Offshore Seamen
JF-Expert Member
- Mar 9, 2018
- 5,489
- 14,091
Marine Cyber Attack ni uvamizi wa mifumo ya uendeshaji wa shughuli za Meli na Bandari. Ambayo inahusisha Bandari, mawakala wa Meli na forodha, idara za Kodi na wenye mizigo.
Shirika la kimataifa linalosimamia Mambo ya Bahari, International Maritime Organization (IMO) baada ya mashambulio na tishio kwenye bahari na bandari walikuja na Sheria za udhibiti miaka ya 2001. Nchi za Ulaya kama Uholanzi wamewahi kupata shambulio kutoka kwa hackers waliovamia system na kupelekea hasara.
Wiki iliyopita tarehe 22/07/2021 nchi ya South Africa mfumo kwenye Shirika lao linalosimamia bandari na reli la Transnet mfumo wa It ulivamiwa na hackers na kupelekea kutokuwepo huduma kwa siku 2 na kusababisha foleni kubwa kwenye bandari zao na hasara kubwa. Hii imepelekea mpaka watumie mfumo wa manual documentation kupunguza kadhia.
Hasara waliyopata ni kontena zenye kuhitaji ubaridi ili zitunze mzigo kuharibika na mzigo upatao Tani 40,000. Baadhi ya wasafirisha matunda ya Citrus walihama bandari za South Africa na kwenda kutumia bandari ya Maputo.
Hii imepelekea hofu ya usalama wa nchi ambapo silaha au vitu hatari kupitishwa. Raia wametaka uongozi wa Transnet kujiuzulu.
Tanzania tuna mengi ya kujifunza na mfumo wetu wa TANCIS ambao mara Kwa mara huwa na tatizo la mtandao.