SoC04 Tanzania tuitakayo ni lazima kwanza itoke kwenye mifumo tegemezi ambayo bado inatufanya tuwe watumwa kifedha na kifikra

SoC04 Tanzania tuitakayo ni lazima kwanza itoke kwenye mifumo tegemezi ambayo bado inatufanya tuwe watumwa kifedha na kifikra

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
Jun 4, 2024
Posts
6
Reaction score
1
1. Tanzania Tuitakayo Ni Lazima Kwanza Itoke Kwenye Mifumo Tegemezi Ambayo Bado Inatufanya Tuwe Watumwa Kifedha, Kifikira Na Mpaka Kutufanya Kuwa Wabinafsi;

Mfano; Mambo Ya Kukopa Fedha Kwenye Benki Ya Dunia Na Nchi Zilizoendelea Ambayo Mikopo Yenyewe Haina Afya Katika Maendeleo Ya Taifa Na Watu Wake Kwa Ujumla Maana Inakuwa Na Riba Kubwa Na Hata Hao Wanaotukopesha Hawawezi Kutupa Masharti Nafuu Lazima Ni Yale Ambayo Yatawafaidisha Wao Mikopo Inarudisha Nyuma Maendeleo Lazima Tujitegemee Wenyewe.

2. Serikali Husika Inabidi Iache Kutegemea Teknolojia Kutoka Nchi Zilizoendelea Inabidi Iwekeze Katika Vijana Wake Wenye Uwezo Wa Kuvumbua Na Kuendeleza Vitu Mbalimbali, Zifunguliwe Shule, Taasisi Na Vyuo Mbalimbali Ambazo Zitatumika Kuwafua Vijana Mbalimbali Ambao Sasa Ujuzi wao Utatumika Ndani Ya Nchi Hivyo Itapunguza Gharama Na Madeni Wanazozitumia Huko Nje Na Hata Mzunguko wa Ndani Wa Fedha Utakuwa Mkubwa Na Hata Serikali Haitakuwa Tegemezi Kwa Nchi Za Magharibi na Asia, Maana Tukiwa na Teknolojia Bora Na Ya Kisasa Tutatengeneza Bidhaa Bora Ambazo Zitasaidia kupunguza Kuingiza Bidhaa Kutoka Nje Kwahiyo Soko La Bidhaa Za Ndani Pia Hizo Bidhaa zitakuwa Salama Kwa Afya Za Watanzania Kuliko Hizo Zitokazo Nje Zisizo Salama Zilizogubikwa na Magonjwa Ya Kisasa Kama Saratani, Kisukari , Shinikizo La Damu Nk. Hivyo Hata Bidhaa Zetu Litafanya Soko La Ndani Kuwa Kubwa Na Pato La Nchi Litakuwa Kubwa Pia, Tutaweza Kutengeneza Barabara Zetu Wenyewe Na Miundo mbinu Mbalimbali Hivyo Uingizwaji Wa Watalaamu Kutoka Nje Na Pamoja Na Teknolojia Yao Utapungua Na Utapunguza Matumizi Ya Fedha Na Kupanua Soko La Ajira Kwa Wazawa Na Kupunguza Ukosefu Wa Ajira.

3. Uzalendo Ndo Chachu Kubwa Ya Maendeleo, Maana Hii Nchi Inarudi Nyuma Leo Kwasababu Walio Na Dhamana Siyo wazalendo Hawafuati Sheria Ila Sheria Inawafuata Wao, Wengi Hutumia Dhamana Ya Madaraka Walionayo Kujinufaisha Wao Na Si Taifa Kwa Ujumla Lakini Uzalendo Ukiwa Mbele Taifa Litapata Maendeleo Makubwa Sana Rasimali Zilizopo Zisiwe Kwaajili Ya Viongozi na Watumishi Bali Zinufaishe Taifa Kwa Ujumla Kwa Mfano Sekta Ya Madini Pekee Ikisimamiwa Bila Ubinafsi Inaweza Ikatupa Barabara Safi, Viwanja Safi Vya Ndege , Umeme Usio Wa Mashaka , Maji Safi Na Salama Lakini Pia Hospitali, Madini Inabidi Yachakatwe Hapa Hapa Ndani Na Liwepo Soko La Kimataifa Ambalo Litawafanya Wuzaji kuuza Kwa Bei Nzuri Kuliko Kwenda Kuyauza Dubai Na Kwingineko Hiyo Itakuza Mzunguko Wa Fedha Ndani Ya Nchi Na Kupunguza Uchumi Tegemezi.

4. Tanzania Tuitakayo Ni Ile Ambayo Wimbi La Matumizi Ya Uraibu Mbalimbali (Madawa Ya Kulevya) Unadhibitiwa Maana Hii Pia Ni Chanzo Cha Taifa Kurudi Nyuma Uingizwaji Wa Madawa Ya Kulevya Unapunguza Nguvu Kazi Ya Taifa Hivyo Taifa Linapoteza Watu Wenye Afya Ya Akili Na Mwili Lakini Pia Upotevu Wa Maadili Na Wengine Kufa Kabla Ya Nyakati Zao Hivyo Madawa Ya Kulevya Yadhibitiwe Balabala Itasaidia Kupata Vijana Wenye Akili Timamu Na Nguvu Hivyo Itasaidia Kuendeleza Rasimali Mbalimbali Na Vipaji Vyao Vitasaidia Kuwa Chachu Ya Maendeleo Taifa Halitakosa Rasimali Watu Na Litapunguza Wimbi La Kuingiza Watalaamu Kutoka Nje.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom