^Burden of proof iko kwako, nitajie faida ya commonwealth.
Hizo sponsorship mwishoni zinasaidia waingereza zaidi ya watanzania, niambie ni wangapi wamerudi baada ya kusomeshwa?
Ni wajibu wa serikari ya Tanzania kusomesha raia wake ,si wajibu wa uingereza kwa hiyo hizo sponsorship sio sababu ya kutetea commonwealth.
Commonwealth ni uendelezaji tu wa mawazo tegemezi ya viongozi wetu ambao mpaka joho la Bunge wanashoneshea Uingereza.
Tuimarishe kwanza local organisations kama AU na EAC, kwa kuwa hizi zitasaidia kumuinua mtu wa kawaida, kufanya biashara na majirani n.k.Kama commonwealth ina meno kweli mbona bado Uingereza haijaondoa subsidies kutoka kwa wakulima wao ili wakulima wetu waweze kuuza bidhaa zao huko ulaya waondokane na kutegemea misaada, wasomeshe watoto wao n.k?
Ndio maana ninasema wataongea maneno tu, labda watakaopata faida ni machangudoa tu wa kampala, na vipesa vya hapa na palemahotelini.Mkutano ukiisha,hali itabaki palepale.