SoC04 Tanzania tuitakayo sekta ya Elimu

SoC04 Tanzania tuitakayo sekta ya Elimu

Tanzania Tuitakayo competition threads

Massawe John

New Member
Joined
Jun 13, 2024
Posts
2
Reaction score
1
TANZANIA TUITAKAYO

# SEKTA YA ELIMU
Kwanini andiko hili limeegemea zaidi katika sekta ya elimu? Jibu ni hili katika maeneo muhimu na nyeti ambayo yakichezewa basi taifa laweza kupoteza dira na mwelekeo ni eneo hili la elimu hivyo kama tutakua makini katika eneo hili tunaweza kuitengeneza Tanzania bora na imara ya sasa na hata siku za baadae,Elimu hii ndio inayozalisha Viongozi,Madactari,walimu na hata Mainjinia kama tutaichezea si kuharibu mfumo wa taifa letu? Nini basi kifanyike kuhakikisha tunakua na mfumo bora wa elimu nchini ambao utaenda kua jibu la changamoto zilizopo sasa hasa katika sekta ya elimu na baadae katika sekta nyingine? Haya ni mawazo yangu yatakayoenda kutoa majibu;

Maboresho ya mitaala kuhakikisha inafanana na mazingira halisi ya Tanzania;kwa kiasi kikubwa mtaala/mitaala inayotumika nchini kwa sasa kuanzia ngazi ya elimu ya chini kabisa yaani msingi mpaka ngazi ya vyuo vikuu haiendani na mazingira halisi ya kitanzania mfano hili somo la Historia ambalo kwa kiasi kikubwa mada zake zinazungumzia historia za tawala za mataifa ya Ulaya,Asia na Marekani hii inaonesha ni kwakiasi gani mitaala inayotumika katika mashule yetu nchini kwa sasa haina uhalisia wa mazingira yanayomzunguka mwanafunzi,hivyo ni ngumu kuwapa wanafunzi juzi ambazo zitakwenda kuwasaidia sao na hata jamii,niwakati wa kupitia mitaala hii na kuifungamanisha na mazingira halisi ya Tanzania.

Maboresho ya miundombinu;hili ni moja ya eneo ambalo limeonekana kua na udhaifu mkubwa idadi ya madarasa pamoja na ubora ni wa hali ya chini kabisa vipi tutaweza kuzalisha wataalamu na wanafunzi bora.Shule nyingi hasa za sekondari nchini hazina miundombinu ya kutosha yaani vyumba vya madarasa vya kutosha pamoja na madawati na kwa baadhi ya shule ambazo zinavyo bado miundombinu hiyo haina ubora mfano mifumo ya umeme,pamoja na sakafu imara mara kadhaa haya yameripotiwa kupitia vyombo vya habari nchini,hivyo ni wakati sasa serikali ikahakikisha ujenzi wa miundombinu ya kutosha na bora ili kuwapatia wanafunzi mazingira bora ya kujisomea.

Kuhakikisha ubora wa waalimu na wakutosha;eneo lingine lenye changamoto kubwa katika sekta ya elimu nchini ni upungufu wa waalimu mashuleni licha ya idadi kubwa ya waalimu wanaohitimu kila mwaka kutoka vyuo mbalimbalo hapa nchini.Upungufu huu wa waalimu unasababisha baadhi ya waalimu kubeba mzigo mkubwa kuliko uwezo wao wa kawaida Mfano ni katika shule moja ya Sekondari iliyopo wilaya ya Moshi vijijini ambayo ina mwalimu mmoja tu anayefundish masomo ya Biashara na Uchumi unaweza kufikiri anataabikaje kuhakikisha anawafundisha wanafunzi wote hao kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne.Katika eneo hilihili tunapaswa pia kuchunguza ubora wa waalimu kabla hatuja waajiri kwani ni jambo la kawaida sana hasa katika shule za serikali kukuta mwalimu wa Kingereza hajui ata lugha yenyewe hivyo ni vyema kupima ubora wa walimu hawa kabla ya kuwaajiri.

Usimamizi na ukaguzi wa mara kwa mara kubaini ikiwa waalimu wanafanyakazi sawasawa na mitaala inavyoelekeza;Baadhi ya waalimu wamebaki kua walevi Jambo ambalo linahatarisha maendeleo ya wanafunzi mashuleni,ikiwa mwalimu ni mlevi unaweza kujiuliza kama ataweza kufundisha sawa na mtaala unavyomhitaji kufanya,na je ataweza kuhudhuria vipindi vyote anavyopaswa kuhudhuria? Kama umepita shuleni bilashaka umekutana na walimu wa namna hii si vyema kuwataja pamoja na shule zao lakini ni wakati sasa serikali ilaweka mkakati wa kaguzi za mara kwa mara na za kushtukiza ili kuhakikisha walimu wazembe wanaondolewa na kuletwa wengine ambao watakua na uwezo na nidhamu ya kazi hii itasaidia kuzalisha wataalamu na wahitimu wenye ubora na juzi muhimu.

Kuhimiza na kufundisha kwa masomo ya vitendo;
Ukipita katika mashule mengi nchini utagundua kua mafunzo mengi yanayotolewa madarasani ni ya nadharia na asilimia chache sana kwa vitendo,wakati mwingine ata yale ya vitendo yasiwe na msaada wowote kwa mwanafunzi,Mmfano mzuri ni ile mada ya "Food test" katika somo la sayansi kidato cha pili na cha tatu inayohusisha utambuzi wa aina ya kundi la chakula katika chakula fulani swali nikwamba mara baada ya majaribio haya yanayofanyika katika maabara hizi mwanafunzi anapohitimu anakwendaje kutumia katika mahisha ya kila siku?Nini kifanyike wizara ya elimu Ina nafasi ya kupitia mitaala na mada au masomo ya vitendo yanayotolewa mashuleni kuhakikisha yatakwenda kutatu changamoto zikabili maisha ya mtanzania ya kila siku.

Kuimarisha na kuongeza idadi ya vyuo vya ufundi nchini;hili ni moja ya eneo ambalo halijapewa kipaumbele kama inavyotakikana,idadi ya vyuo vya ufundi nchini ni ndogo kulinganisha na idadi hitajika ata hivyo haijawekwa sera mahususi itakayotumika kusimamia vyuo hivi.Ikiwa serikali itawekeza nguvu katika eneo hili kwa kiasi kikubwa itakwenda kutatua au kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira inayolikabili taifa kwa sasa kwani ni sehemu pekee ambayo inatoa elimu na juzi ambazo moja kwa moja zinakwenda kutumika katika jamii mfano Ufundi umeme,makenika na ufundi Nguo.

Kusisitiza au kuanzisha elimu shirikishi baina ya mwalimu na mwanafunzi;Mfumo wa elimu wa sasa ni ule wa upande mmoja tuu yaani mwanafunzi kutegemea kila kitu kutoka kwa mwalimu badala ya kubadilishana,Kama serekali na wizara yenye dhamana ya elimu itaweka taratibu ambazo zitaruhusu pamde hizi mbili kufanya kazi kwa kushirikiana basi bila shaka tutaweza kuzalisha au kutoa wahitimu wenye juzi,uwezo mkubwa na wanaoweza kufikiri sawasawa

Kuhimiza Matumizi ya lugha ya kiingereza katika mfumo wa elimu nchini;lugha ya Kingereza imeendelea kua nyenzo kubwa ya mawasiliano katika ngazi ya kimataifa kote ulimwenguni,licha ya lugha hii kuonekana kua na faida kemkem hasa katika jukwaa la biashara za kimataifa lakini bado jitihada zinazowekwa katika ngazi za elimu nchini ni ndogo ulikinganisha na namna inavyopaswa,kwani ni imekua kawaida kumkuta mwanafunzi wa chuo kikuu nchini akishindwa kujieleza kwa kutumia lugha ya kingereza kuanzia ngazi ya msingi mpaka chuo kikuu,hii inachangiwa na kukosekana kwa vitabu vya kutosha vya masomo ya kingereza,walimu wenye juzi za kutosha juu ya lugha hii na mbinu thabiti za ufundishaji wa somo husika hivyo kama maeneo haya yatafanyiwa marekebisho mazuri ni imani yangu kua tutakwenda kuibadili kabisa hali iliyopo kwa sasa na kuinua uelewa wa wanafunzi mashuleni katika somo hili.
Hivyo ni imani yangu kua kama niliyoandika yataenda kuzingatiwa tutegemee mabadiliko yenye tija haswa katika mfumo wetu wa elimu na unaenda kua msaada mkubwa katika utatuzi wa changamoto zetu kama taifa.
 
Upvote 5
Back
Top Bottom