Lekanjobe Kubinika
JF-Expert Member
- Dec 6, 2006
- 3,019
- 579
Ubabe wa serikali haukuuzi uchumi wa nchi, bali nchi legelege isiyokwenda kijasiliamali hubakia ombaomba na kuwa mtumwa wa kudumu. Serikali kaidi haijifunui upevu wake kwa njia ya kiuchumi bali viongozi wasio adilifu huififisha nchi Nyerere Julius Kambarage Mwalimu alisema mara kadha kwamba kiongozi mpumbavu ni kama dodoki ambalo huwa bishi sana kwa kung'ang'ania kuzoa kila kitu kwenye maji pasi kuchuja ili kuchukuwa kizuri na kuachana na kisichofaa, lakini kiongozi mjinga ni mwepesi kusima mazingira na kujifunza kinachokosekana katika jamii nakisha huumiza kichwa kubuni namna ya kuondokana na matatizo ya jamii kwa kumobilize resources zilizopo ambayo kubwa yake ni WATU, ARDHI, SIASA SAFI na UONGOZI BORA.
Watu tunao Tanzania, tena waoga kwa serikali yao kwani wanatii haraka sana maagizo ya serikali zao na ndio maana misamiati kibao inamwagwa vichwani mwao kila kukicha nao wanakunywa tu kimya kimywa kwa sababu wana njaa sana ya kubadilisha hali ya maisha yao yawe bora zaidi ....mfano Kilimo ni uti wa mgongo, Kazi ni Kilimo, MKUKUTA, MKURABITA, BRN, Mtu ni Afya na kadhalika, lakini hakuna kinachotoa matokeo endelevu, viongozi wanabuni njia za kufyamba mali za nchi kwa mbinu hizo ambazo wanaoteshwa tu usiku na mchana na wakishavuna kiasi wanachotaka huanchana na dhana hizo. Wananchi wakiiambia serikali yao nini wanachotaka, wanaambiwa hawana akili ni wafinyu wa kufikiri na wana wivu wa kike. Wasomi wengi huzalishwa nchini na tafiti nyingi za kitaalam zinafanywa lakini serikali haisikii wala kusoma. Watu wa nchi za nje wakitumia matokeo hayo na wataalam hao wanashangaa kwa nini Tanzania imeshindwa kuendelea. Sasa watu makini sana wanafanya kazi nchi za kigeni kwa tija lakini Tanzania tunaletewa EXPATRIETS kuja nchini kwetu kutafuna raslimali zetu tukichekelea na watu wetu wakiendelea kudidimia kiuchumi na kimaisha kwa ujumla. Serikali zetu ziawaenzi sana wageni na kuwainua sana kwa kuwaita WAWEKEZAJI na halafu hao hawaji na hata senti tano, wanakopa kwenye mabenki yetu kwa riba kiduchu na kuondolewa kwenye orodha ya kodi kwa miaka, say mitano - halafu jamaa wenye akili huuza kwa wageni wengine kabla ya kuisha miaka mitano na hao wapya nao huvaa joho lilelile la WAWEKEZAJI na kupata uhalali wa kusamehewa kodi.... It is a vicious circle....mjinga ndiye aliwaye.
