Marapai
JF-Expert Member
- Jun 11, 2013
- 314
- 376
Nchini chile katika uwanja wa ndege wa Santiago , kulitokea wizi wa dola milioni 7 sawa na pesos bilioni 4 za chile. Fedha zilizokuwa zinasafirishwa kaskazini mwa nchi hiyo kwa ajili ya malipo ya kampuni za kimarekani. Habari zinasema hili sio tukio la kwanza nchini chile , mwaka 2006 kwenye uwanja huo huo wezi waliiba kiasi cha dola milioni 1.6 lakini polisi walifanikiwa kuwakamata na wanaendelea na vifungo huko huko chile .
Tukio kama hili liliwahi kutokea kwetu uwanja wa ndege ambapo dola milioni 1 ziliibiwa kutoka kwenye gari ya kubebea fedha na mtuhumiwa wa
mkuu alishakamatwa na kuhukumiwa. Tukio hili la chile , haliwezi kupita bila kulijadili kitekinologia kidogo jinsi wezi
wenyewe walivyoingia na walivyoweza kuzima vyombo kadhaa na kuwezakuondoka na mzigo wote huo.
Taarifa za awali za video zilionesha kuwa watu hao waliingia na gari aina ya van, saa nne asubuhi kama wafanyakazi na baada ya dakika 4 gari hilo
liliondoka lakini tukio lenyewe la kupora halikurekodiwa kwenye video. Ukiangalia taarifa za awali inaonyesha uwanja wa ndege wa Santiago hauna
wigo wa kamera za ulinzi na inaonyesha kamera ziko maeneo machache na sio uwanja na nje kidogo
ya uwanja .
Pale walipoingia kama walipita kwenye mfumo wa usalama ina maana sura zao zilitakiwa zirekodiwe na kuhifadhiwa na kama walikuwa na historia yoyote ya uhalifu au wanatafutwa na mamlaka basi taarifa zingefika moja kwa moja kwenye vyombo husika , tekinologia hii inaitwa Face Recognition au kitambua sura ( uso ). Kwa kutumia tekinologia hii mataifa mengi yamefanikiwa kutambua wahalifu wanaotafutwa sehemu mbalimbali duniani haswa wanapotembelea maeneo ya jumuiya kama nyumba za ibada , viwanja vya mpira , maandamano na vituo vya mabasi .
Pili inawezekana wahalifu walikuwa na vifaa vya kujam mawasiliano ya uwanja au eneo hilo tu la tukio haswa mawasiliano ya simu , radio na vifaa vingine vya mawasiliano, ndio maana tukio lilivyotokea uwanja haukuwa na taarifa yoyote mpaka walivyoondoka .Hili la pili inaonyesha wahalifu walishasoma mfumo wa mawasiliano na ulinzi haswa wa vifaa vya uwanja, kwahiyo ikawa rahisi wao kuingia na vifaa vyao vya kuifanya mitambo husika ikate mawasiliano. Hii inatufunza kutumia kampuni tofauti kwa ajili ya kulinda uwanja pamoja na usimamizi wa mawasiliano ya uwanja ukiacha jeshi la polisi , mamlaka za uwanja na idara nyingine za serikali kama ni uhalifu huwezi kupita kote huko na kufanikiwa haswa kwenye uwanja wa ndege .
Tatu inawezekana walitumika wahalifu wa mtandao kuvamia mfumo wa mawasiliano na hifadhi wa uwanja haswa muda ambao tukio lilikuwa linatokea inawezekana ni virus au aina nyingine ya kuleta mkanganyiko na ukiongeza hiyo jamming basi ni mwisho. Hili la tatu linatufundisha jambo moja, tuwe na aina mbili au zaidi za kuhifadhi taarifa, nyingine ziwe nje ya ofisi au nje ya nchi na nyingine ni hapo hapo ndani ya uwanja ingawa kuna risk nyingine za kuhifadhi nje au kutumia kampuni maalum haswa za nje maana zinaweza kushirikiana na mashirika ya kijasusi kutoa taarifa za viongozi na watu wengine wanapopita ndani ya uwanja husika.
Nne wahalifu hawa walikuwa 8 , lazima walibeba vitu vya kufanyia kazi yenyewe , kujishika inavyoweza kuacha alama za vidole ingawa wanaweza kuvaa vifaa maalumu mikononi au nywele na mawasiliano kati yao wakati wanafanya tukio na kuondoka , vyote hivi ni ushahidi . Wahalifu hawa waliondoka na magari 2 , wakapita njia tofauti na moja wakalitekeleza sehemu , lazima walipita kwenye mataa na sehemu nyingine ambazo kuna kamera za siri za kunasa vitu kama hivyo , kwahiyo tungoje .
Pia tukumbuke nchi za amerika kusini ambapo chile ipo kuna rushwa za hali ya juu , inawezekana rushwa kutumika kulainisha mambo ili uhalifu ufanyike kwa urahisi na kutokomea kama ilivyoonekana .
Mwisho ni kuomba wenzangu wenye uelewa wa mambo mbalimbali unaofanana na huu wawe wanaandika makala na ushauri yanapotokea matukio kama haya ili iweze kuamshawatu na kuelimisha umma kwa ujumla .