Nchama matinde
New Member
- Jun 25, 2024
- 1
- 0
Tanzania tuitakayo itajengwa na mimi,wewe na yule.
Habari wanajukwaa, napenda kuchukua nafasi hii adhimu kuwasilisha wazo langu kama raia mwema na mwenye mapenzi kwa taifa langu huku nikiwa na shauku ya kuifikia Tanzania tuitakayo!
Napenda kutoa mawazo yangu kwa wizara ya kilimo na mifugo
Mimi kwa fikra zangu nikafikiria kwa mfano wizara yetu hii ya kilimo na mifugo ikiamua kubuni mradi wa ufugaji wa wanyama na kilimo (ranchi)kwenye kila mkoa hapa nchini.
Yaani kwa mfano kama tunavyojua kuwa Tanzania yetu ina kilometa za mraba za kutosha na kwamba makazi yetu hayajafikia hata nusu ya ya eneo zima,hivyo utagundua kuwa hifadhi,maeneo ya wazi na mbuga za wanyama ni maeneo yaliyochukua nafasi kubwa zaidi kuliko makazi ya watu.Kwa mantiki hiyo, tukitoa maeneo yenye mbuga za wanyama,maeneo ya wazi na hifadhi zetu za taifa tunaweza kutenga maeneo kwa ajili ya kuanzisha ranchi kubwa kwa utaratibu ufuatao

- Kuandaliwe eneo kwenye kila mkoa ambalo linaweza kuwa na ubora kwa shughuli za kilimo na ufugaji
- Ijengwe miundombinu inayofaa kwa shughuli za ufugaji na kilimo
- Kichimbwe kisima kitakachowezesha shughuli za umwagiliaji kwa urahisi
- Waandaliwe vijana watakaowajibika na shughuli zote za ranchi (hapa namaanisha ufanyike usaili ili kupata vijana wenye vigezo kwenye mkoa husika angalau vijana 30)
- Uendeshaji wa ranchi uwe kama taasisi inayojitegemea kama zilivyo taasisi zingine mf, taasisi ya elimu,afya na nyinginezo(hapa namaanisha mradi wa ranchi utakapoimarka uwe na utaratibu wa utoaji wa ajira kama zinavyotolewa ajira za ualimu,uuguzi n.k) hii itasaidia kuwapa matumaini vijana wetu walioko vyuoni kuwa baada ya kuhitimu ngazi fulani ya elimu wanaweza kupata ajira katika ranchi zilizopo nchini,japo haimaanishi kugandisha mawazo yao ya kuwa wabunifu na kujiajiri
- Taasisi hii iwe na uongozi madhubuti na wapatikane watu wenye mtazamo chanya,weredi na wazalendo
- Vijana waajiriwe kwa mtazamo wa manufaa ya baadae,hapa namaanisha kuwa vijana waajiriwa wakubali kuanza kwa kidogo kitakachopatikana kisha mambo yatakapokuwa mazuri basi wawe wanufaika wa kwanza katika kupata ajira za kudumu endapo mradi utafanikiwa
- Idadi ya watumishi izingatie ukubwa wa mradi ambao kiuhalisia utasimamiwa na halmashauri za mkoa chini ya ya Afisa kilimo na mifugo wa mkoa
- Kuundwe kamati inayoweza kusimamia mradi kwa bajeti isiyoleta hasara
- Ranchi ianze na idadi ndogo ya wafanyakazi wenye moyo wa kujituma kwa hali na mali na kauli mbiu iwe "uwekezaji kwa manufaa ya usoni"
- katika mradi huu kuwepo na kilimo endelevu kitakachosaidia upatikanaji wa malisho ya mifugo kwa urahisi
- Mradi huu uende sambamba na upandaji wa miti kando ya eneo zima la ranchi ili kuepuka ukame na uharibifu wa mazingira na pia kuboresha mandhari
- Vijana waajiriwa wahudumiwe kama serikali inavyohudumia wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya serikali na wapewe posho kidogo za kujikimu kwa nauli na malazi au ikiwezekana wajengewe hosteli ili waishi hukohuko kwenye mradi
- Kama wafanyakazi watakuwa wanakuja asubuhi na kuondoka jioni basi kuwepo na ulinzi wa kuwakagua waingiapo na watokapo(in and out inspection)
- Faida za mradi huu
- Itasaidia kuongeza ajira kwa vijana wanaohitimu ngazi mbalimbali za elimu
- Itasaidia kupunguza vijana wa mtaani waliojaa katika mikoa pasi na kazi za kufanya maana hao ndio watakaotumika katika uanzilishi wa miradi hiyo ili kuepuka gharama za kuajiri wasomi ambao wengi wao hutarajia kuingia kwenye system moja kwa moja angali mradi utakuwa haujaimarika,japokuwa mradi utaanza kwa majaribio lakini kwa uhakika
- Inaweza kupelekea nchi yetu kuwa mzalishaji wa juu wa mifugo yote inayozalishwa Afrika na duniani kwa ujumla
- Inaweza kupunguza baa la njaa nchini linalojitokeza mara kwa mara
- Itasaidia kuongeza pato la nchi kupitia uuzaji wa bidhaa zitakazozalishwa
- Itachochea uanzishwaji wa viwanda kutokana na kuwa na malighafi za kutosha
- Itasaidia kuibua vipaji na ubunifu kwa vijana wakiwa field na itapelekea kupata wataalamu wenye ujuzi kwa vitendo
- Itasaidia maafisa kilimo kupata wigo mpana wa kulitumikia taifa
- Mradi unaweza kusambaza mazao kama maziwa na mayai kwa wananchi kwa bei nafuu ili kuwasaidia wananchi wengi kujipatia bidhaa hizo hata kwa wale waliokuwa wanashindwa kumudu gharama za kununua, usambazaji unaweza kuwa wa bili au kwa malipo ya papo hapo na hivyo kujiingizia pesa za uendeshaji mradi pamoja na kuwanufaisha wananchi kwa kuboresha afya zao