Ardhi kubwa sana, tena yenye rutuba kwa wingi na chini yake kukisheheni madini lukuki. Nyerere Mwalimu alijitahidi kutoharibu mali asili kwa kutoiweka ardhi kuwa huria kwa kila binadamu wa ndani au nje. Lakini waliomfuata walimpuza yeye na fikra zake ambazo walimwimbia kwamba zidumu fikra zake akiwa madarakani, ghafla wakaenda Zanzibar na kumnyongelea mbali na fikra zake na kuvaa ubepari na ukabaila ambao walifundishwa kwamba havifai kwa wajamaa. Kumbe wakaanza kukimbizana wao kwa wao kwenda kuwadanganya wananchi na kuodhi maelfu elfu ya ardhi ambayo hawaiendelezi katu wakiwaacha wananchi wenye huo uti wa mgongo pasipo ardhi (sijui walidhania kilimo kitafanywa hewani???). Wananchi wameachiwa magomvi wakiuana kwa sababu ardhi iliyobaki ni kidogo na isiyo na rutuba wala kufaa kwa matumizi ya kilimo na mifugo ama kwa sababu haina rutuba kwa kuwa yenye rutuba imechukuliwa na viongozi serikalini ama kwa kuwa vipande vidogo hivyo vimechoka kwa kutumiwa kila mara kwa muda mrefu hata kukosa value kwa matumizi hayo. Wakulima na wafugaji wanauana kila siku na serikali inaongea siasa tu pasipo kuchukuwa hatua zozote zenye maana. Wageni wamemilikishwa hekari kedekede na wanalindwa na mapolisi wetu kwa gahrama za nchi. Majirani za wawekezaji hao wanatunguliwa utadhani mawindoni kila mara ati wanavamia maeneo ya kiwekezaji. (Serikali zezeta ni afadhari kuliko jinga kwa sababu wanafanya kwa makusudi wakijua wanafanya nini). Watu wanapofikiria kila siku juu ya usalama wao watawezaje kufikiria juu ya kujikwamua kiuchumi?
Uongozi ndio huo unaozuia maendeleo ila kujilimbikizia utajiri wanaokwapua kutoka kwa mama nitilie na machinga. Angalia sasa wafanya biashara wakubwa na wenye kuingiza vipato sana wengi wao hawalipi kodi. Uongozi bora ungetarajiwa kuweka mazingira muafaka ya kuinua mamilionea wengi ambao wangelipa kodi za uhakika na endelevu kwa kuwawezesha wazalishe zaidi ili kuuza ziada nyingi nje na kupata fedha za kigeni kusudi kuimarisha thamani ya shilingi yetu. Lakini serikali yetu inatwanga nyundo mtu yeyote anayejaribu kuinuka kiuchumi kutoka kwenye shughuli ndogondogo za kiuchumi kama wamachinga na mamanitilie na wafanyakazi. Wanawakamua kupitia TRA kwa kutunga sharia za hovyo na kandamizi kiuchumi ili watu waioko tayari kujishughulisha waogope kufanya shughuli za kiuchumi maana wanapata hasara kila siku na wanawekewa vizingiti hovyo vingiiii! Ndio maana migomo ya wafanyabiashara ni mingi mno na serikali inaongea kiburi tu, wala hawafikirii kwamba mfanyabiashara akifunga ofisi yake saa moja tu serikali nayo inakula kwake kwa kukosa mapato, wanota kuvuruga mifumo ya kibiashara kila siku kwa kutunga sharia subjectively unaweza kukataa kama wamewahi kwenda shule. Mfano ni miswada ya juzi tu inayokandamiza watu wengine utadhani wao wenyewe wanaishi sayari nyingine....mimi Napata taabu sana kwaelewa viongozi hao. Sasa ubora wao viongozi wetu ni katika kutoa miongozo inayoumiza watu wao badala ya kuwa miongozo rafiki kiuchumi. Kenya na Rwanda hawako sayari tofauti, lakini wako mbali mno. Rwanda pamoja na kuwa wamo katika vita kila mara lakini hata hela yao inayo nguvu kuliko matarajio. Viongozi wetu badala ya kujifunza huko wnaeleza sababu za kijinga sana utadhani maendeleo hayawahusu, wanaashiria yaleyale, wivu wa kike. Wanashindwa hata kufikiria kuboresha mahusiano na majirani ili kuvutia biashara zaidi kwa kutumia fulsa zilizopo kama bandari kedekede, miundombinu na utaalam uliopo miongoni mwa watu wake. Tena viongozi wengi wa nchi hizo wamesomea hapahapa kwenye vyuo vyeto kama kina Museveni na kina Kagame. Kwa hiyo nchi hii inawafundisha wageni wakaendeleze kwao wakati sisi wenyewe can't put into practice what we train the foreigners on. Ukienda kule utakuta wataalam wa kitanzania kibao wanatunzwa vizuri na wanajituma kwelikweli maana mazingira yao safiii!! Hata ushauri mwingine tunaomba ugenini kumbe tunalipa pesa nyingi kwa ushauri huo kumbe wanaotutengenezea ushauri huo ukitizama unakuta ni watanzania kabisa wa hapahapa manerumango ila wanatumika ugenini. Watu wazima sie hovyoooo! Viongozi waliopo kama zezeta vile maana wanaingiza siasa kwa sana kwenye mambo ya kiprofession. Angalia ulivyoharibiwa mchakato wa Katiba mpya. Ulianza vizuri kwa weledi hasa, viongozi wetu walipoona hisia kwamba Katiba mpya inaelekea kuwapoka mirija yao ya kujinufaisha binafsi na jamaa zao, wakaingiza siasa ati "Chama change hakipendi hiki na kile....." Unategemea wewe kama kiongozi ukisema maelezo hayo halafu utegemee wao waende kinyume na unachopenda wewe??? Mnajifunzia wapi mambo ya kiutawala nyie???
Siasa safi inawezekana kwa watanzania maana ndio wanapenda sana siasa siasa maana siasa zetu wabongo zimejaa michomekeo ya kutegesheana ili upate zaidi ya mwenzako unachokipenda. Hakuna lugha ya win-win Tanzania bali jitahidi kuwa na macho kama ya nyoka mwenye makengeza. Sera zinapangwa kwa utamu kuburudisha akili za wanaokusikiliza ili uwavute wakupe dhamana. Ukishapata dhamana unatanua tu na wao watajiju. Sera ngumu na complex ambazo hata kwa asiyeenda shule atakuambia hzitekelezeki lakini ukiona anakusumbiua sana akili unamkolimba, unamlimboka, unamwakyembe, unamdaudi mwangosi na kadhalika kw hiyo wananchi wanapaswa kukusifia tu hata kama unajua hauna kitu hapo. Kama mfalme Juha vile ambaye hata akitoka nje yu uchi anafurahi kusifiwa kwa kuvaa suti kali sana. Sera zinazalishwa kila kunapokaribia kipindi cha uchaguzi, ukipita na sera zinawekwa kabatini. Hapa sera zinazotufaa Tanzania ni za msituni ambapo mwenye nguvu ndiye mwenye stahili ya kufaidika. Kila aliuye nacho huongezewa na asiye nacho hunyang'anywa hata kile kidogo ambacho angestahili kuwa nacho. Siasa safi kwetu wabongo ni kushika madaraka na kusafiri sana nje ya nchi na kupata umaarufu, hata kama watu wako wanakuwa fukara huna haja kujua kwa nini watu wako ni fukara, bali unapanga mikakati isiyofika mwisho kila siku na mikakati isiyokuingizia faida binafsi unaipiga chini. Hiyo ndio siasa safi. Unakuwa mzuri kuzitetea sera zako ili ushike madaraka lakini ukishapata madaraka kazi yako ni kutunga sera za kuyalinda madaraka yako hata kama kwa kufanya hivyo watu wako watauwawa. Maana hakuna namna nyingine sasa, unachoka sasa maana watu wako watakwa wajeuri wanaojifanya wao ni zaidi yako na kwa hiyo utatumia dola ulilokabidhiwa ili kulinda utawala wako na mirija yako iendelee kukamua zaidi. je nchi zilizoendelea zinafanya hivyo? Maana viongozi wetu ni hodari sana kutembelea nchi za kigeni tukitaraji watajifunza huko mbinu mpya za kuwaendeleza wananchi wetu kiuchumi, kumbe ni kutembeza bakuli kuombaomba tu??
Tuendapo kwa wenzetu basi watanzania tujifunze yaliyo na tija na tukirudi tuyatumie hata kama yanaumiza wakati wa kuyatumia, ili mradi yalete tija kiuchumi nchini kwetu. Tusipende kunyosheana vidole tu kiunafiki. Siasa iwe part and parcel ya mikakati ya kiuchumi. Kagame alishasema kama angekuwa rais wa Tanzania na bandari moja tu ya DSM, elimu nchini ingekuwa bure kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu maana kusingekuwa maswali ya fedha za kuendeshea elimu. Tanzania tusimbeze Kagame bali tuwe na akili kumdadisi atupatie maono yake yalivyo namna ya kuyafanyia kazi badala ya kumfanya adui yetu kimtizamo.