emback
JF-Expert Member
- Jan 3, 2013
- 444
- 372
Habari za muda huu ndugu zangu watanzania, nimewaza sana na kutafakari ni wapi kama taifa tunaelekea maana ukweli usiopingika kuwa tunazama huku tukijifariji kuwa tupo katika njia sahihi.
Tumeanguka katika nyanja nyingi lakini mie napenda niongelee moja au mbili, ambapo nitaanza na nyanja ya uwajibikaji, watumishi wengi na wa kada tofauti tofauti elimu, nishati, jeshi, bunge, sheria, mawasiliano nk.
Nitatolea mfano katika mawasiliano watu wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea ukiangalia shirika letu pendwa la umma ttcl hawa wapo wanakufa kifo cha kimya kimya na hakuna wa kuwaambia kitu maana wameridhika na kifo chao...mteja unaweza omba huduma mpaka uje uipate hiyo huduma ni kivumbi na jasho, na ukishapata huduma siku umepata changamoto kuja kuitatua ni kama umeanza moja.
TANESCO hawa hata siwezi kusema, afya nako ni uozo na kwingineko.
Ambacho nnaona kingefanyika ni kila mfanyakazi na alipwe kulingana na uzalishaji wake au ufanisi wake katika kazi yaani sio ikifika mwisho wa mwezi mshahara unaingia kama ilivyo now, hapana ikifika mwisho wa mwezi tufanye tathmini ya kile ulichozalisha katika kazi yako ndio ulipwe. Kama hakuna ulichozalisha zaidi ya umbea basi ulipwe umbea.
Kwa maana nyingine tuweke malengo( taget) kwa kila nyanja na tunapotaka kulipa tunakagua ufanisi wa kazi uliyopewa unalipwa kulingana na asimia ulizofikia....na kama umezidisha pia bonus ihusike kwa maana nyingine ulipwe zaidi.
Hii italeta ufanisi, hofu ya kupoteza mapato,na ushindani na ubunifu mkubwa katika kila nyanja ambapo hospitali utapokelewa vizuri na kuhudumiwa kwa wakati maana anataka chati yake ipande, mwalimu atatumia maarifa yake vizuri ili apate ugali wake vizuri, mbuge atapambana kutatua kero za raia wake maana anahakika kuwa pesa yake ipo mikononi mwa wapiga kura wake TANESCO tutasahau umeme kukatika maana itashusha viwango vyao ....ufupi kila mtu atajua kuwa njaa yake ndio engine yake.
Tusiogope kuanza moja na inawezekana.

Upvote
1