Robo karne ijayo Tanzania itakuwa katika nafasi bora ya kiuchumi hili ni jambo la kutia moyo.
Hakuna jambo jema likosalo changamoto zake, changamoto kubwa wa ukuaji wa uchumi ni ongezeko la watu wenye maradhi yasioambukiza na ongezeko kubwa la vifo vinavyotokana na maradhi yasioambukiza NCDs katika nchi zilizoendelea kiuchumi hapa duniani kwa sasa.
Maradhi yasioambukiza ni kama
Maradhi ya moyo,
Saratani,
Sindikizo la damu
maradhi ya figo
sukari n.k.
Ongezeko hili linatokana na sababu kuu mbili;-
Picha fuatanyo inalinganisha sababu 10 zinazoongoza za vifo katika ukanda wa Afrika na ukanda wa Marekani.
Picha hiyo inatuonesha, kabla ya mripuko wa ugonjwa wa korona mwishoni mwa mwaka 2019 maradhi yasioambukiza yanaongoza katika kusababisha vifo vingi katika nchi zilizoendelea, kama ulaya na marekani. Na nchi zibazoendelea kama ukanda wa Africa Sababu kuu za vifo ni maradhi ya maambukizi kama vile Pneumonia, malaria, kifua kikuu n.k
Figure 1.8 Courtesy of WHO World Health Statistics 2024.
Data za sababu 10 zinazoongoza kusababisha vifo Tanzania mwaka 2019, zinaonesha Tanzania kama nchi yenye uchumi wa chini kati ( lower middle income) bado tunasumbuliwa zaidi na maradhi ya kuambukiza.
Image Courtesy ;WHO Data United Republic of Tanzania.
Hivyo basi.
Nini Tanzania inapaswa kufanya ili kudhibiti
Ongezeko la maradhi yasioambukiza.
Kupunguza vifo vya mapema vya NCDs.
Muhimu zaidi kulinda wananchi wake wasiwe katika hatari ya kupata NCDs.
Kinga bora, ugunduzi wa mapema wa maradhi na matibabu bora ndio silaha kuu.
Mapendekezo.
KINGA
UGUNDUZI WA MARADHI MAPEMA NA MATIBABU BORA ILI KUPUNGUZA VIPO VYA MAPEMA VYA NCDs
Kuongezwa kwa matumizi ya serikali katika huduma za afya mpaka angalau asilimia 20% kwa pato la ndani la taifa hadi 2030.
Naamini ni kitu kinachowezekana na naona tunaelekea huko kila budget inayotoka ya afya inatupa moyo tukijiwekea malengo thabiti kwa hakika tutafika.
Matumizi makubwa ya nchi yetu yaelekezwa katika huduma ya afya hasa katika eneo la kinga.
Kuondoshwa kabisa kwa kodi katika usafirishaji wa matunda na mboga mboga ndani ya Tanzania.
Zanzibar ni moja ya sehemu kula matunda inaonekana kama hanasa kwa sababu ya bei za matunda na ugumu wa upatikanaji wake.
hivyo kuondoshwa kwa kodi za usafirishaji wa matunda/ mboga mboga utawezesha kila mtanzania kumudu.
Wakati Tanzania tukipambana kupunguza vifo vitokananvyo na maradhi ya maambukizi na changamoto za uzazi na watoto chini ya umri wa miaka mitano. Tusisahau kuweka mikakati sahihi ya kukabiliana na ongezeko la maradhi yasioambukiza na tuanze sasa.
Naamini katika hizi hatua za kuwaelimisha watu kwenye mitandao au njia za kampeni tofauti tofauti za taasisi tofauti zinaleta tija kwa kiwango fulani ila naamini mabadiliko chanya na ya muda mrefu tuanze kwa kubadilisha mfumo mzima wa elimu yetu na mipango yetu kama taifa.
Tanzania ninayoitaka miaka 25 ijaya ni yenye kiwango kidogo cha maradhi yasioambukiza pia na kwa walionayo wapate matibabu bora ili visitokee vifo vya mapema kutokana na maradhi hayo..
Mungu ibariki nchi hii nzuri TANZANIA.

- Uchumi unapokuwa mzuri na raia kuishi Maisha bora yenye huduma bora za kijamii, tunashuhudia udhibiti mkubwa wa vifo vitokanavyo na maradhi ya kuambukiza na hivyo kuwa katika kiwango cha chini, maradhi ya kuambukiza kama vile maradhi ya Malaria, Ukimwi, Kifua Kikuu n.k.
- Kubadilika kwa mtindo wa Maisha, hivyo watu wengi kuchukua mtindo mpya hasi zidi wa afya zetu, kama vile watu kutumia vyakula vya wiwandani zaidi, kukaa muda mrefu bila kushughulisha mwili, kutojumuika na wana jamii wengine muda mwingi tupo na Simu na Runinga.
Picha fuatanyo inalinganisha sababu 10 zinazoongoza za vifo katika ukanda wa Afrika na ukanda wa Marekani.
