Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Kama kuna kitu nimejifunza kutokana na kurushiana maneno kati ya Trump na rais wa Marekani na Zelensky wa Ukraine, ni kwamba vita vinaweza kusanbabisha mtu kuuza nchi yake.
Marekani imetumia pesa nyingi kumsaidia Ukraine kupambana na Urusi.
Pesa hizo ziko kwa mfumo wa vifaa vya kijeshi na fedha za kujiendesha nchi ya Ukrain.
Trump ameingia madarakani naye hataki kabisa vita, na anataka Ukraine ianze kulipa fedha ilizoikopesha kwa kuila kwa njia ya madini yanayopatikana nchini Ukraine.
Trumpa anajua kwamba Ukraine haina pesa ya kurudisha, basi ikaona Zelensky alipe kwa kumpatia hako ya kumiliki 50% ya vitalu vyote vya madini muhimu hadi deni hilo likamilike.
Masikini Zelensky, jana alikuwa kama mtoto mdogo akikaripiwa na Trump na Makamu wa Rais JD Vance, wakati yeye akiwaya waya mbele ya dunia nzima.
FUNZO KWA TANZANIA
Tusije ingia vita visivyotuhusu, maana mtaji wetu wa madini kuna watu wanaukodoleamacho. Katika mgogoro wowote kuna mataifa yapo ytayari kukupa chochote alimradi wanajua utashindwa kulipa .
Na ukishindwa kulipa macho ya wakopeshaji yataelekea Buzwagi!