ya jitihada zinazowekwa na serikali katika kuhakikisha kilimo kinakua na tija hapa nchini, Bado tunahitaji kufanya mageuzi makubwa zaidi katika sekta hii ikiwa ni pamoja na kuibua teknolojia mpya kwa kudhamini maabara za kilimo , wavumbuzi na wazalishaji wa ndani wa viwatilifu, mbolea na pembejeo ,ikiwa ni pamoja na kuwaongezea thamani wao na bidhaa zao ili kupunguza utegemezi wa teknolojia za kigeni.

View attachment 2979349
Hii itakuza ubunifu na kuibuka kizazi Cha wakulima bora na hata kuuza teknolojia na bidhaa zetu kwa nchi nyingine.

View attachment 2979348
Pia kuongeza nguvu na maarifa ya utoaji wa mafunzo ya matumizi ya teknolojia katika kilimo , hasa katika mitaala ya shule na vyuo mbalimbali hapa nchini. Utungwaji wa sera nzuri za kilimo na teknolojia ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa chombo au taasisi maalumu itakayoshughulikia udhibiti wa viwango vya bidhaa za kilimo nchini ili kuhakikisha viwango Bora vya uzalishaji vitakavyofanya vizuri kimataifa.

Ulinzi na usalama.
Pengine hii ni fursa ambayo mataifa mengi ya Afrika yamechelewa kuitambua. Tanzania inaweza kuwa kitovu cha teknolojia, silaha na vifaa vya ulinzi na usalama na kuibuka kiuchumi ikiwa tutaipigia upatu fursa hii.

cropped-2.png

Kupitia vyombo vya uzalishaji mali vilivyopo ndani ya majeshi yetu kama vile SUMA JKT COMPANY, taifa hili kupitia wataalamu, watu binafsi wenye vipaji na ujuzi linaweza kuanza kuvumbua na kubuni vifaa, na mifumo ya ulinzi na usalama kwa teknolojia mbalimbali.
im-833622.jpeg

hii itasaidia kuimarisha miundombinu ya ulinzi na usalama ndani ya taifa letu na kutengeneza biashara nje ya nchi yetu na hivyo basi kuiandaa Tanzania tuitakayo ambayo ni kitovu cha teknolojia barani Afrika.

Habari na mawasiliano.
Ni wazi kwamba dunia hii ni ya Kidijitali na Kila taifa linahitaji teknolojia ya habari na mawasiliano ili kurahisisha muunganiko wa mtandao na uendeshaji wa shughuli za Kila siku. Umuhumu wa fursa hii ndio unaonishawishi kutazama kwa jicho la kipekee sekta hii kuelekea mchakato wa mageuzi ya kufikia Tanzania tuitakayo.
461145_1_En_2_Fig1_HTML.png


Ni ukweli usiofichika kwamba Afrika Bado Kuna mataifa mengi ambayo Bado hayajapata muunganiko wa teknolojia ya mawasiliano, ikiwa tuta ongeza nguvu na ufadhili na uwekezaji kwenye makampuni ya TEHAMA ya ndani kama vile TTCL, kwa kuongeza na kuimarisha miundombinu yake, kama vile kupata vifaa na mifumo ya kisasa zaidi, tutaweza kukidhi mahitaji ya kitaifa na hata kuwa mkombozi wa mataifa mengine barani Afrika.

Sekta ya Afya
Tanzania tuitakayo ni Tanzania yenye viwango vya juu vya uvumbuzi na matumizi ya teknolojia katika sekta ya Afya. Ikiwa tutalivalia njuga suala la teknolojia na uvumbuzi taifa kwa kuvumbua na kuzalisha madawa yenye viwango vya kimataifa, kama vile kuboresha na kuongezea thamani dawa za asili zinazofanya vizuri katika matibabu, basi taifa hili litakua kinara wa utoaji wa huduma bora za afya barani Afrika na nje ya Afrika.
doctor-touching-modern-virtual-screen-interface-medical-technology_53876-102969.jpg


Ni muhimu kuanzishwa kwa maabara kubwa na za kisasa zitakazo tumika na wavumbuzi wa dawa za asili na mitishamba, kuwekeza katika uboreshaji wa mifumo, sera na sheria zinazosimamia madawa yanayozalishwa ndani ya nchi ili kulinda na kuongeza thamani ya watoa huduma wa ndani ya taifa.
kisscc0-herbal-supplement-alternative-medicine-herbs-656df3208b5418.1550879917017044805707.png

Ni wazi kwamba tunahitaji kuundwa kwa taasisi itakayosimamia uvumbuzi, ubora na kulinda teknolojia za viwanda vya uzalishaji wa madawa na vifaa tiba ndani ya nchi yetu.


