Ukuaji wa taifa lolote wenye kuleta tija unategemea nguvukazi kubwa sana ya vijana wake. Mathalani, rasilimali hii adhimu ya taifa imejikuta ikiachwa nyuma sana katika hatua mbalimbali za kuwezesha kunyambua tija mbalimbali zinazowazunguka na kuweza kufikia lengo la ukuaji wa taifa kwa ujumla.
Waswahili tuna msemo maarufu sana usemao nionyeshe rafiki zako, nami nitakutajia tabia zako. Usemi huu ukiutafakari kwa kina haujalenga moja kwa moja katika kuelezea marafiki zetu, ilhali umejikita haswa katika kunyumbua mchango wa mazingira yetu katika maisha yetu ya kila siku. Ukitazama maisha ya vijana wengi katika nyakati hizi yamejikita na kufanana sawia na mawimbi ya bahari au ziwa kubwa la maji. Ukitazama kwa jicho la nje mawimbi ya maji unaona yametulia, yapo pale pale hayasogei kwenda kokote, lakini ukitazama kwa umakini na kuelewa tabia zake kitaalamu ni mawimbi ambayo yanaweza kukupeleka mbali sana na kuleta matokeo makubwa yawe chanya au hasi.
Vijana wengi hapa nchini kwetu wana fikra nyingi bunifu lakini fikra zao zimeishia kuwa ndoto tu za kufikirika pasi na msaada wowote wa kuzigeuza fikra hizo kuwa kitu chenye tija. Watu wengi ikiwemo wanasiasa na viongozi mbalimbali wamekuwa wakihubiri juu ya suala zima la vijana kujiajiri, lakini je tumeengalia upande wa mazingira wezeshi kwa kijana huyu kujiajiri? Kwa mfano, unakuta kijana ana mtaji kidogo, lakini kupitia mtaji huo huo apate mahitaji yake ya msingi, aweze kusaidia familia yake na ndugu zake, na pia kwa mtaji huo huo aweze kupanua wigo wa biashara zake. Je, tunadhani ni kitu kinachowezekana kwa urahisi? Kwa jibu la haraka ni hapana kwa sababu hela atakayopata itaweza kwa kiasi kidogo kukidhi mahitaji yake lakini sio kwa kufanya kitu kwa muendelezo wa muda mrefu. Na hapo ndipo hazina hii adhimu ya taifa inaposhindwa kuwa na tija kwa mlengo mpana wa taifa hili.
Wahenga walisema usipoziba ufa, utajenga ukuta ndicho kiendeleacho katika maisgha yetu ya sasa. Kijana ambaye ndio msingi mkuu katika kuleta maendeleo amesahaulika kabisa, mwishowe tunaandaa taifa la kesho lisilo na mbele wala nyuma. Kimaadili, kifikra na vile vile kiuchumi tunashindwa kusogea sababu hatuna msingi imara wa kuwajenga vijana wetu.
Kutokana na kasi ya maendeleo na teknolojia tumeishia kuwa watu wa kuiga vitu vya wenzetu katika kila sehemu pasipo kufanya vitu vyenye tija kwa maendeleo yetu. Kwa sasa ni kawaida kukuta vijana wakishinda katika vijiwe vya michezo ya kubashiri, kukaa vijiweni wakipiga soga tu pasipo kujishughulisha na shughuli zozote za mendeleo, na hata wengine kujihusisha na vikundi vya uhalifu.
Pia, limeibuka wingi kubwa la vijana kuwa na tabia za kujipendekeza kwa mtu mwenye nacho katika nyanja mbalimbali iwe kisiasa, kiuchumi na hata kivyeo katika jamii zetu, kitu ambacho si kizuri kwa mustakabali wa Maisha yetu ya baadae. Haya yote ni matokeo ya kushindwa kuandaa na kujenga msingi mzuri kwa vijana kuelekea katika maendeleo ya taifa letu.
Je, nini kifanyike kuweza kulinusuru taifa letu? Ukitazama kwa mambo yanayoendelea ni dhahiri shahiri kwamba siasa imeshika hatamu ya maisha yetu. Ndio maana hivi sasa kote duniani wanamlenga kijana kwa sababu ndiye nguvu kazi ya taifa lakini katika namna ambayo haileti matokeo ya moja kwa moja kwake. Kuna sera nzuri sana zenye kujaribu kumkwamua kijana katika nyanja mbalimbali ikiwemo kilimo, ujasiriamali, viwanda na hata katika masuala mbalimbali ya michezo, sanaa na burudani. Lakini hizo sera zote zimegeuka propaganda zisizo na tija ya moja kwa moja kwa hao vijana na taifa letu kwa ujumla.
Kuna haja za dhati kabisa zinazotakiwa kufanyika ili kuweza kunusuru kuangamia kwa kundi hili ambalo ni kubwa na la muhimu sana katika jamii yetu. Ukuaji wa teknolojia umeshika hatamu duniani kote katika nchi zinazoendelea na zilizoendelea, lakini ni kwa namna gani tunaitumia teknolojia katika kujikwamua na kupiga hatua mbele? Hili ni swali la msingi ambalo tukiweza kulitatua linaweza likatusaidia moja kwa moja kuokoa kizazi hiki kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia.
Vile vile, kwenye suala zima la elimu za darasani, vitendo na hata elimu za kifedha ni vitu muhimu sana ambacho kinaweza kutusaidia katika maendeleo ya taifa letu. Ukitazama kwa makini, vijana wanapoenda katika taasisi mbalimbali za kielimu wanapata ujuzi lakini wanashindwa kuugeuza kuwa fursa nzuri ya kujijenga kwa kizazi kijacho na kujipatia kipato. Hii yote inachagizwa na mfumo wetu wa elimu na maisha ambao haumsaidii kijana kujitegemea pindi amalizapo masomo yake.
Masuala yahusuyo fedha limekuwa nalo ni janga kuu sana lisilo na mtatuzi, kwani vijana wengi wakipata fedha wameishia kuzifuja vibaya kwa matumizi yasiyo na tija. Hili jambo suluhu yake ni ushirikishwaji na ufundishwaji wa vijana katika nidhamu ya fedha kuanzia ngazi ya utotoni kupitia malezi ya wazazi. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, ukishindwa kuandaa msingi imara kwa mtoto wako maana yake unamuandalia nyumba mbovu ya baadae.
Katika suala zima la masuala ya kujenga fikra yakinifu ana afya za akili, vijana wanapaswa pia kupewa huduma mbalimbali zihusuzo mambo hayo na yote yanayoendelea katika jamii na hivyo kuwasaidia katika kuishi na jamii inayowazunguka vizuri. Kuna wimbi kubwa la vijana ambao wanafanya mambo kwa kuwaiga wenzao lakini hayana tija yoyote kwao. Hili linaweza kutatuliwa kwa kusaidia kumjengea fikra za kuweza kujitambua na kuweza kupamnbana na changamoto zote zilizopo katika jamii yake kupitia upembuzi wa mambo mbalimbali.
Mwisho kabisa, waswahili tunasema nyota njema, huonekana asubuhi. Hivyo basi kwa jamii yetu ya sasa yatupaswa tuamke na kufanya kwa vitendo vitu mbalimbali vinavyoweza kuwa msaada katika Maisha yetu na taifa letu la baadae kwa ujumla. Upangaji mzuri na utekelezaji wa mipango ni msingi mkuu katika kuleta maendeleo ya nchi yetu. Tukishindwa kupanga na kutekeleza mipango yetu maana yake tumejipanga kushindwa.

Upvote
2