Picha hiyo inatuonesha, kabla ya mripuko wa ugonjwa wa korona mwishoni mwa mwaka 2019 maradhi yasioambukiza yanaongoza katika kusababisha vifo vingi katika nchi zilizoendelea, kama ulaya na marekani. Na nchi zibazoendelea kama ukanda wa Africa Sababu kuu za vifo ni maradhi ya maambukizi kama vile Pneumonia, malaria, kifua kikuu n.k
Figure 1.8 Courtesy of WHO World Health Statistics 2024.
Data za sababu 10 zinazoongoza kusababisha vifo Tanzania mwaka 2019, zinaonesha Tanzania kama nchi yenye uchumi wa chini kati ( lower middle income) bado tunasumbuliwa zaidi na maradhi ya kuambukiza.
Image Courtesy ;WHO Data United Republic of Tanzania.
Hivyo basi.
Nini Tanzania inapaswa kufanya ili kudhibiti
Ongezeko la maradhi yasioambukiza.
Kupunguza vifo vya mapema vya NCDs.
Muhimu zaidi kulinda wananchi wake wasiwe katika hatari ya kupata NCDs.
Kinga bora, ugunduzi wa mapema wa maradhi na matibabu bora ndio silaha kuu.
Mapendekezo.
KINGA
- Kuanzishwa kwa somo linaloitwa NCD’s and Lifestyle : Somo hili liwe litakalosomeshwa kuanzia elimu ya msingi mpaka secondary. Somo litakuwa linafundisha juu ya ulaji bora na umuhimu wa mtindo bora wa Maisha. Pia watajifunza jinsi ya kufanya vipimo vya nyumbani kama vile upimaji ya presha, sukari, waist hip ratio (WHR) body mass index (BMI) n.k. Angalau 50% ya watanzania ifikapo mwaka 2050 wawe na uwezo wa kupima hivi vipimo muhimu akiwa nyumbani na kuweza kuwa makini na muenendo wa afya yake.
- Upimaji huu wa nyumbani ni muhimu sana katika kugundua maradhi yasioambukizwa kwa wakati sahihi pia katika matibabu yake kwa ufanisi mkubwa.
- Ufaulu mzuri wa somo hili liwe ni moja la somo la kipaumbele ili mwanafunzi kupata Daraja la juu na hata udhamini wa masomo. Hivyo itafanya Tanzania iwe nchi ambayo mhandisi, daktari, mwalimu na hata muuza duka nyumbani awe ni nutritionist mzuri.
- Kuanzishwa kwa vituo vya mazoezi vya serikali (Community sports center) na kwa idadi inayoendana na shule za sekondari nchini. Wakufunzi wawe waajiriwa rasmi wa serikali. Kuwe na vituo tofauti vya wanawake na wanaume vyenye umbali usiyopungua mita 500- 1000 na wakufunzi wawe wa jinsia hiyo hiyo, hili litawezesha ushiriki bora wa watu wa jamii zote.
- Hili litaichukua Tanzania miaka 10- 20 kulitimiza.
UGUNDUZI WA MARADHI MAPEMA NA MATIBABU BORA ILI KUPUNGUZA VIPO VYA MAPEMA VYA NCDs
- Kuajiriwa kwa watoa huduma wa kutosha kuendana na pendekezo la WHO. Physician density ( idadi ya madaktari katika kila idadi ya watu elfu 10). Kwa dunia nzima kwa sasa ni densiti ya madaktari kwa kila watu elfu 10 ni 17.7 Ila density ya madaktari kwa kila watu elfu 10 Tanzaia ni 1.3. ( Source world bank group data na WHO data) Na hapo si madaktari tu, bali hata nurses and midwives, wafamasia pia tuna upungufu mkubwa .
- Pendekezo la kufikia angalau daktari mmoja kwa kila watu 1000, linaweza kufikliwa mwaka 2050. Hivyo kila budget ya mwaka ya wizara ya afya ijiwekee idadi ifaayo ya watumishi wa afya wapya ili kufika 2050 tuwe tumefikia lengo la 1:1000.
- Mwaka 2050 tunatarajiwa kuwa na idadi ya watu Milioni 129 (WHO data United Republic of Tanzania) hivyo mipango yetu ya idadi ya watoa huduma iaendane na ukuaji wa idadi ya watu unaokuwa kwa kasi,
- Marekani kwa sasa katika kila watu 1000 kuna daktari 2.6 na huku Italy wakiwa mbele zaidi ya madaktari wanne katika kila watu 1000.
- Kama ilivyoripotiwa na gazeti la THE CITIZEN tolea la 20/08/2022 ikawa na kichwa cha Habari “Doctor fatigue a rising concern in Tanzania’s hospitals”. Hakika ni kweli Daktari waliochoka hawatoweza kuwahudumia wanachi kwa uhodari mkubwa.
- Watoa huduma za afya wa TAMISEMI walipwe mshahara na mururupu sawa au zaidi ya madaktari wa waliopo chini ya wizara ya afya.
- Bima iwe na fungu maalumu la angalau mwaka mara moja mteja wao kufanya vipimo vya afya(Medical checkup).

Upvote
1