SoC04 Tanzania tuitakayo: Serikali iwekeze kwenye ujenzi wa vyuo vya ufundi kupunguza tatizo la ajira kwa vijana

SoC04 Tanzania tuitakayo: Serikali iwekeze kwenye ujenzi wa vyuo vya ufundi kupunguza tatizo la ajira kwa vijana

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
May 5, 2024
Posts
21
Reaction score
10
UTANGULIZI
Mimi ni miongoni mwa vijana wa kitanzania ambao ni wahanga wa ajira za serikali baada ya kuhitimu elimu yangu ya juu na ni takriban miaka minne sasa niko mtaani ninatrust process lakini kama ningeendelea kusubiri mfumo pengine leo ningekuwa maskini wa kutupwa kiasi cha kushindwa kupata angalau hata milo miwili kwa siku na vocha ya shilingi 1000 ili nimjulie mamayangu hali huko kijijini.

Lakini ndugu msomaji nataka ujifunze kitu hapa kwa lengo la kuokoa maelfu ya vijana wa kitanzania kuondokana na fikra duni, ndugu msomaji mimi leo kipato changu kwa siku siyo chini ya 20,000 kwani nafanya kazi ya ufundi vigae (tiles) hiyo 20,000 nliyoitaja ni malipo ya day kwa mafundi wenzagu lakini ikitokea nimeshika kazi mimi mwenyewe nyumba ya room 4 self siyo chini ya laki nane Hadi 1 million na ni kazi itakayofanyika ndani ya wiki mmoja ndugu msomaji.

Lengo la kuwapa huo ushuhuda nataka kila mtu ajifunze kitu na achukue hatua, zipo fani nyingi za ufundi zenye hela nyingi sana lakini mchango wa serikali yangu tukufu unahitajika kuwaletea vijana hawa huduma ya mafunzo ya karibu kwa kuwajengea vyuo vya ufundi angalau kila wilaya chuo kimoja kisha kuwafundisha fani zifuatazo ambazo zitawapa faida ya mmoja kwa mmoja vijana.

UFUNDI UASHI (BRICK&BRICKLAYING)
Hii ni fani ambayo itawafaidisha vijana kwani kila kukicha mijini na vijijini watu wanajenga na wataendelea kujenga, vituo vya afya vinajengwa, shule zinajengwa na ajira nyingi zitapatikana kwa vijana na kipato cha kutosha kwani kujenga tofali mmoja la block ni 300 sasa imagine nyumba hadi inakamilika matofali mangapi yamejengwa then zidisha kwa idadi ya mafundi na wasaidizi wao tumekwamua vijana wangapi kiuchumi.

UFUNDI PAA
Baada ya kusimamisha ukuta kifuatacho ni upauzi, kazi ya kupaua nyuma ya vyuma 4 self contained haichukui zaidi ya wiki mmoja lakini malipo yake ni makubwa sana ndugu msomaji, tokeni magetoni vijana muache kubeti na kukaa vijiweni bila tija yeyote,

UFUNDI UMEME(ELECTRICAL INSTALLATION)
Je' umeshamwona fundi umeme yeyote ambaye ana maisha magumu, Jiulize mwenyewe kama hujawahi kuwona fanya utafiti kisha umfananishe na mhitimu wa fani ya ualimu pale mkwawa au SAUT na yupo mtaani kwa miaka mitano, sijasema ualimu ni mbaya la hasha bali tuangalie fursa zinazotuzunguka pia Ili kuondokana na umaskini wa kipato cha ajabu zaidi fani ya ufundi umeme unaipata kwa miezi mitatu tu na ada yake ni 300,000 tu kwa baadhi ya vyuo vya ufundi yaani unaweza ukawa na bachelor yako safi ya ualimu na ukaendelea kupiga mishe za umeme ukapiga hela nyingi kama mimi halafu siyo mchoyo wa kuwashirikisha fursa utaniambia nini ila naishukuru pia JF kwa kuweka jukwaa hili Ili kusaidia kujenga Tanzania tuipendayo.

UFUNDI MABOMBA(PLUMBING & PIPE FITTING)
Moja ya fani ambayo ni applicable maeneo ya mijini na vijijini ni hii, fani ambayo haina mipaka na pana sana kwani kwenye ujenzi wa majumba lazima yafungwe mabomba chooni na bafuni lakini pia mabomba ya kumwaga maji ya mvua pia mabomba ya maji ya RUWASA na wale wa mijini pia huko vijana watajipatia ajira za mmoja kwa mmoja na kuondokana na umaskini.

UFUNDI VIGAE(TILES)
Moja ya kazi ambayo inaelekea kunitajirisha ni ufundi tiles yaani inaelekea kunitajirisha kabla hata sijaingia kwenye mfumo wa serikali na bado niko below 30 lakini nataka kuwakomboa vijana wenzagu Ili kujenga uchumi imara wa nchi yetu kwa sababu kuinua uchumi wa nchi inategemeana pia na uchumi wa wananchi wake nchi haiwezi ikawa developed halafu watu wake ni maskini, ndugu msomaji anza kuchukua hatua za kimkakati leo maana mwenye jukumu la maisha Yako na wewe wala siyo mzazi wako au ndugu yako flani, anza kufanya mazoezi tafuta watu wanaojua unachotaka kujua kisha utafanikiwa.

UFUNDI SEREMALA(CARPENTRY)
Ufundi useremala ni ufundi wa kutengeneza thamani zote zinazihusiana na mbao kama vile vitanda, meza , makochi n.k.

Ndugu msomaji watu lazima walale kwenye vitanda na lazima wawe na meza tena hata vile vitanda vilivyotengenezwa kwa mda mrefu huharibika na lazima watu warudi sokoni kwa fundi kisha kutengeneza vingine hivyo hoja yangu ya msingi hapo ni kwamba demand ipo ya uhakika na ni wewe tu kuanzia kutengeneza pesa taratibu na kisha kuondokana na umaskini wa kipato, hamna siku ambayo nimepita karibu na carpenters halafu nikakuta hana order maana yake ni kwamba uhakika upo wa kazi.

HITIMISHO
Wito wangu kwa serikali yangu sikivu chini ya mama yetu mpendwa Ili tuwe na Tanzania tuitakayo haina budi kuwekeza katika vyuo vya ufundi ijenge angalau chuo kimoja kwa kila wilaya ni ngumu lakini mikakati ikiwekwa baada ya miaka 10 inawezekana maana hayo yote niliyoyaeleza hapo juu haviwezi kufanikiwa bila msaada wa mmoja kwa mmoja wa serikali.

Wito wangu pia kwa vijana watoke magetoni acheni kubeti tuchape kazi maana hatuwezi kujenga Tanzania tuitakayo bila kujitolea kwa asilimia zote na kuanza kujifunzia fani ndogondogo zenye tija mtaani badala ya kutegemea ajira za serikali na mwishowe kuwa na idadi ya vijana wasomi lakini maskini.

Naishukuru pia Jamiiforum kwa kuleta wazo hili la stories of changes kwani kupitia hili jukwaa naamini watu wengi saana watajifunza vitu vingi na tofautitofauti lakini pia imetupa fursa za kutoka maoni yetu kwa lengo la kujifunzia pamoja na kuelimishana baadhi ya mambo. Ahsanteni.

MWISHO.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom