Tanzania tumeweka record mpya

Tanzania tumeweka record mpya

MIDFIELD

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2013
Posts
1,944
Reaction score
702
Jana usiku timu yetu ya taifa kwa kitendo cha kuchapwa bao 7 kwa bila, bila shaka hii ni record mpya ambayo tumeiandika kwani toka miaka ya nyuma nimejua habari za soccer mpaka leo hii sijawahi kuona wala kusikia kwamba tumewahi kupigwa goli nyingi kama hizo kwa miaka ya nyuma toka uhuru. Ni kutokana na mantiki hii ndo maana nimesema tumeandika record mpya. Kuandika record siyo lazima kwa mazuri tu, hata mabaya ni record jamani. Sina uhakika 100% juu ya hili, ila kwa mwenye data/kumbukumbu tunaomba atufahamishe akitutajia mwaka, magoli tuliyofungwa, timu iliyotufunga na mchezo ulichezewa wapi.
Karibuni Great thinkers tujadiliane na the way Forward
 
Mara ya mwisho timu ya Tanzania kupigwa sana nje ya nchi katika mechi za mashindano ilikuwa tarehe 20/09/1998 ambapo Yanga SC (wakimataifa) walipigwa 6-0 na Raja Casablanca ya Morocco
 
Ok, ilikuwa ni Yanga kama club au timu ta Taifa
 
Mara ya mwisho timu ya Tanzania kupigwa sana nje ya nchi katika mechi za mashindano ilikuwa tarehe 20/09/1998 ambapo Yanga SC (wakimataifa) walipigwa 6-0 na Raja Casablanca ya Morocco

Tunazungumzia timu ya taifa na sio club yetu ya Yanga.Usitukumbishie machungu,sisi tumeshasahau vp wewe ..
 
Mm nakumbuka Cku simba walivyo tufunga yanga tano,,,,,,,,,
 
Mm nakumbuka Cku simba walivyo tufunga yanga tano,,,,,,,,,
.

Hahaaaa, sawa lakini tunaongelea timu ya Taifa, yani Taifa Stars. Je, kuna kipigigo ilishawahi kupata kama hiki au zaidi ya hiki huko nyuma? kama ni bado basi ina maana hii ni record mpya au vp
 
Nilichoona jana sisi sub-Sahara bado tuna tatizo la mental slavery (inauma sana kusema haya lakini ndio mwanzo wa kujitambua).

Yaani refa Mkameroni kazi yake ni kutoa penati na kadi tu hata zisipotakiwa, ndio maana kumuonyesha Mtz yellow alafu wachezaji wa Algeria wanamfuata kumwambia 'hii ni ya pili' then akampa nyekundu!
Lakini pia na watangazaji wetu hapa wanaonyesha wazi 'upenzi' wao kwa Algeria, sijaelewa ni sababu ya ideology ama nini. Uzalendo na umoja wa timu unaanzia kwa mashabiki, wapenzi, watangazaji, makocha, wanasiasa, viongozi nk nk.

Ambaye hajaelewa ninachojaribu kusema anaweza kuwa anapitia kwenye hii link apatapo muda, sio kwa nia mbaya lakini:
>>>>THE REUNION OF BLACK FAMILY WORLD WIDE
 
Taifa star'ziiiiii nikumbushe ndyo kitu gani?
 
Tumwombe Jecha Afute Matokeo ya Mechi ya Jana, Hadi Hapo Baadae Atakapoona Inafaa Kuchezwa Mechi ya Marudiano.
 
nadhani ni timu ya shule flan waliamua kuchezesha darasa la 1 (Taifa staaaziii) na darasa la 7 (Algeria). Hii si haki
 
Tuachane na jina la Taifa Stars tuwaite Serengeti Wildebeests angalau tutaambulia kutangaza utalii kidogo....
 
Nilichoona jana sisi sub-Sahara bado tuna tatizo la mental slavery (inauma sana kusema haya lakini ndio mwanzo wa kujitambua).

Yaani refa Mkameroni kazi yake ni kutoa penati na kadi tu hata zisipotakiwa, ndio maana kumuonyesha Mtz yellow alafu wachezaji wa Algeria wanamfuata kumwambia 'hii ni ya pili' then akampa nyekundu!
Lakini pia na watangazaji wetu hapa wanaonyesha wazi 'upenzi' wao kwa Algeria, sijaelewa ni sababu ya ideology ama nini. Uzalendo na umoja wa timu unaanzia kwa mashabiki, wapenzi, watangazaji, makocha, wanasiasa, viongozi nk nk.

