SoC04 Tanzania Tuitakayo: Tatizo la ajira lifike kikomo

SoC04 Tanzania Tuitakayo: Tatizo la ajira lifike kikomo

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
Jun 21, 2024
Posts
7
Reaction score
13
Nawasalimu kwa jina la jamhuri. Kama lilivyo tamu kulitamka jina la nchi yangu Tanzania ndivyo ninavyotamani kuona mabadiliko ya kijamii na kichumi kwa ujumla viwe na ladha hiyo ya utamu. Kumekuwa na wimbi kubwa la vijana wasomi wasio na ajira tangu mwaka 2015 hii Kutokana na sera na mabadiliko ya viongozi wa kisiasa wanaoingia madarakani. Vijana wanaohitimu elimu ya juu ni wengi ukilinganisha na kiwango Cha serikali kuajiri na hivyo kusababisha uwepo wa wimbi kubwa la vijana wasio na ajira.

Kwa mujibu ya ripoti ya Taasisi ya Utafiti na kupunguza Umaskini Tanzania (NEPOA) ya mwaka 2019 takribani vijana 1,000,000 wanahitimu kila mwaka kutoka Taasisi mbalimbali za kielimu huku idadi ya ajira zinazozalishwa kutoka serikalini na sekta binafsi ni 250,000 kwa wastani kila muhitimu anatumia miaka 5.5 kupata ajira .(chanzo BBC news Swahili 11 June 2023)

"Waziri wa TAMISEMI Anjelina kairuki alipozungumza na vyombo vya habari alieleza kuwa waomba ajira 419 walidanganya kuwa walemavu kati ya waombaji 171,916 katika ya ualimu na afya.katika kada hizo mbili waliopata ajira ualimu 13,130 na afya 5319 jumla 18,449 na walioachwa kwa sababu mbalimbali ni 153,512" (Chanzo:BBC NEWS 11 June 2023).

Kulingana na mchanganuo huo hapo juu tunaona kwa upana zaidi tatizo la AJIRA linavyoathiri TAIFA letu haswaa kwa vijana. Serikali inashindwa kumudu suala la ajira kwa sababu.

1. Vyuo kudahili wanafunzi wengi kuliko uhitaji wa ajira katka kozi mbali mbali . Kwa Sasa nchi yetu Ina vyuo vingi vya elimu juu na vya kati hivyo kila mwaka kuzalisha wahitimu wengi kuliko uhitaji. Mfano vyuo vya elimu ya juu vikiwemo UDSM na matawi yake MUCE na DUCE, UDOM, MZUMBE, SAUT, TEKU na vinginevyo vile vya kati vinatoa kozi ya ualimu wa Sanaa na sayansi. Kwa upande wa serikali wao uhitaji wao mkubwa na waalimu wa sayansi hapo tunaona jinsi gani wahitimu wengi wanazalishwa bila kuendana na mahitaji.

2. Serikali Bado haijaweka mazingira mazuri kwa wajasiriamali, vijana wengi waliokosa ajira wanajikuta wanaangukia katika ujasiriamali ili kuweza kumudu mahitaji yao ya msingi lakini serikali inaweka Sheria kandamizi kwa vijana hawa. Mamlaka ya mapato inachukua Kodi hata sehemu isiyo stahili mfano kijana ameamua kujiajiri kwa kufungua library au vigenge vidogo huko mtaani kwa mtaji mdogo lakini serikali inaingilia kati kutaka Kodi hapo muuzaji anaweza hata akajikuta amefunga kibanda kisa TRA.

Ukosefu wa ajira katika TAIFA huathiri zaidi taifa kiuchumi kwa sababu vijana umri kati ya 18-40 ambazo ndio nguvu kazi hujikuta wakiathirika zaidi na hivyo kuchangia asilimia chache za ujenzi wa taifa, Hali hii huleta athari zifuatazo:

1. Kukithiri kwa vitendo vya uhalifu, vijana waliokosa ajira huanza kujitafutia riziki kwa njia isiyo halali kama vile ujambazi, ukabaji, kujiuza kwa vijana wa kike na mauaji Kutokana na Imani za kishirikana wakiamini ndiyo njia sahihi za wao kutoka kwenye Hali ngumu ya maisha. Miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia uwepo wa magenge ya kiuhalifu kama vile PANYA ROAD, uwepo wa madada poa lakini hii yote husababishwa na ukosefu wa ajira.

2. Ongezeko la magonjwa ya akili kwa vijana. Vijana kati ya umri wa miaka 25-45 hukumbwa na matatizo ya akili na kuanza kuchanganikiwa pale wanapokosa shughuli sahihi ya kuwaingizia kipato na ilihali Wana majukumu ya kuhudumia familia. Kuna wengine wanafika mbali hata kuamua kukatisha uhai baada tu ya kukata tamaa ya maisha Kutokana na Hali ngumu.

3. Kuongezeka kwa matumizi ya madawa ya kulevya kwa nguvu kazi ya taifa. Vijana waliokata tamaa hujikuta wakishiriki matumizi ya madawa ya kulevya Kutokana na msongo wa mawazo, na Hali hii inaweza kusababisha matatizo ya akili pia.

Tanzania tuitatakayo ni Ile yenye vijana wenye tija wakiwajibika ipasavyo katika kulijenga taifa wakishirikiana na serikali katika kutatua changamoto za ajira. Katika kufanikisha hili napendekeza marekebisho kadhaa juu ya ajira katika ngazi mbalimbali tukianzia ngazi ya jamii mpaka wizarani.

1. SoMo la ujasiriamali lianzie nyumbani. Hapa tuangalie ushiriki wa mzazi/mlezi katika kumkuza mtoto namna ya kutumia mazingira yanayomzunguka. Kumekuwa na tabia ya wazazi au walezi kuwaweka watoto katika Hali ya ubize na masomo Hadi wakati wa likizo jambo linalofanya mtoto kutojifunza vitu nje ya elimu ya darasani, hata hivyo Kuna masomo ambayo yanahitaji ushiriki wa mazingira ili kuelewa zaidi. Mzazi au mlezi unapoandaa bustani ya mboga mboga mfunze mwanao namna ya kuhudumia hata kwa kupalilia ili siku akikosa kuajiriwa basi aweze kujiajiri na kwakuwa atakuwa amepata elimu basi atatumia vyema sayansi nateknolojia

2. Vyuo vya ufundi vitoe elimu kwa vitendo halisi na kwa ubora. Serikali imefanya jitihada katika kuanzisha vyuo vya ufundi VETA katika ngazi za kikanda na kimkoa lakini na vijana nao hawako nyumba katika kupata elimu, wengi wao wanapotoka kwenye mafunzo hayo hujiajiri. Sasa endapo vyuo hivi vitatoa elimu Bora zaidi basi itasaidia kuondoa tatizo la kukosa ajira na kupata vijana wenye ufundi Bora kuendana na uhitaji wa soko la ajira.

3. Bodi ya vyuo (TCU) ikishirikiana na serikali iweke mikakati juu ya udahili wa wanafunzi Wanaoendana na mahitaji ya ajira katika baadhi ya kozi.

4. Serikali iongeze juhudi katika kuwawezesha wajasiriamali hii itatufanya tufikie lengo la TANZANIA YA VIWANDA na kupunguza tatizo la ajira.

5. Somo la stadi za kazi kwa shule za msingi litiliwe mkazo na lifundishwe kwa vitendo kwa maana ndilo somo linalobeba dhana nzima ya ujasiriamali kwahiyo itamuwezesha kijana kujiajiri anapokosa ajira.

MWISHO.
 
Upvote 8
Back
Top Bottom