Uhifadhi na utunzaji wa mazingira na utalii.
Umuhimu wa uhifadhi wa mazingira na utalii kwa teknolojia za kisasa ni nyenzo muhimu ya kuhakikisha tunafikia Tanzania tuitakayo. Teknolojia yaweza kutumika kuharibu au kutunza mazingira , sisi katika Tanzania tuitakayo tunachagua kuitumia kutunza mazingira kwa kiwango Cha juu na Cha kuigwa mfano, kwa kuwekeza katika kuhamasisha uvumbuzi wa mifumo na teknolojia za uhifadhi na utunzaji wa mazingira yetu pamoja na vivutio vya utalii kwa viwango vya juu zaidi.
wildlife-conservation.jpg

Zipo njia nyingi za kuhakikisha mazingira yanabaki katika hali nzuri na salama lakini Kuna ziada kubwa pale teknolojia inapohusishwa, kwa mfano kuanzishwa kwa miradi ya kimkakati ya uhifadhi wa mazingira kama vile mifumo ya kisasa yenye uwezo wa kubaini na ku ripoti uharibifu kwa njia ya kidijitali, kuongeza n kuwekeza kwenye vifaa vya ufuatiliaji wa hali ya ikolojia kidijitali na upanuzi wa misitu.
1-s2.0-S004896972034701X-ga1.jpg

Pia kuanzishwa taasisi na vyombo vya utafiti wa teknolojia ya uhifadhi na vyuo maalumu vya mazingira.

Mwisho: naambatanisha maoni yangu juu ya falsafa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya R 4, kwa jinsi ambayo itaongeza ari ya mabadiliko katika nyanja zote za kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni.
Wako katika ujenzi wa taifa
B.m.kinabo.
Picha zimepakuliwa kutoka tovuti za iStock, Adobe Stock na APAC.
 

Attachments

  • download.png
    download.png
    4.6 KB · Views: 3
  • kisscc0-herbal-supplement-alternative-medicine-herbs-656df3208b5418.1550879917017044805707.png
    kisscc0-herbal-supplement-alternative-medicine-herbs-656df3208b5418.1550879917017044805707.png
    296.7 KB · Views: 4
  • ldh-web.jpg
    ldh-web.jpg
    209.5 KB · Views: 3
Upvote 3
Pamoja na hayo ni muhimu kuanzishwa kwa vituo atamizi (executive stations)kwa ajili ya watoto wenye vipaji vya kipekee katika uvumbuzi wa teknolojia ili kuwaandaa kufikia maono yao na ya taifa kiujumla.
Dada, ninaunga mkono jambo hili.

Hivi ni kwa nini hata wale matajiri wasiweke ule mtindo wa kuyakuza makampuni madogo 'startup' kwa mtindo wa kutoa mafungu na kupatiwa hisa. Kuna haja ya kuongeza umakini wa soko la fedha nchini.


,ikiwa ni pamoja na kuwaongezea thamani wao na bidhaa zao ili kuondokana na utegemezi wa teknolojia za kigeni.
Sawa sawia.

kisscc0-herbal-supplement-alternative-medicine-herbs-656df3208b5418.1550879917017044805707.png

Ni wazi kwamba tunahitaji kuundwa kwa taasisi itakayosimamia uvumbuzi, ubora na kulinda teknolojia za viwanda vya uzalishaji wa madawa na vifaa tiba ndani ya nchi yetu.
Utafiti na muendelezo wa dawa ni sekta inayohitaji kutiliwa mkazo na watu sahihi. Safari ya kufikia mafanikio hayo. Ahsante
 
Dada, ninaunga mkono jambo hili.

Hivi ni kwa nini hata wale matajiri wasiweke ule mtindo wa kuyakuza makampuni madogo 'startup' kwa mtindo wa kutoa mafungu na kupatiwa hisa. Kuna haja ya kuongeza umakini wa soko la fedha nchini.
Mawazo Yako ni mazuri sana pia 👏👏👏👏
Naomba unipigie kura tusonge mbele pamoja
 
Dada, ninaunga mkono jambo hili.

Hivi ni kwa nini hata wale matajiri wasiweke ule mtindo wa kuyakuza makampuni madogo 'startup' kwa mtindo wa kutoa mafungu na kupatiwa hisa. Kuna haja ya kuongeza umakini wa soko la fedha nchini.



Sawa sawia.


Utafiti na muendelezo wa dawa ni sekta inayohitaji kutiliwa mkazo na watu sahihi. Safari ya kufikia mafanikio hayo. Ahsante
100% 👏👏👏
 
Back
Top Bottom