Ambaye hajaelewa ninachojaribu kusema anaweza kuwa anapitia kwenye hii link apatapo muda, sio kwa nia mbaya lakini:
>>>>THE REUNION OF BLACK FAMILY WORLD WIDE

Mkuu lukindo nakubaliana na wewe kabisa kuhusu refa. Yaani nilimshangaa alikuwa mwepesi sana kutoa card kwa upande wa weusi wenzake kuliko kwa waarabu. hili limenipa tabu sana hasa nikiangalia penalt ya kwanza, ukichunguza vzr utagundua mchezaji wa stars alifanyiwa rafu kabla lkn refa akajifanya hakuona,ila akaona ya mwarabu kuangushwa. Kwa mtazamo wangu refa itakuwa alipewa chochote kuhakikisha algeria inashinda au ndo hilo ulilosema mental slavery
 
Hata mimi sijawahi shuhudia tukipigwa saba toka nianze kufahamu soka ni nini!
Kwa upande wa timu nakumbuka TANO ZA YANGA HAPA TZ.
 
Mara ya mwisho timu ya Tanzania kupigwa sana nje ya nchi katika mechi za mashindano ilikuwa tarehe 20/09/1998 ambapo Yanga SC (wakimataifa) walipigwa 6-0 na Raja Casablanca ya Morocco
Upande wa club nimeshuhudia timu kubwa ya Tz yanga wakila sita huko Casa Blanca, yaani saba kasoro moja, na pia huyo huyo yanga akalishwa 5 kwa nunge na mnyama, yaani saba kasoro mbili.
 
Mabeki wote Yanga, golikipa yanga! Jana kafungwa Yanga, na Tp Mazembe...

Eti Samata anataka kucheza mpira nje ya Arica..wapi...Labda hapo hapo Mazembe, not Europe
 
Tunazungumzia timu ya taifa na sio club yetu ya Yanga.Usitukumbishie machungu,sisi tumeshasahau vp wewe ..

Upande wa club yanga ndo wa pumching bag, ndani ya nchi na nje!
Wakitoka wanakutana na Casa Blanca wakirudi ndani ndani wanakutana na tano, dah!
 
Azam na Yanga wametuabiasha kinoma uarabuni kupigwa 7
 
Maoni yangu:
1. Kwanza refa alituuma sana, kwa kutoa kadi ovyo na ku-call fouls ambazo hazina kichwa wala miguu. Inawezekana alishalambishwa. Mfano, binafsi zile penalti mbili si halali kabisa; ya kwanza mlinzi wa stars alichezewa vibaya kabla ya yule wa algeria hajazongwa na 'kuangukia' mwenyewe kwenye penalti box, haikuwa penalti kabisa. Halafu ile ya pili kipa wetu alitoka na kuupigampira pembeni mbele ya mshambuliaji wa Algeria, hakukuwa na nia yoyote mbaya ya rafu, lakini refa akawapa penalti, very sad
2. Umati wa washangiliaji wa Algeria na makelele yao vilikuwa very intimidating toka mwanzoni kabisa, Stars walijiona wapweke sana. Uzoefu ulihitajika sana hapa
3. Kitendo cha Stars kuruhusu goli la kwanza dakika ya kwanza kiliwachanganya sana stars wakaona kama wameshafungwa tayari. Laiti kama wangekomaa bila kufungwa walau hadi dk ya 10 Stars wengestabilize na kucheza vizuri zaidi
4. Kitendo cha kadi nyekundi kiliwanyongonyesha zaidi Stars wakaona biashara ndio imeisha! Of course hii ilitokana na Stars kufanya rafu za kizembe

Way forward:
- Hakuna wa kumlaumu, timu bado ni nzuri kama tulivyoiona ikicheza Dar. Sema tu Algeria ni timu bora sana na walikuwa nyumbani kwao na refa wao. Tuwatie moyo wachezaji wetu na benchi zima la ufundi. Hakuna cha ajabu kufungwa 7 na Algeria, hata Brazil walifungwa 7 tena kwao na Germany, itakuwa TZ ugenini?
- Kwa sasa waelekeze nguvu na mbinu katika kombe la Challenge linaloanza jumamosi; huko wahakikishe wanatoa vipigo vya haja kwa vibonde wenzetu ili kulinda heshima ya Tanzania.
- Nadhani kocha aanze kutafuta mbadala wa Cannavaro na Yondani, hawa wamecheza mda mrefu na inaelekewa kasi yao imepungua esp wakipambana na strikers wa kasi ya Algeria
 
Back
Top Bottom